Angalizo: Kumbe tulidanganywa kuhusu nchi zenye furaha duniani

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,563
2,000
Wakati nakua nimekuwa nikisikia watu wanasema Tanzania ni nchi yenye amani..

"kisiwaCha Amani Duniani"
Juzi tu nimesoma ripoti inayonesha nchi ambazo watu wake hawana furaha...

Angalia Hii.

Ripoti ya utafiti wa Viwango vya Furaha Duniani 2016 ambayo hutolewa kila mwaka na shirika la maendeleo endelevu (Sustainable Development Solutions Network (SDSN)) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa, imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kwenye orodha ya nchi zenye furaha.

Utafiti huo ulitumia vigezo vya pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi, kuwa huru dhidi ya ufisadi, na ukarimu miongoni mwa jamii.

Kitu kilichowashangaza wengi ni Tanzania kuzidiwa na nchi mbalimbali ambazo ziko katika vita na machafuko ama zikikabiliwa na baa la njaa ikiwemo Somali ambayo imeshika nafasi ya 76 huku Tanzania ikishika nafasi ya 149 kati ya nchi 157.Mbali na Tanzania, nchi nyingine Kumi zilizoko kwenye orodha hiyo ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria, na Burundi ambayo imekuwa ya mwisho.

Ripoti hiyo iliyotolewa Mjini Roma nchini Italia siku tatu kabla ya Dunia kuadhimisha siku ya furaha duniani (Machi 20), imeitaja Denmark kuwa nchi inayoongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha zaidi duniani.

Zipo baadhi ya nchi ambazo tayari zimeteua mawaziri wa ‘Furaha’ ikiwemo Venezuela. Waziri wa Furaha hushughulika kuhakiksha wananchi wanaongeza furaha kila siku.

Hizi ni nchi 10 zenye furaha zaidi duniani:

1. Denmark

2. Switzerland

3. Iceland

4. Norway

5. Finland

6. Canada

7. Netherlands

8. New Zealand

9. Australia

10. Sweden

Leo tena naangalia hapa ripoti ya nchi zenye amani Tanzania ipo nafasi ya 52 duniani...
Orodha ya hizo nchi zenye amani duniani 2020 hii hapa;
1.Iceland
2.New Zealand
3.Portugal
4.Austria
5.Denmark
6.Canada
7.Singapore
8.Czech Republic
9.Japan
10.Switzerland..

Hizi taarifa zinanipa wasiwasi na utata mkubwa...
Hivi kweli nchi yetu haina furaha na amani..
Au ni tafiti zenye biasness na kutaka kuwachefua watanzania na Afrika kwa ujumla..??
 
Sethshalom

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
443
1,000
A researcher finds data to suit his/her objectives. Sasa huyo mzungu alieandaa hiyo report alitumia sample gani kwa Tanzania kwa mfano?? Issue ya furaha ni relative not absolute and ni multidimensional with culture as one of the components. To me the report is useless and fully biased
 
Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,391

Si ujifunze kujua dhana (conceptual framework), mbinu (methodology) na viashiria (indicators) zinazotumika kupata matokeo ya utafiti husika badala ya ku-bash jambo usilolijua?
 
ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,156
2,000
Umejichanganya amani na furaha ni vitu viwili tofauti unaeza kuwa na amani usiwe na furaha na unaeza usiwe na furaha ukawa na amani.
 
Sethshalom

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
443
1,000
Si ujifunze kujua dhana (conceptual framework), mbinu (methodology) na viashiria (indicators) zinazotumika kupata matokeo ya utafiti husika badala ya ku-bash jambo usilolijua?
Who did the report???? Mtu anafanya research to fit ,defend his objectives. Hii ni social science where all biases can apply, there is no scientific laboratory to test this and prove it.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,568
2,000
Wakati nakua nimekuwa nikisikia watu wanasema Tanzania ni nchi yenye amani..
"kisiwaCha Amani Duniani"
Juzi tu nimesoma ripoti inayonesha nchi ambazo watu wake hawana furaha...

Hizi taarifa zinanipa wasiwasi na utata mkubwa...
Hivi kweli nchi yetu haina furaha na amani..
Au ni tafiti zenye biasness na kutaka kuwachefua watanzania na Afrika kwa ujumla..??
Mkuu Zagarinojo, kuwa kisiwa cha amani ni jambo moja na kuwa na furaha ni jambo jambo jingine.

Tanzania ni kisiwa cha amani kiukweli
P
 
zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,563
2,000
Mkuu Zagarinojo, kuwa kisiwa cha amani ni jambo moja na kuwa na furaha ni jambo jambo jingine.

Tanzania ni kisiwa cha amani kiukweli
P
Kwani vitu vinavyoleta furaha ni vipi!
Sitegemei Congo kuwa na Furaha ingali haina Amani!
Amani nadhani ndio huleta furaha
 
Aridhi tukufu

Member
Aug 10, 2020
24
45
A researcher finds data to suit his/her objectives. Sasa huyo mzungu alieandaa hiyo report alitumia sample gani kwa Tanzania kwa mfano?? Issue ya furaha ni relative not absolute and ni multidimensional with culture as one of the components. To me the report is useless and fully biased
Weka za kwako kupinga,acha mdomo kasuku bila matendo. Mbona zz Twaweza hamzitaki
 
THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,205
2,000
Ila Utajiri unaleta furaha kwa njia ipi kwasababu Marekani na China sijaziona kwenye list ni nchi tajiri duniani..!
Umeziona hizo tuu eee, nchi za nods zina watu wenye furaha kwa sababu RAIA wake wana pesa.

Note. China. Siyo nchi tajiri.
 
Aridhi tukufu

Member
Aug 10, 2020
24
45
Mkuu Zagarinojo, kuwa kisiwa cha amani ni jambo moja na kuwa na furaha ni jambo jambo jingine.

Tanzania ni kisiwa cha amani kiukweli
P
Mayaloa,hapa napingana na wewe. Amani huleta furaha kwa kuwa huru kuamua Mambo yenu kwa pamoja ndio humfanya mtu kujisikia ni miongoni mwa kinachofanywa na hivyo kuwa na furaha
 
zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,563
2,000
Umeziona hizo tuu eee, nchi za nods zina watu wenye furaha kwa sababu RAIA wake wana pesa.

Note. China. Siyo nchi tajiri.
China siyo tajiri kivipi na wakati ndio most industrialized county in the world..
Na Kama ni most industrialized county inamanisha it has equal balance of payment
Yaani more exports than imports within a year..if its more industrialized it means ajira zinapatikana kwa wingi so the circulation of money inaongezeka na wealth is generated among people
 
Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,019
2,000
Natamani kuzitembelea nchi za Scandinavia naona zipo na furaha sana.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,837
2,000
Wakati nakua nimekuwa nikisikia watu wanasema Tanzania ni nchi yenye amani..

"kisiwaCha Amani Duniani"
Juzi tu nimesoma ripoti inayonesha nchi ambazo watu wake hawana furaha...

Angalia Hii.

Ripoti ya utafiti wa Viwango vya Furaha Duniani 2016 ambayo hutolewa kila mwaka na shirika la maendeleo endelevu (Sustainable Development Solutions Network (SDSN)) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa, imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kwenye orodha ya nchi zenye furaha.

Utafiti huo ulitumia vigezo vya pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi, kuwa huru dhidi ya ufisadi, na ukarimu miongoni mwa jamii.

Kitu kilichowashangaza wengi ni Tanzania kuzidiwa na nchi mbalimbali ambazo ziko katika vita na machafuko ama zikikabiliwa na baa la njaa ikiwemo Somali ambayo imeshika nafasi ya 76 huku Tanzania ikishika nafasi ya 149 kati ya nchi 157.Mbali na Tanzania, nchi nyingine Kumi zilizoko kwenye orodha hiyo ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria, na Burundi ambayo imekuwa ya mwisho.

Ripoti hiyo iliyotolewa Mjini Roma nchini Italia siku tatu kabla ya Dunia kuadhimisha siku ya furaha duniani (Machi 20), imeitaja Denmark kuwa nchi inayoongoza kwa wananchi wake kuwa na furaha zaidi duniani.

Zipo baadhi ya nchi ambazo tayari zimeteua mawaziri wa ‘Furaha’ ikiwemo Venezuela. Waziri wa Furaha hushughulika kuhakiksha wananchi wanaongeza furaha kila siku.

Hizi ni nchi 10 zenye furaha zaidi duniani:

1. Denmark

2. Switzerland

3. Iceland

4. Norway

5. Finland

6. Canada

7. Netherlands

8. New Zealand

9. Australia

10. Sweden

Leo tena naangalia hapa ripoti ya nchi zenye amani Tanzania ipo nafasi ya 52 duniani...
Orodha ya hizo nchi zenye amani duniani 2020 hii hapa;
1.Iceland
2.New Zealand
3.Portugal
4.Austria
5.Denmark
6.Canada
7.Singapore
8.Czech Republic
9.Japan
10.Switzerland..

Hizi taarifa zinanipa wasiwasi na utata mkubwa...
Hivi kweli nchi yetu haina furaha na amani..
Au ni tafiti zenye biasness na kutaka kuwachefua watanzania na Afrika kwa ujumla..??
Ni kweli ukienda nchi hizo halafu ukarudi nyumbani ndio utagundua kuwa watu wanaishi kama mashetani nchi za Afrika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom