Angalizo; (picha ndani zinatisha) maajabu ya mazishi ya Tibet, Mongolia, China

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,779
14,302
Maisha hayaishi kutufundisha mapya kila siku, Leo kuna jipya nimejifunza maishani tena. Kuna Mzee alikuwa mtu wa mtungi sana mtaani kafariki majuzi na awali alikuwaga muumini wa kanisa moja (sitalitaja) kwa sababu za kimaadili na utu. Baada ya kufariki church wakasema kwanza Mzee alianza kupiga monde na hakua anatoa Dhaka kanisani hivyo kanisa halitamzika maana halimtambui kama muumini wake halali. Wanandugu wakavurugwa ufahamu na akili mjadala nikauacha unafukuta wa kumuombea mzee azikwe na kanisa ili at least aende akiwa na Baraka za kanisa kwenye maisha ya milele.

Suala ili likanikumbusha aina za maziko kutokana na tamaduni mbalimbali Duniani zinavyotofautiana huku zingine zikiogofya na kuustajabisha zaidi..sikia hii..kule Asia nchi kama Tibet, Mongolia, baadhi ya sehemu za China wanazika kwa namna inayoitwa "sky burial" ikoje hii.

Iko hivi, punde tu baada ya kufariki marehemu anachukuliwa anachanwa na visu vikali sehemu mbali mbali za mwili wake hadi nyama za ndani zionekane kwa urahisi ili kuwaraisisha kazi wakamilisha ibada ya mazishi wale ndege Tai then anapelekwa sehemu waliopo ndege aina ya vultures (Tai) wala mizoga hawa then inafanyika ibada ya mwisho kwa kuwapa hawa tai waule ule mwili kama sehemu ya ibada ya kukamilisha safari yake ya peponi ikiaminika kwa kuwapa Tai basi roho ya mtu aliekufa itapelekwa hadi mbinguni kwa Mungu na mhusika atauona ufalme wa Mungu haraka na kwa uhakika zaidi sababu wao kwao wanaamini kwa vile Tai anaruka umbali mrefu zaidi angani basi atafika haraka kwa Mungu na pia wanaamini hawa Tai ni sehemu ya malaika wa Mungu wanaowasiliana nae kutokana na kukaribia mbinguni.

Then kwa namna nyingine kwao pia inakuwa ni kama sadaka kwa wale tai(Malaika) kupata chakula kizuri chenye madini na vitamini zote hapa Duniani.

Isitoshe watu wanasisitizwa kubakia na kushuhudia mlolongo mzima wa tai wakimla marehemu hadi aishe kabisa kama ishara ya kuukabili uoga juu ya kifo na kukiambia kifo hatukuogopi pia kufeel na kuapreciates ukweli wa kwamba maisha yetu kama binadamu sio permanent hapa Duniani hivyo watu wanasisitizwa kukaa Karibu sana na kushuhudia tukio zima hatua kwa hatua. Hatari sana!

Sasa nikiangalia hizi dhana mbili za mazishi wale Tibet wangesikia hii ishu ya huyu mzee kugomewa kuzikwa na kanisa na wao kama familia kuchanganyikiwa wangeshangaa sana maana kwao wao kwenda heaven ni simple sana ni kuwasusia tu maiti Tai then Tai wanabeba hadi kwa Baba juu. Ahahaha!! Hamna gharama za msiba wala nini, hamna kupigizana kelele za kuwasubiri ndugu walioko mbali..hamna kumbembeleza kasisi aendeshe misa ya mazishi...hamna gharama za sanda wala sanduku...its simple wape wale Tai, mtu anafika heaven hima hima.

Nikifa nikazikwe Tibet... Nataka kufika heaven faster kwa lift ya Tai.

Dunia ina mambo sana!
2E0EF32000000578-0-image-a-10_1446539732208.jpg
images-4.jpg
tumblr_mutbesNq251s1ktkdo2_r1_1280.jpg
1280px-Vulturesfeasting.jpg
2E0F034C00000578-0-image-a-8_1446539257511.jpg
2E0E7A9C00000578-0-image-a-2_1446539183526.jpg
 
Hakuna sehem wanachoma maiti hapa tz, ili nikifa nichomwee?
Utachafua hali ya hewa..namna nzuri ya mazishi ni kuzikwa ardhini ili wale minyoo na funza wachukue madini na mbolea ya mwili mwako wapeleke ardhini na ardhi ipate rutuba ya kutosha ili kuifanya dunia iwe endelevu..yaani sustainable environmental world.

Njia ya kuzika ni njia sahihi sana ili kuirecycle world's Flora and
Fauna.

Dunia hii inarecycle kila kitu hii. Usichomwe utachafua hali ya hewa na ozone layer.

Zikwa ardhini ili uwe recycled na kuwa mbolea ya Dunia ili Dunia iwe endelevu na yenye rutuba.

Mother Earth first.
 
Kuzika kunamaliza ardhi na pia kunachafua underground water kwa sababu karibia maiti zote lazima zichomwe ile dawa ya kuchelewesha kuoza hivo inaenda ku- contaminate underground water. Pia tunaharibu sana misitu kwa ajili ya kuchonga majeneza nk,Uchomaji wa wafu kwa gesi ni environmental friendly na kwa gharama nafuu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom