Anguko lako mafanikio kwa wengine

Anguko lako mafanikio kwa wengine

nimechafukwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
290
Reaction score
237
Wadau kuna kipindi nilikua nafanya kazi kampuni fulani nikawa nalipwa laki 4 kwa mwezi sasa basi mkubwa wangu Akaja kuzingua anataka mshahara mkubwa wakati huo alikua analipwa 1m yeye anataka 2m basi Ile company ikaamua kuachana naye na mm nikapewa nafasi ya mkuu wangu na salary ya 2m nilishang'aa sana kwann hawakumpa yule boss wangu hyo hela wamenipa mm..basi baada ya mwaka na mm nikawa na kiburi nikajiona ni jembe hawawezi kuniachia basi nikaandika resignation letter nataka 3m ili nibaki...wakati huo kuna kazi nilikua nimepata ya salary ya 1.2m kwa hyo niliitumia kama chambo cha kutingisha kiberiti...sikuamini macho yangu pale mwajiri aliponipiga chini bila kutaka discussion akaletwa mrithi wangu akalipwa Ile 3m...na mm Sikua na lakufanya zaidi ya kwenda kwenye Ile kazi ya 1.2m....wakati mwingine nikiwazaga hichi kitu huwa naumia sana...je wadau nilikosea wapi?
 
Hukuona kilichomtokea mwenzako? Ukiona akinyolewa wewe tia maji
 
Ndio maana ikazaliwa methali "mtaka yote hukosa yote"

Aliona akikupandishia hiyo mil 3 na bado siku utataka akuongezee mil 4

Binadamu huwa haridhiki.
 
Ndio maana ikazaliwa methali "mtaka yote hukosa yote"

Aliona akikupandishia hiyo mil 3 na bado siku utataka akuongezee mil 4

Binadamu huwa haridhiki.
Na huyo aloletwa ipo siku atataka milion 4 hahah
 
Huu uzi kuna vingi vya kujifunza ila funzo Kubwa lipo kwako ww muajiriwa unaitwa mkuu, manager au Director kuwa kipi kilianza Kampuni au icho cheo chako? Kama jibu kampuni ndiyo iliyoanza basi unajukum la kufata taratibu za kudai stahiki. Pia, ktk nafasi za kuteuliwa kiungozi Kubwa tunaangalia insensitives (malupu malupu) wala siyo mshahara mana unaweza utendaji wako Kama meneja au mkuu Fulani unatengeneza mili 200 Kwa mwaka faida afu mshahara 3mil kumbe ungepewa malupu lupu ungejikuta Kwa mwaka umelipwa MIL 50 japo mshahara mdogo
 
Back
Top Bottom