Kama Igunga, hapo CCM ipeleke majembe yake yote, Mwigulu, Nape, January na Lusinde aka kibajaji, jimbo linakwenda CCM.
Haaaaaaa Mtaji wa kafu unanichekesha sana lol,ngoja tuone KGM kusini wana mtaji gani?
Mwigulu tupe raha wana CCM tena kama ulivyo wabutua wale mgambo Igunga wakatoka Igunga kimya kimya na safari hii fanya vile vile!
kwa mujibu wa Tendwa..uchaguzi mdogo hutumia bilion19 hadi 20 mbali na Vyama husika kutumia gharama zao! so ni zaidi ya billion 20 Mkuu!Mabilioni ya pesa inaenda kuteketezwa tena kwenye kajimbo kamoja tu! Masikini Tanzania yangu!
Ni kweli kabisa CDM wanaweza kushinda bila Kafulila lakini kwenye Vita ni lazima ujihami sana kwani sheria zetu zinasema ukishindwa kwa kula moja bado umeshindwa sasa kwa nini kukataa kula ya Kafulila ambaye ni Mpinzani kama Chadema?.Suala la tofauti kimutizamo lipo kila mahali na ndio maana ya vyama vya upinzani?Vyama vingi vinatokana ni mitizamo mingi ya upinzani na sio mitizamo ya kuunga mkono CCM!Kule Kenya Kibaki na Odinga hawaelewani Kimutizamo lakini wote hawa ndio wameingusha KANU chama tawala ambacho kilikuwa na nguvu kuliko CCM.We angalia CCM pamoja na kumutukana Rostamu Aziz hawakuwa tayari kupoteza kura yake .Leo Mbatia katangaza kwenda kumuona JK kuhusu Katiba mbinu ni hiyo hiyo CCM inataka kuhifadhi kura zote za NCCR kigoma kusini.Kule Igunga kulikuwa na ndoa kati ya CCM na CUF lakini Kigoma kusini kuna ndoa ya NCCR na CCM!Kama ulimusikiliza Mh Agripina Buyogera ana sema yeye na Mbatia walizunguka sana na Mbatia huku Agripina akimutelekeza mume wake kuhakikisha majimbo yote yanakuwa NCCR ,lakini akaogopa kumalizia kuwa fedha za kuzungukia zilitoka CCM!!.Ukweli Mbatia ni Injinia wa Maji ,hafanyi kazi sasa alipata wapi fedha za kuzunguka na mke wa mtu wakati NCCR haina ruzuku na Mbatia hana Kazi??CDM wataibuka kidedea Kigoma kusini hata bila ya Kafulila
Sio lazima kafulila arudi chadema, kumbuka alivyoondoka kwa dharau na kiburi, mi napendekeza kafulila kama anaipenda chadema kweli aombe radhi cdm na cdm isimpe nafasi yoyote ya uongozi kwa sasa, impe nafasi ya kuwa mwanachama tu.
Kafulila toka amekuwa mbunge umaarufu wake jimboni umekuwa ukiporomoka kwa kasi sana kwani muda wote alikuwa akipanga mikakati yao na zitto, nimeongea na wafanyabiashara wengi tu wanao tokeo jimboni kwake na walinieleza kuwa kafulila amewabadilikia.
Pia cdm ina hazina kubwa ya watu wenye uwezo wakutosha kugombea huo ubunge na sio lazima tumtumie huyo kafulila au huyo mgombea wa mwaka jana, kwanza kwa kufanya hivyo tutakuwa tunampa kichwa zaidi na hakika hataacha tabia zake uasi, bila kupata adhabu kidogo hatojifunza.
Mwigulu tupe raha wana CCM tena kama ulivyo wabutua wale mgambo Igunga wakatoka Igunga kimya kimya na safari hii fanya vile vile!
Mwenye matokeo yaliyopita kigoma kusini atupatie tuanze na tathmini
CCM------
CHADEMA____
NCCR______
Candidate | Political Party | Number of Votes | Percentage Votes |
KAFULILA DAVID ZACHARIA | NCCR-MAGEUZI | 23,162 | 40.34 |
KIFU GULAMHUSSEIN SHABANI | CCM | 20,367 | 35.47 |
MUSLIM HAIDERALI RAJABALI | CHADEMA | 7,676 | 13.37 |
OPTATUS BEDA LIKWELILE | CUF | 3,468 | 6.04 |
AZIZI HASSANI MOHAMED | CHAUSTA | 491 | 0.86 |
FILIPO JOHN FUMBO | DP | 345 | 0.6 |
SELEMANI SAIDI MSANU | JAHAZI ASILIA | 310 | 0.54 |
MVANO RASHIDI RAMADHANI | NRA | 58 | 0.1 |
MWAJUMA MALIKI ATHUMANI | UPDP | 57 | 0.1 |
MWITO JUMA KHAIRALLAH | SAU | 57 | 0.1 |
ZABIBU MRISHO KALIZA | UMD | 52 | 0.09 |
SPOILT VOTES | 1,376 | 2.4 | |
TOTALS | 57,419 | 100 |
**** weweKafulila kuwa mpole na ikiwezekana rudi ccm kwan hata iweje ccm inaenda kuongeza jimbo hlo halina ubish cdm ni kanda ya kaskazin,mi naamin waha wapo makin sana na kuriludisha jimbo nyumban
Hivyo vyama vingine ni vipi hivyo unaweza taja hata kimoja.CDM NI CHAMA KIKUU CHA UPINZANI LAKINI BILA KUWA NA NGUVU YA UMOJA NA VYAMA VINGINE HALI INAWEZA KUWA MBAYA.KULE IGUNGA BILA MPASUKO WA CCM CDM ISINGE SHINDA. Kuimarika CDM KUNATOKANA NA MPASUKO WA VYAMA VINGINE.