Rais Samia anastahili pongezi kwa kuwajali Watumishi kwenye maslahi na vitendea kazi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Habari Wadau.

Moja ya sifa ya Kiongozi Bora ni yule anaewajali wale walio chini yake na anafanya kazi nao.

Kwa hili Rais Samia ameonesha Kwa vitendo Kwa kufanyafanyia mambo mazuri Watumishi wa Umma, Miongoni mwao ni kama ifuatavyo,

1.Salary increment hasa kima Cha chini, maposho na kupandisha madaraja.

2.Kufuta Ile riba haramu kwenye mkopo,hapa Mimi ni shahidi maana mwaka huu namaliza deni Bodi ya mikopo ambalo lingeisha miaka 3 mbele.

3.Ajira Mpya ambazo sio tuu zimewapa kazi jobless Bali zimeleta nafuu na kupunguza mzigo Kwa Watumishi,ameajiri zaidi ya Watumishi 55,000 na Bado anaendelea kuajiri.

4.Amelipa madeni mengi ya Watumishi,madai Yao nk,boss X alikaiku ukubwa miaka ya JK na Mwanzo wa Mwendazake,mwaka Jana kalipwa zaidi ya mil.60 za arears.

5. Ameimarisha mazingira ya Kufanyia kazi hasa ofisi nzuri kwenye kada mbalimbali na

6. Ameimarisha Vitendea Kazi Kwa Watumishi kama vifaa vya Kisasa maofisini eg huko mahospitalini, vishkwambi kwa walimu, magari Kwa idara na taasisi mfano pikipiki 2400 Kwa maofisa ugani, pikipiki 900 Kwa Watendaji Kata, ambulance zaidi ya 600, magari ya taasisi mbalimbali nk..

Kwa namna Rais anavyowapigania Watumishi wa Umma ni mtu wa ajabu pekee ndio atakuwa haoni haya..

Leo VP kazindua Magari zaidi ya 54 ya Tarura,soon Magari ya Wahandisi wa Umwagiliaji yatakabidhiwa Wizara ya Kilimo. Kiufupi mifano ni mingi sana.

Nampa kongole nyingi sana mheshimiwa, DktSamia sio kama wale waliokuwa na visingizio lukuki na propaganda na vitisho visivyo na msingi na kukejeli Watumishi. Ila Kuna wale wachawi watajifanya wamesahau haya miaka 2 tuu iliyopita
---
TARURA wakabidhiwa magari 54
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewaagiza watendaji wa kata na viongozi wa mikoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutumia vitendea kazi wanavyokabidhiwa na serikali katika kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasikiliza, kuwahudumia, kufuatilia miradi ya maendeleo na siyo kutumia kwa manufaa binafsi.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa TARURA pamoja na pikipiki 916 kwa watendaji kata, zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amewaagiza watendaji wa kata kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kwa kuhakikisha vikao na wananchi katika ngazi ya vijiji na mitaa vinafanyika kama inavyopaswa.

Pia Dkt. Mpango amewataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha shilingi laki moja inayopaswa kutolewa kwa Maafisa Watendaji wa Kata kama posho ya madaraka inatolewa kwa wakati na kupewa kipaumbele kabla hazijalipwa posho za vikao vingine vya halmashauri.
 
Hii ni mojawapo ya Hospital ya Wilaya ,unaweza ona vifaa tiba vilivyo safi na vya Kisasa.

Iko hivyo hospital zote za Wilaya
---
Halmashauri ya Mji Mafinga imepokea vifaa vya kutolea huduma kutoka TAMISEMI kwaajili yaJengo la dharura(EMD)lililopo katika Hospitali ya Mji Mafinga .

Serikali imejenga majengo 80 ya kutoa huduma za dharura nchini na yamekamilika ambapo kwa sasa Serikali imeanza kusambaza vifaa vya kutolea huduma katika majengo hayo.

Kwa Halmashauri ya Mji Mafinga jumla ya Shilingi milioni 300 zilipokelewa kutoka Serikali Kuu kwaajili ya Ujenzi wa Jengo la (EMD) Katika Hospitali ya Mji Mafinga ambalo limekamilika.

Jengo la dharura litasaidia kutoa huduma za haraka kwa wagonjwa wa dharura pamoja na kuboresha huduma katika Hospitali ya Mji Mafinga. Aidha, baadhi ya vifaa vya kutolea huduma katika jengo la dharura( EMD) Katika Hospital ya Mji Mafinga vimepokelewa kutoka TAMISEMI.

IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- MAFINGA

Sima Bingileki
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha. Mawasiliano Serikalini- Mafinga TC
 
Kote umezunguka,target yako ilikuwa hapa
hapana target yangu ni hapa
20230214_205614.jpg

TARURA wakabidhiwa magari 54

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewaagiza watendaji wa kata na viongozi wa mikoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutumia vitendea kazi wanavyokabidhiwa na serikali katika kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasikiliza, kuwahudumia, kufuatilia miradi ya maendeleo na siyo kutumia kwa manufaa binafsi.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi magari 54 kwa TARURA pamoja na pikipiki 916 kwa watendaji kata, zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Amewaagiza watendaji wa kata kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kwa kuhakikisha vikao na wananchi katika ngazi ya vijiji na mitaa vinafanyika kama inavyopaswa.

Pia Dkt. Mpango amewataka Wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha shilingi laki moja inayopaswa kutolewa kwa Maafisa Watendaji wa Kata kama posho ya madaraka inatolewa kwa wakati na kupewa kipaumbele kabla hazijalipwa posho za vikao vingine vya halmashauri.
 
Ni lini maslahi ya watumishi yaliboreshwa?

Kuna siku mtakuja kulaaniwa na kauli zenu za kukejeli watumishi wa umma wa nchi hii ambao kutwa kuchwa wamepauka usoni kwa hali ngumu ya maisha kutokana na maslahi duni muwapayo.
 
Wewe ndio utalaaniwa,hayo niliyoeleza hapo yamefanyika aunhayajafanyika?
 
Back
Top Bottom