NI mojawapo ya sala zenye kugusa mioyo ya watu wa dini mbalimbali. Huwa inasemwa kwa Kiswahili:
"Bwana nifanye niwe chombo cha amani yako" kwenye lugha yake ya asili Seigneur, faites de moi un instrument de votre paix
Dunia yetu hii ingekuwa na furaha zaidi na hata katika maisha ya kawaida tungekuwa na furaha zaidi kama kila mmoja wetu angejitambua kama "chombo cha amani" ya Mungu duniani. Kwa wanaokumbuka maneno ya Injili Yesu anapotoa ila sala ndefu kwenye Yohana 14 anasema hivi:
Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, amani niwapayo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo... (mstari wa 27). Sasa nikifanye commentary kidogo hapa nikuwa amani ya dunia hutolewa kwa vita, ugomvi, mapigano na ushindi. Kwamba yule anayeshinda anaamua terms of peace. Amani ya Kristu ni ile ambayo Mtume Paulo baadaye anaiita "Amani ya Mungu ipitayo ufahamu wote" (Phillipians 4:7).
Kumbe kutaka kuwa watu wa amani ni jambo jema sana, linatuliza mioyo na kama St. Francis anavyosema ukiwa chombo cha aina hiyo basi utaleta furaha penye huzuni, upendo penye chuki, n.k
Thanks Roullette.... kutukumbusha kutafuta amani hii mioyoni mwetu kwanza na kutoka hapo kuwafikishia wengine kama mfereji ububujikao amani katika bustani iliyojaa vurugu, chuki, hasira, kisasi, wivu, masimango, woga na zaidi ya yote husuda.