Angalizo; (picha ndani zinatisha) maajabu ya mazishi ya Tibet, Mongolia, China

Utachafua hali ya hewa..namna nzuri ya mazishi ni kuzikwa ardhini ili wale minyoo na funza wachukue madini na mbolea ya mwili mwako wapeleke ardhini na ardhi ipate rutuba ya kutosha ili kuifanya dunia iwe endelevu..yaani sustainable world.

Njia ya kuzika ni njia sahihi sana ili kuirecycle world Flora and
Fauna.

Dunia inarecycle kila kitu hii. Usichomwe utachafua hali ya hewa na ozone layer.
hakuna kinachopotea hata tai wanakufa na still nutrients zitapatikana tu kwa ajili ya mimea
 
Ningekuwa na uwezo ningelazimisha nikifa nipigwe kiberiti majivu yangu yakatupwe baharini nipotee kabisa, Masuala ya makaburi siyapendi basi tu hata nikisema bado watanizika nyumbani wananzengo!..
 
Niliishuhudia hii kwenye moja ya Frontline documentaries. Wao wanaita Mountain burial. Kimsingi inawekwa kiimani lakini suala kubwa hapo ni kwamba nchi yao ni milima na hawana sehemu za kuzikia kwahiyo inapendeza zaidi kuwapa maitii tai wale halafu ibakie mifupa tu ambayo haitaleta athari kiafya, maisha yanaendelea. Na kila mtu anajua akifa atapitia mkondo huo sawa tu na wewe utakayezikwa kwenye jeneza sijui la milioni ngapi au yule atakayechomwa moto. Ni mlolongo ule ule wa maisha, unazaliwa na ukimaliza safari yako unaondoka unapisha wengine
 
Mwanadamu anatakiwa kusitiriwa kwa kuzikwa ili tusirudi kwenye Cannibalism,kwa kumtupa maiti ili aliwe na Tai kutapelekea watu kutaka kuonja nyama.
 
Back
Top Bottom