Angalia vitu vya Mchina hivi

Angalia vitu vya Mchina hivi

Nyadundwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2008
Posts
234
Reaction score
290
Ahsante Mjapan kwa mitumba, lakini siku zako zinahesabika!
 
Attachments

  • baic c500.jpg
    baic c500.jpg
    175.8 KB · Views: 2,382
  • changan cs75.jpg
    changan cs75.jpg
    111.4 KB · Views: 2,112
  • changan-cs95.jpg
    changan-cs95.jpg
    85.2 KB · Views: 2,024
  • Dongfeng A60.jpg
    Dongfeng A60.jpg
    89.3 KB · Views: 1,973
  • fengshen-ax7.jpg
    fengshen-ax7.jpg
    30.7 KB · Views: 1,919
Sio utani. Magari makubwa (Howo, Faw) na mabasi Yutong yapo na yanafanya vyema tu. Sijui haya madogo tatizo ni nini?

mkuu mi nadhani hawajaamua tu kuwa na soko huku.. sijui bei zake kama sitakuwa sawa na mjapan. . . akishusha bei huku lazima ateke soko.
 
Ahsante Mjapan kwa mitumba, lakini siku zako zinahesabika!

mkuu...nimebahatika kuona na kuendesha gari ya kichina inaitwa LANDMARK ya 2014 ukiiona ni kama ya 1992,imechoka kila kitu ndani kimebanduka,yaani ni gari mbovu sijawahi kuona!! kwenye magari wachina bado sana hasa haya magari madogo.
 
Wachina ni watu wasio na akili.
Kila kitu wanachotengeneza wamekopi teknolojia yake. Hayo magari yanafanana na Range, Audi, BMW, Mercedes.
Hawana ubunifu wowote ule.
Kwa watu tunaopenda majina ya magari kamwe siwezi endesha kitu cha bei rahisi ambacho najua ipo siku kitaharibika
 
Lakn pamoja na kukopi technology lakn umeona uchumi wao? Ni sawa na Tanzania?
Maisha ni akili na ujanja ila sio ujanja wa akina change na genge lake
 
Hakuna sababu ya kuwabeza wachina kwa lolote lile, wakati mabasi ya Yutong yanaingia tuliona kama hayafai leo hii sote tukifika Ubungo tunatamani kupanda Yutong au Zengtong maana yana raha yake kuliko scania eti. Watakuja na magari hayo kwa design zote maana tangu WTO liwakubali wameteka soko la dunia eti.
 
Wachina sio wabaya kitechnologia. Wakopi wasikopi cha msingi ni kutoa product zinazoteka soko kwa ubora unaolingana na bei ya kitu. We cannot re-invent the wheel. Uvumbuzi ulishafanyika na akina Newton, Archimedes, Plato etc. Sasa hivi Waganda, Waghana na Wanigeria wameingia kutengeneza magari na ukiyaona ni mazuri tu. Ni sisi tusiokuza technologia tuliyoianza Nyumbu na kukalia kuagiza magari ya nje tu... Tubadilike, na kama kubadilika inahitaji kuiga tuige!...
 
mkuu...nimebahatika kuona na kuendesha gari ya kichina inaitwa LANDMARK ya 2014 ukiiona ni kama ya 1992,imechoka kila kitu ndani kimebanduka,yaani ni gari mbovu sijawahi kuona!! kwenye magari wachina bado sana hasa haya magari madogo.

Mkuu, usitegemee haya magari kuwa sawa na technologia ya magharibi yenye miaka zaidi ya 100. Mdogo mdogo, wanapiga hatua. Angalia haya mabasi ya Yutong, mbona yana kaa tu mpaka miaka 5? wakati trip 150 tu za moshi hela yako imerudi.
 
Wachina ni watu wasio na akili.
Kila kitu wanachotengeneza wamekopi teknolojia yake. Hayo magari yanafanana na Range, Audi, BMW, Mercedes.
Hawana ubunifu wowote ule.
Kwa watu tunaopenda majina ya magari kamwe siwezi endesha kitu cha bei rahisi ambacho najua ipo siku kitaharibika

Hapo umezidisha mkuu, hivi kama wachina hawana akili, Bongo tutakuwa kwenye kundi lipi kiakili? Na gari gani haitakuja kuharibika? Ukiangalia vizuri, magari machache sana hayafanani, hivyo kama kuiga kampuni zote zinaiga.
 
Back
Top Bottom