Watumishi wengi sana wanalia kuwa majina yao hayapo kwenye orodha ya madeni na wana ushahidi wote kuwa wanadai. Angalizo langu natoa kwa zoezi linalokuja la kupandisha watumishi madaraja. Hili tatizo lisijitokeze tena. Hali ya sasa hivi hasa katika halmashauri nyingi haieleweki. Ndani ya halmashauri moja watumishi ajira mwaka mmoja lakini wako ngazi tofauti za mshahara. Sasa hivi kuna makundi mawili yamefungana na wote wanastahili kupanda mfano ajira 2012 na ajira 2013. Ili kuepuka kuzalisha madeni mapya mnapaswa kuwa makini sana.