Angalizo: Chadema nunueni magari ya Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo: Chadema nunueni magari ya Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, May 5, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ushauri wangu ni kuwa chadema myanunue magari hayo tu mpaka yatapopitia kwenye hatua zifuatazo:
  1. yathaminiwe na msamini ambaye ni independent.
  2. yapitie kwa dealer wa magari hayo ili kujua uzima wa magari hayo.

  hayo yote yakishafanyika na kujiridhisha munaweza kununua kwa kuwa tayari mlishakuanza kuyatumia nayo pia inaweza kuwapa picha nzuri kama yanafaa na kwa kuwa mnanunua yote kwa wakati mmoja uenda mbowe akawapa hapo discount ambayo hamuwezi kupata sehemu nyingine.

  kuhusu ufisadi:
  hakuna ufisadi hapa kwani magari yanafahamika ni mitumba na wenyewe chadema ndio walikuwa wakiyatumia, ufisadi ungewepo tu endapo mbowe angejaribu kusema kuwa magari ni mapya huku akijua sivyo kama ambavyo ccm wamekuwa wakifanya kumbuka Pantoni ya kigamboni(m.nyanganyi),ndege za ATC, MITAMBO YA DOWANS yote hii ilikuwa mitumba tena mibaya lakini iliitwa mipya, huu ndio ufisadi.
  kununua magari ya mitumba siyo jambo baya kwa hali ya chama kama chadema ambacho bado akijawa na uwezo mkubwa wa kifedha ukilinganisha na serikali. La msingi hapa ni ubora wa mtumba unaonunua na pili bei unayonunulia huo mtumba kwani asilimia kubwa ya watanzania wanaendesha magari ya mitumba na yamekuwa yakiwasaidia.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unachosema kinaweza kufanyika na kweli kinahitaji kufanyika. Lazima kuwa na a sense of independent examination and valuation. Lakini kwangu mimi kunabaki ishu ya ETHICS. Chama hakiwezi kununua vifaa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama. Hata kama mkifanya process iwe wazi kwa namna gani, kumbuka kuwa huyu mtu bado ana influence. Ni sawa na director wa kampuni au CEO kuuzia kampuni vifaa. Hii hairuhusiwi kisheria kabisa. Ni kwa namna hii ndio ufisadi unaanza.
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo linakuja hata kama tathmini itafanyika kwenye huo mchakato wa tathmini na Mbowe atakuwepo.

  Wewe uliona wapi mtu mathalan kwenye kampuni unafanya kazi hapo hapo halafu unatoa humuda ya usafiri!! huwa haitakiwi

  Kiutaratibu si sahihi , Chadema watangaze tenda kama mbowe anaweza na yeye ajitose a BID!
   
 4. h

  hoyce JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Chama kimeyatumia tangu yakiwa mapya, bure, kinayajua. Baada ya uchaguzi hakikuyarudisha, kimeendelea kuyatumia (yamekuwa mitumba kwa sababu wameyatumia wao), kwa nini kimwachie mtu mwingine kuyanunua?
   
 5. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Tumeambiwa kuwa magari haya Mhe. Mbowe aliyatoa kwa ajili ya Kampeni za Uchaguzi 2010 tayari CDM wameyatumia na bado yanatumika.
  Kwa hiyo kuyanunua haya magari ni sawa kabisa. Nothing is wrong here! Wanaopinga wanataka yapelekwe wapi? Acheni porojo baana.
   
 6. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono kwa hoja yako ya CDM kununua magari hayo ya mtumba kwa sababu;

  • CDM bado ni chama kichanga na hakiwezi kununua magari mapya ambayo yatakidhi mahitaji ya wakati huu ambapo magari mengi zaidi yanahitajika.
  • Sheria ya manunuzi haivibani vyama vya siasa na hivyo ni halali, na sio ufisadi kununua magari ya mitumba. Suala la ufisadi ni mbinu inayotumia na baadhi ya viongozi wetu kama mtaji wao wa kisiasa.
  Narudia tena, CDM wanunue magari ya mtumba yanayotosheleza mahitaji na wasiwaige Chama Cha Magamba ambao walionunua magari ya kihindi yasiyo na uwezo wa kukidhi mahitaji!?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Nakuunga mkono mkuu, besides hata Tanzania kila kitu ni mtumba. hata leadership ngazi zote zimekaa kimtumba mtumba
   
 8. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi wana CHADEMA nani anaweza kumlipa Mbowe pesa na nguvu alizotumia kwa CHADEMA?Mbowe ametumia mali zake bila kujali atalipwa na nani na hakika bila Mbowe kusingekuwa na CHADEMA LEO kumbukeni nyie mnaobeza kila asemalo Mbowe ni wehu ALIKUJA NA SERA YA KUTUMIA CHOPPER 2005 MKASEMA SANA.Hauwezi mfananisha Mbowe na yeyote ndani ya CHADEMA kwani hata Zitto anajua.KAMA SIYO UTAJIRI WA MBOWE KUSINGEKUWA NA CHADEMA YENYE NGUVU LEO
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hayo tunakubali, lakini lazima ujue ethics za kazi. CEO hawezi kuuzia kampuni vifaa. Sawa katoa magari yatumike wakati wa kampeni. Ni vizuri na tumpongeze. Lakini kuuzia chama magari? Ivi where do you draw the line with such behavior? Ivi kweli si mwingine anaweza akawa ananunua magari wakati wa kampeni kwa kusudi la kuuzia chama kampeni zikiisha? Tunajuaje Mbowe hakufanya hivi? Lazima chama kichore mstari. Namna hii ndio ufisadi unavyoanza!!
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata kwenye tenda hatakiwi ku-bid! Hii ni simple ETHICS za kazi. Ivi mnadhani ufisadi ccm ulianzaje? Mmeambiwa kuwa UFISADI ni CANCER. Unadhani cancer inaanza kwa mlipuko mmoja? Ndio hivi ivi inaanza. Mmoja atapewa tenda, mwingine atafanya hivi. Mwisho wa siku mtashindwa kunyosheana vidole na kwa kuwa wote mmehusika!
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  You have missed the point mkuu. Chama sio Mbowe. Hata kama angetoa roho yake kwa ajili ya Chama, haina maana tufanye vyote atakavyo! Kuna ETHICS za kazi na zinahitaji kufuatwa. Inaelekea ETHICS ni tatizo la jamii ya Tanzania!
   
Loading...