Angalia Watanzania tunavyojidanganya; Mbwana Samatta hatoteuliwa kuwa mchezaji bora Nigeria

Status
Not open for further replies.

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kutokana na kwamba wengi wetu leo tunajua kuwa Mchezaji wetu anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Tout Puisant Mazembe Mbwana Samata " POPA " leo atateuliwa kuwa Mchezaji bora huko nchini Nigeria. kwa mtu anayejua mpira na uchambuzi mzuri wa mpira kwa vigezo na sifa fulani fulani Mbwana Samata leo hawezi KUTEULIWA kuwa ni MSHINDI.

Tukutane baadae na kwa wale ambao mtapenda kufuatilia hii sherehe basi hakikisheni ifikapo tu saa tatu ( 3 ) kamili muangalie super sports nine ( 9 ). na kwa taarifa yenu ni kuwa mpaka sasa naandika UZI huu tayari wachezaji 11 watakaochuana yameshatajwa na kila nikiwaangalia hao Wachezaji wenzio ambao ni MAHIRI sioni ni wapi Mbwana Samata ATASHINDA na kinachonichekesha ni kwamba Watanzania wote na hadi media zote za Tanzania bila kusahau humu mitaani watu TUNADANGANYANA kuwa Mbwana Samata atatwaa TUZO hiyo wakati mimi naona ni NDOTO YA ABUNUASI tena ni ya MCHANA kabisa.

Nawasihi tu tujifunze KUANGALIA mambo kwa KINA na kwa UPANA wake.
 
Mbona hujachambua umengangania mbwana hatatwaa hatatwaa. Njoo napoint za msingi tukuelewe lasivyo tutakuona unabif za chuki tu
 
kwa taarifa yenu ni kuwa mpaka sasa naandika UZI huu tayari wachezaji 11 watakaochuana yameshatajwa na kila nikiwaangalia hao Wachezaji wenzio ambao ni MAHIRI sioni ni wapi Mbwana Samata ATASHINDA ..

Tunaomba hiyo orodha ya wachezaji 11
 
si hatua ndogo alipofikia ........................kwa kuwa wote wameingia kwenye duru naamini yeyote anweza kutwaa tuzo
 
Samatta ana kila sifa yakuchukua tuzo

huwa nafurahi mno kujibizana na " wajinga " kama wewe na ili uone kuwa najiamini kwa uwezo wangu mkubwa wa kuona mbali nimekuwa wazi tena humu kukuambia kuwa Mbwana Samata hatoshinda na kama upo katika runinga sasa unatizama nadhani unaona nini kinaendelea. hata hivyo sikulaumu kwani siyo kosa lako.
 
Alifikaje 3 bora? Acha chuki

na ndiyo maana huwa nawadharau hivi kufika tatu bora ndiyo kushinda? hoja yangu hapa ni yeye kuwa mshindi na siyo yeye kuwemo katika tatu bora. na najua hapo ulipoandika ndiyo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia au kufikia kikomo ila shukrani kwa Serikali ya Dr. Magufuli kwa kuja na Elimu bure na lazima kuanzia mwaka huu kwani nina uhakika kuwa utaenda na wewe kusoma ili angalau uwe na uwezo wa kufikiri na kujenga hoja.
 
na ndiyo maana huwa nawadharau hivi kufika tatu bora ndiyo kushinda? hoja yangu hapa ni yeye kuwa mshindi na siyo yeye kuwemo katika tatu bora. na najua hapo ulipoandika ndiyo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia au kufikia kikomo ila shukrani kwa Serikali ya Dr. Magufuli kwa kuja na Elimu bure na lazima kuanzia mwaka huu kwani nina uhakika kuwa utaenda na wewe kusoma ili angalau uwe na uwezo wa kufikiri na kujenga hoja.
Mkuu kama umeshaona hapa watu wana uwezo mdogo wa kufikiri basi ebu tueleweshe ni kwanini Samatta hafai au hatopata, na wewe unaona ni nani anaweza kuondoka na hiyo tuzo na ni kwasababu zipi...

Nadhani ukifanya hivyo sie tusio na uwezo wa kufikiri na kuchambua tutakuelewa vyema... Ahsante !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom