Angekuwa ndiyo Lowassa...

Angekuwa ndiyo Lowassa...

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,099
Reaction score
136,709
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
 
Unanena kiMMM
 
Sasa hivi namba tunaisoma, huku watu wanafukuzwa kazi Kote serikalini na private, biashara haziendi, nchi haiwekezeki, hospitali hakuna dawa(chanjo Zinatafutwa kama tochi), kwenye Elimu vijana wananyimwa mikopo.
Ki ukweli watawala wajiangalie maana CCM tuliishaichoka matumaini yalikuwa kwa mtu na sio Chama, sasa na yeye Ndio Hali kama hii.
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
MKUU ukiona umeingia upinzani kazi yako ni kupinga tu hata kama ni zuri,Mie ni heri ninyamaze kuliko kukaa upinzani.

Kibaya zaidi siasa za tz zimejaa unafiki,watu wanatumia siasa kwenye kila kitu, hawaoni mazuri ya upande wa pili hata kidogo!
 
Lowasa angetendaje kama Magufuli? Yaan mwanasanaa atende kama mhandisi,swali la ajabu kabisa vile tu umesema mwenyewe unafikiri kinadharia basi sawa!
 
Angepingwa panapostahili pia angelaumiwa panapostahili kama ilivyo kwa JPM.Lakini tatizo JPM hana kipaumbele katika serikali yake,anaendesha nchi atakavyo na siyo inavyostahili.

Btw kwa vile ni nadhalia inawezekana Lowasa angefanya mabaya zaidi kuliko JPM,na angelaumiwa zaidi.
 
Hivi huu uozo anaousafisha mtukufu Rais, ulisababishwa au ulitoa chini ya utawala wa chama gani???? watu walewale walioasisi sehemu ichafuliwe ndo wanaoisafisha na bado wanataka wapongezwe kwa juhudi hizo.....
 
Back
Top Bottom