Angekuwa ndiyo Lowassa...

Acha kumfananisha lowassa na mambo kipuuzi
 
Lowasa angetendaje kama Magufuli? Yaan mwanasanaa atende kama mhandisi,swali la ajabu kabisa vile tu umesema mwenyewe unafikiri kinadharia basi sawa!
Yaani Magufuli ni mhandisi??? Toka lini mwalimu wa kemia akawa mhandisi??? Acha kutudhalilisha wahandisi mkuu
 
Ulipaswa ukae na ujiulize mwenyewe, ni wangapi waliosimama kidete kutetea safari za nje hovyo hovyo kuwa ziko na maslahi makubwa kwa taifa letu ni wakutoka chama gani na sasa wakiulizwa kuhusu safari za nje wanajibu nini?
 
Angekuwa na hajawa, hakuna haja ya kujisumbua, tutavuka daraja tukilifikia
 
Endapo nae angekuwa anawakandamiza wapinzan(ccm), anabana uhuru wa habari na kutoa matamko yasiyotekelezeka tukampinga kwa nguvu zote
 
swali lako liko nusu na linaweza lisijibiwe objectively.

try this one for size....

je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?
NA
je, watu wanamuunga mkono kila kitu rais Magufuli sasa hivi, pia wangemuunga mkono hivyo hivyo Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?
 
Upuuzi huo Lowasa asingekuwa nao kweli.
 
ooh hatujinyongi wala hatunywi sumu tutaisoma nambaa tutaisoma nambaaa ....ebu tuendelee kuimba choir masta dk pombe endeleza tuwimbo huu
 
Nyani Ngabu,

Binafsi sipingi anayofanya JPM, bali the way anavyofanya. It is unsustainable. There's no vision.

Kwa kiongozi yoyote anayejielewa na Mzalendo lazima angefanya anayofanya JPM, cleaning the house but at the same time you need the right system to carry on your legacy. Kesho na kesho kutwa akiingia nyang'au mwingine kama waliopita, nchi itarudi pale pale.

In short, we need a system to carry out his vision for the country. Not these light, camera, action moves. They won't last.

Mbio za sakafuni ...........
 
Sio fisadi. Maana aliwaambia wanaodhani ni fisadi wakashtaki mahakamani...je kunae aliyeenda kushtaki???? Bottom line!:, sio fisadi!
Kwahiyo mafisadi ni wale waliyoshtakiwa tu kama hujashtakiwa sio fisadi?
 

What kind of system do we need?

Can you elucidate more on it, please?
 
Nyani Ngabu,

You know better than that man. Hivi unapokuwa na mtumishi wa serikali au taasisi ya umma ambaye kipato chake hakimuwezishi kuwa kiasi X cha mali, kweli unahitaji executive branch ya nchi kutoa amri ya nini kifanyike? Takukuru, police, usalama wote hao wako wapi? Sheria ni msemeno, sio matamshi na press release zisizokuwa na mwisho.
 
Kuna kitu ambacho wachangiaji wengi hawajakiona hapa. Mazingira ya urais wa Lowassa yangekuwa tofauti kabisa na ya sasa (ya urais wa Magufuli) kutokana na kuwa na agenda tofauti. Kimsingi, kuna "variable" ingeongezeka: Lowassa angetawala chini ya Katiba ya Warioba; jambo linalofanya huu mlinganisho "hypothetical" kati ya urais wake na wa Magufuli kuwa batili. Ikumbukwe kuwa Lowassa aligombea urais akiungwa mkono na vuguvugu la Ukawa, na agenda yao kubwa ikiwa ni kupitisha Katiba ya Warioba mara moja. Na tofauti kubwa kati ya katiba ya sasa na ya Warioba ni kwamba, wakati katiba ya sasa inampa Rais Magufuli mamlaka makubwa yasiyohojika ya kiutawala, katiba ya Warioba ingemdhibiti "Rais" Lowassa kwa kuzipa uhuru na nguvu kubwa taasisi za kiutawala. (Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa katiba ya sasa ni mbovu na haitufikishi kokote).
 
Imkuu una maswali ya msingi mno
 
Nginana,
Well said mkuu. Ndio maana nikasema inachofanya serikali ya awamu hii ingetakiwa kiwekwe kwenye system badala ya hii mihemko ya kila kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…