Angalia Muundo wa ACT, Huu sio Udikteta Huu?

Angalia Muundo wa ACT, Huu sio Udikteta Huu?

Jibu swali wewe! Ina maana mkubwa wa chama sharti aitwe Mwenyekiti?

Nitajie cheo kimoja CCM mwenye nguvu kuliko Mwenyekiti wa Chama?! Kwani walishindwa madaraka yote ya Kiongozi Mkuu wa Chama akapewa mwenyekiti na kisha huyo kiongozi wa chama akawa ndie mwenyekiti?!

Hoja yako ingeonekana ni ya msingi endapo hiyo nafasi ya Kiongozi wa Chama ingekuwa ni ya kudumu na exclusively kwa watu au mtu fulani lakini katiba yao inasema wazi kwamba hiyo ni nafasi ya kuchaguliwa na vile vile kiongozi wa chama anaweza kuondolewa!
Kuna haja ipi ya kuwa na mwenyekiti na katibu halafu uwe na kiongozi mkuu wa chama kama sio kujitengenezea vyeo vyenye mamlaka zaidi ni nini? huo ni ulafi tu wa madaraka.
 
Nadhani ni majina ya cheo tu, labda huyo Kiongozi Mkuu wa Chama, kwenye Chama chako anaitwa Mwenyekiti.
 
Nadhani ni majina ya cheo tu, labda huyo Kiongozi Mkuu wa Chama, kwenye Chama chako anaitwa Mwenyekiti.
Kwa maana hiyo jina jingine kwa mwenyekiti na katibu wake ni lipi? Kama Kiongozi mkuu ndiye mwenyekiti kwa mantiki hiyo?

Vyeo vya kujitengenezea havijawahi kumuacha mtu salama. lazima tu mwisho wa siku uumbuke kama hivi.
 
Kwa upeo wako mdogo unautafsiri udiktetakutokana na ukubwa wa maamuzi!

You are solely nothing.

Dictatorship is not having absolute power but utilizes it in an oppressive or abusive manner.

Jamii inayofaham inakushangaa kwa upeo wako mdogo wa uelewa.
Anyway, keep on utafika kiwango cha kutambua mambo.

KAMA KUWA NA MAMLAKA MENGI NI UDIKTETA, RAIS WA TZ ANAVYOTEULIWA TU ANAPASWA KUITWA DIKTETA KWA KUWA NA MAMLAKA MENGI.
nilitegemea hoja yako ingejikita katika mambo haya;

1. katiba iliyowekwa hapa si halisi.

2. content za ibara zilizokuwa qouted sio sahihi.

ungezitia nyama hoja hizo mbili kwa kuweka katiba sahihi yenye ibara sahihi ili nionekane kuwa ninapotosha.

Hujafanya hivyo.

Na kuchallenge kuweka hapa katiba yenu ya chama, otherwise unapiga porojo tu.
 
Kwa upeo wako mdogo unautafsiri udiktetakutokana na ukubwa wa maamuzi!

You are solely nothing.

Dictatorship is not having absolute power but utilizes it in an oppressive or abusive manner.

Jamii inayofaham inakushangaa kwa upeo wako mdogo wa uelewa.
Anyway, keep on utafika kiwango cha kutambua mambo.

IKAMA KUWA NA MAMLAKA MENGI NI UDIKTETA, RAIS WA TZ ANAVYOTEULIWA TU ANAPASWA KUITWA DIKTETA KWA KUWA NA MAMLAKA MENGI.
Kutengeneza mazingira ya kuwa na absolute power ni chembe chembe za udikteta.
 
Kwa pamoja tuangalie muundo wa chama cha ACT-wazalendo kwa kutegemea katiba ya Chama;

Tuanze na Ibara ya 29 ya Katiba, Ibara ndogo ya 1 na 2, hizi ndizo Ibara zilizotoa mchanganuo wa uongozi wa Chama Cha ACT - Wazalendo kitaifa , Nanukuu;

29. ACT-Taifa

(1) ACT-Taifa ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na Halmashauri Kuu yaTaifa.

(2) Viongozi Wakuu wa Chama Taifa watakuwa ni:

i) Kiongozi wa Chama;

ii) Mwenyekiti wa ACT-Taifa;

iii) Makamu Mwenyekiti wa ACT-Taifa upande wa Zanzibar;

iv) Makamu mwenyekiti ACT-Taifa upande wa Bara;

v) Katibu Mkuu wa ACT-Taifa;

Kwa shida ni nini-huo ndio mfumo wa uongozi walioona unawafaa. In practise, hata CCM mwenyekiti hana shughuli nyeti kama Katibu mkuu. Usilamimishe Vyama vyote viwe na mfumo unaofanana wa uongozi
vi) Naibu Katibu Mkuu ACT-Taifa upande wa Zanzibar;

na vii) Naibu Katibu Mkuu ACT-Taifa upande wa Bara.

Kwa mchanganuo huo hapo juu, utaona kuwa kiongozi wa Chama ndiye kiongozi Mkuu wa Chama, nikiwa na maana kwamba Mwenyekiti wa Chama kama wengi tunavyofahamu hana mamlaka yoyote juu ya kiongozi wa Chama.

Sasa tuyaangalie majukumu ya kiongozi wa chama; Ibara ya 29 Ibara ndogo ya (25)

(25) Kazi na sifa za Kiongozi wa Chama

i) Atakuwa kiongozi wa Chama na Mwenyekiti wa kikao cha Mkutano Mkuu wa kidemokrasia

ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafi sa wa chama; ACT Wazalendo Katiba.

iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Chama Taifa na uteuzi kuthibitishwa na Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii;
iv) Kuteua wasemaji wa kisekta ambao pia watakuwa ni wenyeviti wa Kamati za Makao Makuu;

v) Kuteua Naibu Kiongozi wa Chama kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi atakapoona haja hiyo;

vi) Kiongozi wa Chama anaweza kuteua mwanachama mwingine mwenye mchango maalumu kuingia katika vikao vya chama kwa kushauriana na Mwenyekiti na Katibu Mkuu kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo kwa maslahi ya chama;

vii) Kupendekeza majina ya washauri wa chama baada ya kushauriana na Mwenyikiti;

viii) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa;

ix) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa;


x) Ataendesha vikao vya Kamati za Kisekta ili kutengeneza misimamo ya kisera ya chama na kuwasilisha mapendekezo ya kisera katika vikao vya chama kwa maamuzi Nakadhalika.


kwa afya ya mjadala ni vyema tukaangalia sasa majukumu ya Mwenyekiti wa Chama

Ibara ya 29 ibara ndogo ya 28 ya Katiba ya ACT, 2015;

(28) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa:

i) Atakuwa mlinzi mkuu wa sera zilizopendekezwa na kupitishwa au jambo lolote litakaloamuliwa na kupitishwa na vikao vya chama;

ii) Atahakikisha kuwa ngazi zote za chama zinatekeleza maamuzi yaliyotolewa navikao;

iii) Atahakikisha kuwa ngazi zote zinafanya kazi ndani ya mipaka ya katiba, kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na vikao vikuu vya chama;

iv) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama katika Chama Taifa;

v) Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama ya kitaifa isipokuwa vikao vya utendaji na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa Wanachama;

vi) Atafanya shughuli nyingine za Chama kama atakavyoelekezwa na vikao vya Chama

vii) Atapendekeza kwa Kamati Kuu majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa Manaibu Katibu wakuu kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi ya Kitaifa Nakadhalika


Ukisoma katiba hii ya ACT, Utagundua yafuatayo;

1. Mwenyekiti wa chama hana mamlaka kumzidi kiongozi wa chama.

2. Mwenyekiti wa chama anafanyakazi kwa kufuata maelekezo ya vikao vya chama, hivyo hana maamuzi.

3. Mwenye mamlaka yote ya Chama ni kiongozi wa chama.

Kitendo cha Kiongozi wa chama kujilimbikizia mamlaka yote hayo ni cha kibinafsi na kinatakiwa kuogopwa na wapenda demokrasia wote hapa nchini,

Kwa muktada huo, kuna kila dalili za udikteta kwenye chama cha ACT wazalendo na umehalalishwa kabisa kisheria.
 
The problem is not having absolute(total) power, but how can you use that unqualified power!.

TARATIBU UTAELEWA TU.

DONT DESPAIR.
Kutengeneza mazingira ya kuwa na absolute power ni chembe chembe za udikteta.
 
The problem is not having absolute(total) power, but how can you use that unqualified power!.

TARATIBU UTAELEWA TU.

DONT DESPAIR.
Hili ndilo tatizo lakujibizana kwa hoja na mtu asijeelewa kuwa haelewi. Wala asiyejua kuwa hajui. Siku njema mkuu.
 
Hongera mwl wa kiswahili, mnahitajika sana Somalia mkafundishe lugha hiyo.

ACT wazalendo ni taasisi makini. Ni chama chenye misingi imara na kinajitambua.

Chama makini akiwezi "jishaua" (lugha za mipasho), chama kinatoa "MAAMUZI".

Anna tumeamua apumzike uenyekiti wa chama.
Wewe ulitakaje?...tumzuie kwenye nafasi aliyoteuliwa? (that is a person interest!)

Kama chama tumekuja na maamuzi makini ya kumsimamisha uenyekiti.

Dr Kitila aliandika barua kuachia nafasi ya ushauri wa chama.

Ulitakaje tuikatae barua!?
Kwa hiyo akili yako inakuambia kuwa mtu akiamua kuacha kazi ya chama hicho chama siyo cha maana!?

Wale madiwani wa CDM pale Arusha wanahamia ccm.(whether they have been corrupted or not), kwa hiyo chadema hakina future!?

THINK BIG WEWE!
Acha fikra mgando.

Ukitaka kuongelea habari ya upeo wewe mtu ambaye hata Kiswahili hujui, hujui kwamba hakuna neno "kubadirishwa" na neno sahihi ni "kubadilishwa" katika Kiswahili, kwa ushamba wako huo, huna cha kuniambia kuhusu upeo.

Mwalimu Nyerere alikuwa muajiriwa wa serikali ya mkoloni, akaona harakati za chama cha TANU ni muhimu kuliko kufanya kazi ya serikali ya mkoloni. Akachagua kufanya kazi ya chama. Akaacha kufanya kazi serikali ya mkoloni.

Uamuzi wake huo unatuambia wasomi wa historia mpaka leo kwamba kati ya kazi ya ualimu serikali ya mkoloni na kazi ya chama, kipi aliona muhimu.

Viongozi wenu wamepewa nafasi ya kufanya kazi ya chama au serikali hii, wamechagua serikali kwa sababu chama chenu hakina future.

ACT imejishaua kumuondoa Anna Mghwira uenyekiti baada ya Anna Mghwira kukitosa chama na kuamua kukubali ukuu wa mkoa aliopewa na Magufuli.

Mchumba kakwambia kapata mchumba mwingine, unawahi kusema eti umemuacha wakati yeye kwa kukuambia tu kapata mchumba mwingine maana yake yeye ndiye kakuacha wewe.

Kama Kitila Mkumbo alibadili kazi moja na nyingine tu katika serikali, kwa nini alijiuzulu kuwa senior consultant wa ACT Wazalendo? Kwa nini Zitto alisema Kitila mkumbo hawezi kuendelea kuwa mshauri wa chama?

Kama ACT ni chama cha maana sana, kwa nini Anna Mghwira aliamua kukubali ukuu wa mkoa aliopewa na Magufuli?

Kili RC Anna Mghwira stripped off ACT chairmanship

Tanzania: Prof. Kitila Mkumbo Named Permanent Secretary in Water, Irrigation Portfolios
 
Ni maamuzi mazuri, maana namuelimisha mtu aliyekunjwa maji ya chama na mwanga wa mwenge.

Shida sana.

TWAWEZA hawakukosea kwenye tafiti yao.
Hili ndilo tatizo lakujibizana kwa hoja na mtu asijeelewa kuwa haelewi. Wala asiyejua kuwa hajui. Siku njema mkuu.
 
Hivi mwigamba bado ni katibu mkuu?
Mimi hata muda mchafu wa kufuatilia nani katibu mkuu wa ACT sina.
Hongera mwl wa kiswahili, mnahitajika sana Somalia mkafundishe lugha hiyo.

ACT wazalendo ni taasisi makini. Ni chama chenye misingi imara na kinajitambua.

Chama makini akiwezi "jishaua" (lugha za mipasho), chama kinatoa "MAAMUZI".

Anna tumeamua apumzike uenyekiti wa chama.
Wewe ulitakaje?...tumzuie kwenye nafasi aliyoteuliwa? (that is a person interest!)

Kama chama tumekuja na maamuzi makini ya kumsimamisha uenyekiti.

Dr Kitila aliandika barua kuachia nafasi ya ushauri wa chama.

Ulitakaje tuikatae barua!?
Kwa hiyo akili yako inakuambia kuwa mtu akiamua kuacha kazi ya chama hicho chama siyo cha maana!?

Wale madiwani wa CDM pale Arusha wanahamia ccm.(whether they have been corrupted or not), kwa hiyo chadema hakina future!?

THINK BIG WEWE!
Acha fikra mgando.
Wewe hujajua kwamba "akiwezi" si neno la Kiswahili, neno sahihi ni "hakiwezi".

Kajifunze Kiswahili kwanza kabla ya kuja kurukia mijadala ya siasa kwa lugha usiyoijua.
 
Kuna haja ipi ya kuwa na mwenyekiti na katibu halafu uwe na kiongozi mkuu wa chama kama sio kujitengenezea vyeo vyenye mamlaka zaidi ni nini? huo ni ulafi tu wa madaraka.
Kujiongezea mamlaka zaidi kivipi? Nimekuuliza kwani hayo mamlaka ambayo yapo kwa Kiongozi Mkuu yasingeweza kuwekwa kwa Mwenyekiti na muhusika aka-exercise hayo mamlaka huko huko kwenye nafasi ya Mwenyekiti?! Kama ni ulafi, angerundika mamlaka yote kwa mwenyekiti kisha yeye ndo akawa Mwenyekiti; which means, hiyo hoja haina msingi!

Sana sana mfumo wao nauona mzuri kwa chama kichanga kama ACT kwa sababu, wakati Zitto ambae ni very experienced politically, anakuwa juu kuwasaidia mwenyekiti na katibu ambao possibly wanaweza wasiwe experienced kama yeye.

Kwa mfano, ingawaje Anna Mghwira amefanya siasa kwa muda mrefu lakini sikumbuki kama ameshawahi kuwa active kwenye siasa za majukwaani kabla hajawa mwenyekiti wa ACT. So, kama kusingekuwa na nafasi ya kiongozi mkuu, sioni namna gani Mama Anna angeweza kuwa Mwenyekiti wa ACT wakati mwanzilishi wa chama yupo!

Lakini kuwapo kwa nafasi ya kiongozi mkuu, yeye kukampa nafasi ya uenyekiti na hatimae kuanza kuchukua uzoefu wa siasa za majukwaani; uzoefu ambao huenda asingeupata!
 
Back
Top Bottom