Angalieni Star tv live NOW!

Angalieni Star tv live NOW!

Nishashududia mtu anakuf kwa kutopelekwa hospital mpka ikawa too late eti wanamwambia aombe tuu. Mwingine ameambiwa asimshitaki mdeni wake polisi. Yaani hawa jamaa story zao ni kama mchezo wa kuigiza lakini ndo wanafanya kweli.
Mbali na majina yao maa. Mamlaka , sijui utukufu. Na jamaa marehemu Munuo aliwaambia alishamuua shetani tangu 2008 so wanakula bata tuu kusubiri kuingia Paradiso. Hawa jamaa ni shida
 
Taratibu tu mtaelewa kwamba Hakuna apasaye kuabidiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja, mtukufu, muumbaji na hana mshirika ambaye Sisi waislam tunamwita Allah...Muumba wa mbingu,ardhi Na vilivyomo.Hajazaa,hajazaliwa Na wala Hakuna anaefanana nae.Mtaelewa tu kwa sababu hata mtoto mdogo wa chekechea ukimwambia Kuna Mungu baba,Mungu Mwana Na roho mtakatifu yaani mtoto unamchanganya sana na anaona mauza uza tu kwasababu hata akili ya kitoto inakataa.Lakini mtoto Huyo Huyo ukimwambia Kuna Mungu mmoja tu Mkuu na Muumbaji wa vyote hapa mtoto atakulewa haraka sana Na pia mchunguze hata mwanao kaa nae Afu muulize anamjua Vp Mungu,atakachokujibu moja kwa moja utagundua mtoto yeyote wanamtambua Mungu katika "Umoja" wake kwa sababu kiasili iko hivyo na atakujibu hivyo kwa sababu ndiyo ukweli wenyewe japo kwa kufuata matango poli ya wazazi wake mtoto habadilishwa Imani yake kwa influence ya wazazi....ila kimoyo moyo kila mtu anaamini Mungu Ni Mmoja tu Na si watatu.

Povu ruksa...ila kimoyo moyo tunakubali.
 
Wanavaaga nguo nyeupe tuu ktk kuabudu.
Hawa jamaa huwaambii kitu. Mimi ni mkristo lakini hawa jamaa hawafai hata kidogo. Kuna ugomvi ulitokea ktk familia moja hapo tegeta. Yaani Munuo kabla hajafa alitangaza mbele ya kanisa kuwa amepata maono ya nani wa kuamuachi kanisa endapo akifa. Akampata jamaa mmoja mwenye juhudi ambae alikuwa msaidizi hapo kanisani. Jamaa alikuwa msomi mwenye kazi yake. Sasa ili amshawishi awe full time hapo kanisani ikabidi amwambie aache kazi na achome vyeti vyake vyote ili atumike vuzuri kanisani. Hii ikaleta mtafaruki ktk familia ya yule jamaa sana. Lakini mwishowe jamaa aliacha kazi na kuchoma vyeti vyote. Munuo alipofariki jamaa akashika kanisa lakini ukaibuka mgogoro wa kimaslai kati ya jamaa na mke wa Munuo akidai kuwa yeye ndo anatakiwa aendeshe kanisa. Sijui mgogoro wa o uliishia wapi
Mkuu ule mgogoro kama kumbukumbu zangu zitakuwa sawa mpaka serikali ilitishia kulifunga hili kanisa lakini kilichotokea ni kugawanyika kwa kanisa so kunasiloam church za aina mbili wapo wanaomfata mke wa marehemu na wengine wanamfata sijui ni nani
 
anasema kiongozi wao alinyakuliwa kama Yesu,anavilaumu vyombo vya habari havikurusha lile tukio na wengi hawakubali huu ukweli kua yule kiongozi wao Adam Elia wa pili alinyakuliwa
Imani zingine huwa ni magereza ya fikra bila kujua
 
Hivi hizi jumuiya za Kikristo hazina wajibu kufuatilia vitu basic kama hivi? Tofauti za madhehebu zipo lakini huwezi kujiita Mkristo huku ukiamini Yesu si Mungu! Huku hujui Yesu ni Mungu kweli na mtu kweli!
Huo ndo uhuru wa kuabudu usiwapangie kila mtu na imani yake
 
Huyu jamaa Na lisauti lake ni wapotoshaji.
Kuna mchagga mmoja ndiye aliyeanzisha hilo kanisa hapo Mbezi Beach wao ndio Wana mregard kama Yesu. Huyo Mchagga ndio wanamuita Elia Adam wa pili.
Jamaa alikufa miaka kadhaa nyuma wakaanza kusambaza uzushi eti ameonekana akipaa Huko Bagamoyo
Kweli hata mimi nilisikia hii story
 
Hawa jamaa kila jumapili wapo live star tv.

Nauliza tu kwa nia nzuri, je kurusha matangazo mubashara kwa muda wa zaidi ya saa 1 je kuna gharama kubwa? hawa jamaa je ni sadaka pekee au kuna mfadhili?
 
Halafu hii Tabia ya watumishi wa Kiroho kutembea na watu nyuma sijui wameitoa wapi yaani mtu anasimamiwa nyuma kama mgonjwa wa kifafa.
ni mfuasi... ameacha yote na kuamua kumfuata popote atakapo enda... sasa sijui hata akiwa na mamsapu nipoze roho mamaa nimechanganyikiwa kwa penzi lako... [HASHTAG]#Kwa[/HASHTAG] sauti ya Prof j"
 
Mkuu ninadada angu anasali hilo kanisa ni shida humwambii kitu
hawa dada zetu nao ni shida hasa wa mikoani wakija mjini wana jifanya dini wana ifahamu kweli... dada yetu na sisi aliwahi kung'ang'ania kwa mchungaji japo mchungaji ana mke na watoto lakini na yeye anatafuta wokovu... tena tulimtafuta kweli kweli mpaka tukaja ambiwa yupo kanisa moja mjini...

aisee tulipiga dada etu kwakuwa hakutaka kutusikia na hakutuaga na hakutaka kuongea na sisi... hivyo tulimpandisha gari kwa nguvu arudi akapambane na wazee wake kwa kuwa hataki msaada wetu hapa mjini...
 
Hivi hizi jumuiya za Kikristo hazina wajibu kufuatilia vitu basic kama hivi? Tofauti za madhehebu zipo lakini huwezi kujiita Mkristo huku ukiamini Yesu si Mungu! Huku hujui Yesu ni Mungu kweli na mtu kweli!
Kwani wewe unaamini Yesu ni nani
 
huyo anayehubiri mwenyewe ukimwona unajua kabisa kuwa ana minyoo kwenye ubongo wake!
 
Thanks Mleta Mada ,, Mungu Atuepushe Na Kila Chachu , Bdo Wale Wala Majani ,nyoka, Sabuni Nk Alaf Ndo Wana Washirika Wengi Kupita Kiasi
 
Back
Top Bottom