Angamizo

Feb 5, 2016
16
4
“Na nitakachomfanyia dada yako atakusimulia kesho, kama hajakusimulia utayaona machozi yake kwa mara ya kwanza katika maisha yako”

Jackson aliondoka kwa hasira.

Jackson hakumsimulia yeyote yule juu ya salamu zile za Faridu, alibaki kimya huku mara kwa mara akifikiria Faridu atamfanya nini Sabrina. Lakini hakupata jibu. Baada ya saa kadhaa Faridu alisahau kabisa kuhusu tishio la Faridu.

Alikuja kukumbuka tena juu ya tishio lile saa moja na nusu usiku. Sabrina alirudi nyumbani huku akiwa analia. Ilitokea kama bahati mbaya Jackson kutofatana na Sabrina kutoka shule. Ilitokea kama dharura na pengine hakulitilia maanani tishio la Faridu. Kilio cha Sabrina ndicho kilimkumbusha juu ya tishio la Faridu.

“Na nitakachomfanyia dada yako atakusimulia kesho, kama hajakusimulia utayaona machozi yake kwa mara ya kwanza katika maisha yako”

Na sasa Sabrina alirudi nyumbani huku akiwa analia. Alikuwa anayaona machozi ya Sabrina kama alivyoambiwa na Faridu.

“Faridu kanibaka!” Sabrina alisema huku akimkumbatia Jackson.
 
Back
Top Bottom