Angel? Devil? . . . .

i believe kuna luck na mtu anaweza kukupa mafanikio by encouragement au ushauri mzuri, but not random like kumjua fulani unapata good/bad luck. my best friend ni mlokole, he knows my secret and hakutetereka masomoni or something similar in fact he would even ask me to study 2gether na sote tulifaulu uhandisi with honor degrees.
 
Hiyo kitu ipo.Mtu anaweza kuwa ni Angel at the same time ni devil (mara nyingi bila kujijua)
Nilikuwa na rafiki yangu ni married. Alikuwa ananipenda sana na kunijali.Na kunisaidia kwenye mambo mengi..Lakn baadae akabadilika na kutaka kugegedana. Kwa akili zake yeye kunipenda kimapenzi ndio Kuimarisha upendo zaidi lakn kwangu ilikuwa ni ushetani.Ilifika mahali alikuwa na wivu sana kiasi cha kwamba asinione nikiongea na mwanaume yeyote anaweza anzisha varangati hata mbele ya watu.Kwa sababu zake eti analinda nisije rubuniwa au kuumizwa na watu wasiofaa.Hiii ilinisababishia kukosa marafiki.
 

Kongosho;
Nuru na giza havichangamani. You can prove this, kama Mungu akihitaji uhakikishe hili. As of recent, hata mimi mwenyewe nilikuwa sijui.
Nikaja kuona kitu muhimu zaidi kwenye imani ni kuwa kuna facts ambazo ziko kwenye belief lakini ni provable kwa baadhi/mtu fulani, ila proof yake haitumii scientific instrument na wala haifanyiki kwenye maabara kama hizi za kisayansi tunazozijua. Wewe kama Kongosho unaweza ukaonyeshwa kitu fulani na kikatokea, ukabisha ukasema pengine kimetokea kwa bahati mbaya, ukaletewa vingine hata kumi mfululizio mapaka pale ubishi wako utakapoisha. Ukishafikia kwenye stage ya namna hii, kwako wewe proof hizi ulizoonyeshwa zinakuwa siyo belief tena, ila ni FACTS. Lakini sasa kwa sababu zuimekuwa revealed kwako tu tena pengine ukiwa peke yako na katika mazingira ambayo mtu mwingine hawezi kuvishuhudia vikitendeka kwako, linapokuja swala la kuvishuhudia hivi vitu kwa watu wengine, unavishuhudia kama IMANI, ila kwako wewe unayevijua vilishabadilika kutoka kwenye IMANI na kuingia kwenye uhalisia, yaani FACTS. Mtu mwingine of course hawezi kukubaliana na wewe kwa sababu hana clues za kumfanya akukubalie. Vivyo hivyo na wewe kwa issue ambazo zimekuwa revealed kwa mtu mwingine ila si kwako, huwezi ukavikubali kama facts, sana sana utavichukua kwa imani tu basi.

Kwa hiyo napenda kukusisitizia kuwa NURU NA GIZA HAVICHANGAMANI, hii kwangu mimi ni FACTS, wewe chukua hii kwa imani, mwombe Mungu akusaidie kuibadilisha imani hii ninayokupa ili iwe FACTS na kwako pia. Siku njema sana.
 
Last edited by a moderator:

Malaika wa giza huwa wanakuja katika disguise ya nuru pia, inategemea na mazingira uliyopo na imani yako ilivyo kwa Mungu. Malaika wa shetani ni wa shetani, na wa Nuru ni wa Nuru, hakuna duality ya namna hiyo unayoeleza wewe hapa
 
refer to Yuda Iskarioti, alikuwa mmoja wa mitume wazuri wa Yesu but alichokuja kumfanyia bwana wake mwishoni, ulimwengu hauwezi sahau.
 
mtu anakuchota akili weeee anakulead weeee
anakusupport weeee
kumbe ni njia tu ya kufika kwenye nukta ya moyo wako ilipo UMUAMINI!AKUTENDE !
ipo sana tena kuliko maelezo!
angalia ni watu wangapi uliwaamini sana na ndio wamekuja kuwa mwiba katika maisha yako!
mh!
 
You are very brave, you deserved kufaulu

Hapa nachosema, ni kuwa mtu anakusaidia kabisa kufanikiwa, tena kwa juhudi zake zote
Lakini mtu huyo huyo anachangia maanguko yako mengi wakati mwingine bila hata yeye kujua
do you mean anakupa ushauri mbaya bila kukusudia?? ngoja nijaribu huu mfano kati ya friend A(likes drinking) na B(does not drink)
  1. A: twende bar kupata 1 moto 1 baridi
  2. B: sipendi pombe
  3. A: acha hizo, kidogo tu
  4. B: okay *wanenda bar*
  5. B: *after 3 bottles* nasikia kizunguzungu
  6. A: 3 tuu!! hebu ongeza, kuwa mwanaume
  7. B: sawa *ana0geza zingine*
  8. *B anapata hangover na kufeli test ya economics kesho yake*
  9. *A haelewi kwamba alimpa ushauri mbaya B. hakujua kama mwenzie hajazoea pombe na alimwacha alewe ingawa yeye mwenyewe hakulewa licha ya kunywa the same amount*
I experienced 1-5, 6-9 ni alternative ending to the scenario lakini haikutokea
 

Malaika wako hawezi kuwa shetani wako!
Giza na mwanga haviwezi kukaa pamoja. Kuhusu mafanikio yako kuwa anguko lako, ngoja nisimulie story niliyosimuliwa kanisani.
Huko China, kulikuwa na peasant mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwa watu as a means ya kujipatia kipato; amesota kwa kutembea nyumba hadi nyumba mpaka alipofanya saving na kununua Farasi, Farasi yule aliweza kumsaidia kuongeza idadi ya nyumba alizozihudumia hivyo kupata kipato zaidi (muda wa kutembea umepunguzwa); majirani wakampongeza kwa mafanikio yake; jibu lake lilikuwa "Baraka au Laana sijui". Siku moja farasi wake alipotea alivyokuwa ameenda kuchungwa, so akarudi kwenye kutembea kwa miguu; kama kawaida majirani zake ambao walikuwa wanafuatilia maisha yake, wakampa pole kwa kupotelewa na Farasi na kurudi kwenye shida ya zamani; again jibu lake lilikuwa "baraka au laana sijui". Baada kama ya mwezi hivi, farasi wake akaja kuonekana lakini akiwa na farasi wengine 5 ambao hawakuwa na mwenyewe (at least mwenyewe hakujulikana); so yule peasant akawa na jumla ya farasi 6, ambao wengine aliwakodisha na hivyo kipato chake kukua sana. Majirani kama kawa wakaja kumpongeza na jibu lake mnalijua, "baraka au laana sijui". Ikawa siku moja mwanaye akiwa anawachunga wale farasi, wakasala (as we say in kinyamwezi) na kumuangusha na kumvunja mguu kijana wa kiume wa yule peasant; majirani wakaja kumpa pole na kusikitika jinsi gani farasi wale wamekuja na balaa, you can guess jibu la yule mbaba "baraka au laana sijui". So kijana wa peasant ni kilema, na maisha yanaendelea; ikatokea vita ambapo vijana wote wa kiume walipaswa kwenda kupigana, na bahati mbaya katika kile kijiji hakurudi kijana yoyote, ila alibaki yule kijana wa peasant kwakuwa ni kilema hivyo hakwenda vitani.

Anyway ni story ndefu, na unaweza usione relevancy na mada yako; lkn kila kitu duniani kina consequences. Zinatofautiana tu uzito au ukubwa. Na mara nyingine tunaweza omba (sali) sana kupata kitu fulani na hatupati just because Mungu anajua madhara ya hicho kitu tukikipata hapo baadaye. "Who knows what would have happened if your prayer for better condition would have been answered?" T.B Joshua.

The devil, is there to snatch every good thing that we have or can get, au anaweza kutupa 'pride' au hata 'arrogancy' ili tuwakanyage wengine vichwani kwa blessing au mali tulizojaliwa nazo. Lakini kama ukimaintain presence ya angel basi atakulead blessings zako ziwabless wengine pia; challenge ni jinsi ya kumaintain uwepo wa huyo malaika au Roho Mtakatifu, wengi wetu tunakwama hapo.
 

Kumbuka shetani ni malaika , kabla hajawa shetani alikuwa malaika tena mwenye nguvu. Kwa hiyo anajua kujiegeuza geuza kama malaika ili akunase au akuingize matatizoni.
"ILA UNATAKIWA KUWA NA MACHO YA KIROHO ZAIDI KUGUNDUA HILI" :confused2::confused2:
 

I am interested kwenye hiyo kitu. LOL
 

Kwanzani kosa kuchaguliwa mchumba ambaye atakayekujak uwa mmeo/mkeo....!
mmeo/mkeo hutoka kwa MUNGU wa kweli ambapo unahitaji maombi kwanza ili yeyeaku patie huyo mmeo/mkeo.....!
 

Umenikumbusha Maruweruwe sasa wanasema Maruperupe duu mujini shule. Back to topic...Shetani wa mtu anatokea pale matendo yanapokuwa mabaya kwani mwenyekiti wa maovu ni shetani...Uangel wa mtu unakuja anapokutendea mambo mazuri kwani mungu anawatuma malaika kujaza baraka kwa binadamu (KIIMANI ZAIDI).
 
You are very brave, you deserved kufaulu

Hapa nachosema, ni kuwa mtu anakusaidia kabisa kufanikiwa, tena kwa juhudi zake zote
Lakini mtu huyo huyo anachangia maanguko yako mengi wakati mwingine bila hata yeye kujua

Toa mfano!
Usichanganye, conscious na subconscious state ya mtu. Kama mtu anatumia conscious state kufanya mema, anaweza kuchagua kutofanya mema pia; so huyo ni mtu
Kama anafanya kitu subconsciously basi anaweza kuwa led by roho au evil au holy.

lakini pia, usisahau wewe mwenyewe una mamlaka juu ya maamuzi yako mwenyewe; juu ya kushindwa na kushindwa.
 
Kaunga, story yako ina mantiki pia
'baraka ama laana'? Sijui

Huwezi jua hayo maanguko yangekuwa mafanikio, ningekuwaje pia.
 
Last edited by a moderator:

Ever heard the saying "it could have been worse"?, unajuaje kuwa mke ambaye ungemchagua wewe angekuwa sindano ya wanyama shingoni mwako badala ya mwiba unyayoni?

Wangapi wameoa the girls of their dream lakini mambo yakageuka kuwa tofauti?

Na wawezaje mlaumu say baba kwa uhakika na sio wewe mwenyewe labda umechangia mkeo kuwa mwiba?
 
Swali gumu, 'nitasara' bure
Ngoja nitafakari kwanza

 
Nimetoa mfano kwa hapo juu miwili


Au niseme in general, hujawahi ishi na mtu, ukitafakari highest achievement zako nyingi, kuna juhudi zake, na ukiangalia lowest score zako nyingi alishiriki pia?

Au hujawahi tafakari hilo?

Nimeusoma na nimekujibu. Kweli kuna watu ambao nilifikiri wamenikwamisha, na kwakweli ktk kipindi hicho they real did; lakini nilikuja kupata kitu au vitu baada ya kukwamisha ambavyo nakuja mshukuru aliyenikwamisha. Mfano halisi ni kwamba wengi wamejenga nyumba baada ya maudhi ya mwenye nyumba; wengi wameacha kazi na au kuanzisha shughuli zao au kutafuta kazi nyingine baada ya maudhi ya mabosi.

So mara nyingi, ktk kila kitu kibaya kinachonitokea (kuacha kufiwa) kuna positive outcome ambayo inanifanya sio tu nisilaumu bali nimshukuru Mungu kwa mapito niliyoyapitia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…