Angalizo kwa vyombo vya usalama dhidi ya EWURA

troiker

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
1,429
2,264
Ewura ni chombo cha serikali mahususi ku -regulate bei ya nishati nchini, pia chombo hiki kipo kwa mujibu wa sheria
.
Kabla ya hayati Magufuli kufariki mfumuko wa bei kwa kiasi flani ulitulia sana pamoja na changamoto nyingi ikiwemo gonjwa hatari la uviko-19.

Ghafla Ewura kwa sasa ni kama kuna ka kundi nyuma yake kamepenyeza rupia kwa ajili ya ku-maximize profite upande wa nishati, na kupelekea wananchi wa mwisho kama walaji kubeba mzigo mzito wa kupanda kwa bei ya bidhaa.

Hii inapelekea serikali kuchukiwa na wananchi na wengine wanasema mbona enzi za hayati hali hii ilikuwa nadra sana .

Nashauri serkali kuwafuatilia kwa kina watendaji wa Ewura, kwa siri na umakini mkubwa sana ,isije kuwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waminifu wameanza kuichezesha serikali mchakamchaka kiaina .

Napongeza kauli ya waziri Kalemani kutengua maagizo ya Ewura,ili kutoa nafasi kwa wadau kupitia upya hali halisi ya kinachondelea,kwani ukipandisha bei ya mafuta ,ni kupandisha bei ya bidhaa na anaeumia ni mlaji wa mwisho .
 
Lisemwalo lipo ,hapa ndio tutaelewa nani ni msada kwa watanzania wanyonge
 
Mkuu hapa angekuwepo Magufuli asingewachelewesha waendelee kuumiza wananchi harakaharaka hivi
Kabisa mkuu.

Jamaa alikuwa avumili ujinga ujinga kama huu as if hakuna serikali, kila kitu kinaenda shaghala bagala, mara TOZO halafu wanajistukia wanafuta, wanasema kuna corona ila wanajaza watu barabarani
 
Kabisa mkuu.

Jamaa alikuwa avumili ujinga ujinga kama huu as if hakuna serikali, kila kitu kinaenda shaghala bagala, mara TOZO halafu wanajistukia wanafuta, wanasema kuna corona ila wanajaza watu barabarani
Yule jamaa itanichukua muda mrefu sana kumtoa moyoni ,kifupi hakuwa na mzaha kwenye maslahi ya wengi ,hata uwe karibu naye
 
EWURA wanakula rushwa kwenye upandaji wa mafuta, wachunguzwe ikiwezekana bodi na mkurugenzi wao wapumzishwe kazi
 
Back
Top Bottom