Angalia na Usikie MWENYEWE!

dizbap

Senior Member
Nov 25, 2009
156
86
Hebu anagalia na sikiliza Mbunge Wa Iringa Akiongelea kuhusu Bajeti Yetu;

Hii Hapa;

Iringa kwa Kweli Hamkukosea. Good, Very Good.

Wana Magamba Mpo? Presha inapanda Presha Inashuka!

Thanks.
 
Last edited by a moderator:
Dah...kwa kweli cdm ina "majembe"......CCM wanayo haki ya 'kuweweseka'!
 
Umeona eeh!! 2015 tunaongeza MAJEMBE mengine.... Wazee CCM watahama Mjengoni tu, maana patakuwa hapawafai, Presha inakuwa JUU sana mule ndani, Mtu ipo na BP, KISUKARI etc.. Hatoweza Kabisa kukaa Mule ndani. Good Work CDM!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
kazi ya mchungaji ni kulisha kondoo wa bwana.Hapa anatetea wanachi wake,Hongera wana Iringa kwa kuwa na mbunge imara
 
Machozi yamenitoka baada ya kusikiliza ukweli aliousema huyu mbungu hakika mungu atusaidie ili wabunge wa ccm wapuingue bungeni 2015!!
 
asante kwa speech ambayo hata wabunge wa chama changu cha ccm wakikaa miaka mingine 20 bungeni hawawezi kuitoa
 
asante kwa speech ambayo hata wabunge wa chama changu cha ccm wakikaa miaka mingine 20 bungeni hawawezi kuitoa

amesema kazi ya wachungaji ni kuwaombea wazinzi na wanaokamatwa ugoni na wake za watu!....................
 
AHSANTENI SAAAANA WANANYALUKOLO KWA KUTULETEA KIFAA HICHI...! poleeni saana wana mtera na tahira lenu!
 
CCM siokwamba hawaelewi nini kinachoendela bali wanajiwehua tu na kujifanya hawajui kinachoendela, wanaelea fika hii ni dhama za uwazi, mwananchi wa sasa sio yule wa 1961 kipindi cha uhuru ni kipindi cha utandawazi wanaelewa kila kitu sasa sio kipindi cha NDIYO MZEE kwa kila jambo.

Mbunge wa CCM anapiga kelele wee mwisho wa siku anaunga mkono bajeti kwa 100% na anaelewa fika kuunga mkono hoja wananchi wake ndio wanaotaabika asilimia kubwa wananchi yeye anaendelea kutesa mjini. Huu ni upuuzi!!!
 
Jembe jana limewaka magamba wote walikaa kimyaa wakafyata!hongereni iringa maana huyo ndie mbunge wa iringa nzima
 
halafu kumbe "ukitukana" kwa kiingereza hufukuzwi eh? Maana baadhi ya nahau zake za kiingereza zinetafsiriwa kwa kiswahili wangemu-mnyika sasa hivi.
 
Ndugu zangu huyu Mch, Msigwa ni jembe haswa na alichosema chote ni kweli tupu!. Amesema ukweli halisi ambao kwa hakika Nyi Nyi Emu (CCM) wanatakiwa wafike mahali wajitambue! Hivi nini kigumu kinachowafanya hawa jamaa washindwe kuvunja ukimya? Yaani wanahitaji na kusubiri mpaka hisani ya wamarekani ili kuweza kutambua huu upuuzi unaoendeshwa na serikali dhaifu, kweli magamba! Kweli magamba hamuelewi haya mambo rahisi??? Mmelishwa nini hivi hata mnashindwa kuwatetea wananchi wenu? Kama alivyosema mchungaji Msigwa, ambacho pia ni kijembe cha uhakika kama sio ngumi ya uso kwamba wengi hamjachagulia au kupita kiuhalali ndo maana mnaionea aibu serikali dhaifu! Nawasikitikia maana wengi wenu 2015 hamtarudi kama hamtaamua kuvunja ukimya!
 
kwa kweli REV Msigwa ametoa hotuba ya miaka 5. Iringa mnajua kuchagua watu. Kidogo machozi yanitoke baada ya kumsikiliza huyu jamaa siyo hawa vilaza wakina Lukuvi
 
Machozi yamenitoka baada ya kusikiliza ukweli aliousema huyu mbungu hakika mungu atusaidie ili wabunge wa ccm wapuingue bungeni 2015!!
Pole Sana....But hivyo ndo MAGAMBA wanavyotulostisha sisi WATANANZANIA, Can you Imagine eti Nape Alimfananisha Mch. Peter Msigwa Huyo alieongea Points zilizokutoa machozi eti ni kama PUNDA. Hapo ndo utaona wanamagamba ni BURE. Mungu atatusaidia tupate Majembe kama haya tu 2015! Chadema Oyeee!
 
Mheshimiwa Msigwa hasemi huo uzalishaji uongezwe vipi. Kasema yeye mwenyewe kwamba CCM hawawezi kutatua matatizo maana wao ndio "wametuweka kwenye mess hii, you guys are tired." Sasa suluhisho lake yeye ni nini?

Ameshambulia wazinzi na wanaotembea na wake za watu (shambulizi kwa Mwigulu mwenye sifa hiyo, ambae ndie alisema CHADEMA waombewe) lakini hapo hapo amekosoa majadaliano ya "khanga na ngonjera." Yale yale ya vijembe!

Kwenye theology kuna matundu kwenye hoja zake. Amesema hakuna nadharia ya maombi katika uchumi wala theology na kwamba Mtume Paulo alisema "asiyefanya kazi na asile," sio aombewe. Ni kweli, lakini Kristo Yesu alisema tuige mfano wa ndege wa angani, "ndege wao hawapandi wala hawavuni wala hawahifadhi chochote kwenye ghala lakini Baba wa Mbinguni anawalisha." Kesheni Mkiomba. Kwa hiyo hata Biblia hapa haina majibu.

Amesema serikali haisikilizi ushauri wa ma professa. Ushauri gani? Toa mfano!

Yeye ni mpinzani, hajaja hapa kuisifia serikali, ana wajibu wa kuipinga. Ok. Na CCM wana kosa gani kutokukusifia wewe, kwani CCM ni upinzani wenzako?

Asilimia 42% ya watoto wamedumaa ubongo, unadai. Sawa. Sasa hapa Waziri wa Fedha iandike vipi bajeti ili watoto wasidumae akili, atenge fungu la kulisha watoto samaki mashuleni kuwapanua akili?

Na mwisho, kama unadai CCM hawawezi kuwa solution kwa sababu ndio chanzo cha tatizo kwa nini unawasihi CCM hao hao walete suluhisho? Amedai watu wa "stretch their brains," lakini yeye hajatupanulia mjadala.
 
Jana nilikuwa nimechoka sana, but mchungaji you made my day brighter; Hongera sana, CDM haibahatishi, jembe moja juu ya jembe lingine A to Z.
 
he is not insane as y........ ila huo muda wa dakika 15 au less angewezaje kujibu haya unayosema kwani hapa tena yako obvious kwa mtu ambaye hana uhsuiano na ufisadi. Majibu mengi yapo hata ukimuona atakupatia kama ni lazima yatoke kwake! alichokuwa anasema ni kuwa watu waache kuzomea wenzao counseling*ushauri zaidi! sasa kuna ubaya gani hapo unaoona kakosea!!! Mara nyingi wabunge wa CCM hata hawasilikizi hoja za wapinzani wao ni kuzomea tu kama ulivyozomea hapo juu lakini wakitoa hoja hata kama si nzuri wa au si masilahi ya taifa watampigia makofi simply tu kwa kuwa ni CCM, elewa hata sisi wengine si kuwa tunaichukia CCM bali matendo yao na wengi wao ni wana CCM halisi humu humu na kadi hai ila wasipoangalia kwa mwendo huu kadi nyingi zitatupiliwa mbali!
 
Back
Top Bottom