zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,835
Wakati nakua nimekuwa nikisikia watu wanasema Tanzania ni nchi yenye amani..
"kisiwaCha Amani Duniani"
Juzi tu nimesoma ripoti inayonesha nchi ambazo watu wake hawana furaha...
Angalia Hii.
Ripoti ya utafiti wa Viwango vya Furaha Duniani 2016 ambayo hutolewa kila mwaka na shirika la maendeleo endelevu (Sustainable Development Solutions Network (SDSN)) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa, imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kwenye orodha ya nchi zenye furaha.
Utafiti huo ulitumia vigezo vya pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi, kuwa huru dhidi ya ufisadi, na ukarimu miongoni mwa jamii.
Kitu kilichowashangaza wengi ni Tanzania kuzidiwa na nchi mbalimbali ambazo ziko katika vita na machafuko ama zikikabiliwa na baa la njaa ikiwemo Somali ambayo imeshika nafasi ya 76 huku Tanzania ikishika nafasi ya 149 kati ya nchi 157.
Mbali na Tanzania, nchi nyingine Kumi zilizoko kwenye orodha hiyo ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria, na Burundi ambayo imekuwa ya mwisho.
Ripoti hiyo iliyotolewa Mjini Roma nchini Italia siku tatu kabla ya Dunia kuadhimisha siku ya furaha duniani (Machi 20), imeitaja Denmark kuwa nchi inayoongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha zaidi duniani.
Zipo baadhi ya nchi ambazo tayari zimeteua mawaziri wa ‘Furaha’ ikiwemo Venezuela. Waziri wa Furaha hushughulika kuhakiksha wananchi wanaongeza furaha kila siku.
Hizi ni nchi 10 zenye furaha zaidi duniani:
1. Denmark
2. Switzerland
3. Iceland
4. Norway
5. Finland
6. Canada
7. Netherlands
8. New Zealand
9. Australia
10. Sweden
Leo tena naangalia hapa ripoti ya nchi zenye amani Tanzania ipo nafasi ya 52 duniani...
Orodha ya hizo nchi zenye amani duniani 2020 hii hapa;
1.Iceland
2.New Zealand
3.Portugal
4.Austria
5.Denmark
6.Canada
7.Singapore
8.Czech Republic
9.Japan
10.Switzerland..
Hizi taarifa zinanipa wasiwasi na utata mkubwa...
Hivi kweli nchi yetu haina furaha na amani..
Au ni tafiti zenye biasness na kutaka kuwachefua watanzania na Afrika kwa ujumla..??