Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,017
- 51,144
Kwa pamoja tuangalie muundo wa chama cha ACT-wazalendo kwa kutegemea katiba ya Chama;
Tuanze na Ibara ya 29 ya Katiba, Ibara ndogo ya 1 na 2, hizi ndizo Ibara zilizotoa mchanganuo wa uongozi wa Chama Cha ACT - Wazalendo kitaifa , Nanukuu;
29. ACT-Taifa
(1) ACT-Taifa ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litaundwa kwa kuzingatia masharti ya Kanuni za Chama zilizotungwa na Halmashauri Kuu yaTaifa.
(2) Viongozi Wakuu wa Chama Taifa watakuwa ni:
i) Kiongozi wa Chama;
ii) Mwenyekiti wa ACT-Taifa;
iii) Makamu Mwenyekiti wa ACT-Taifa upande wa Zanzibar;
iv) Makamu mwenyekiti ACT-Taifa upande wa Bara;
v) Katibu Mkuu wa ACT-Taifa;
vi) Naibu Katibu Mkuu ACT-Taifa upande wa Zanzibar;
na vii) Naibu Katibu Mkuu ACT-Taifa upande wa Bara.
Kwa mchanganuo huo hapo juu, utaona kuwa kiongozi wa Chama ndiye kiongozi Mkuu wa Chama, nikiwa na maana kwamba Mwenyekiti wa Chama kama wengi tunavyofahamu hana mamlaka yoyote juu ya kiongozi wa Chama.
Sasa tuyaangalie majukumu ya kiongozi wa chama; Ibara ya 29 Ibara ndogo ya (25)
(25) Kazi na sifa za Kiongozi wa Chama
i) Atakuwa kiongozi wa Chama na Mwenyekiti wa kikao cha Mkutano Mkuu wa kidemokrasia
ii) Atakuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafi sa wa chama; ACT Wazalendo Katiba.
iii) Kuteua wajumbe watano wa Kamati Kuu baada ya kushauriana na Mwenyekiti wa Chama Taifa na uteuzi kuthibitishwa na Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba hii;
iv) Kuteua wasemaji wa kisekta ambao pia watakuwa ni wenyeviti wa Kamati za Makao Makuu;
v) Kuteua Naibu Kiongozi wa Chama kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi atakapoona haja hiyo;
vi) Kiongozi wa Chama anaweza kuteua mwanachama mwingine mwenye mchango maalumu kuingia katika vikao vya chama kwa kushauriana na Mwenyekiti na Katibu Mkuu kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo kwa maslahi ya chama;
vii) Kupendekeza majina ya washauri wa chama baada ya kushauriana na Mwenyikiti;
viii) Atakuwa ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa Chama katika mambo ya kitaifa na kimataifa;
ix) Atakuwa mtoa habari mahususi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa;
x) Ataendesha vikao vya Kamati za Kisekta ili kutengeneza misimamo ya kisera ya chama na kuwasilisha mapendekezo ya kisera katika vikao vya chama kwa maamuzi Nakadhalika.
kwa afya ya mjadala ni vyema tukaangalia sasa majukumu ya Mwenyekiti wa Chama
Ibara ya 29 ibara ndogo ya 28 ya Katiba ya ACT, 2015;
(28) Kazi za Mwenyekiti wa Chama Taifa:
i) Atakuwa mlinzi mkuu wa sera zilizopendekezwa na kupitishwa au jambo lolote litakaloamuliwa na kupitishwa na vikao vya chama;
ii) Atahakikisha kuwa ngazi zote za chama zinatekeleza maamuzi yaliyotolewa navikao;
iii) Atahakikisha kuwa ngazi zote zinafanya kazi ndani ya mipaka ya katiba, kanuni, sera na maamuzi yoyote yaliyoagizwa na vikao vikuu vya chama;
iv) Atafuatilia na kuratibu masuala ya ulinzi na usalama katika Chama Taifa;
v) Atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya chama ya kitaifa isipokuwa vikao vya utendaji na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa Wanachama;
vi) Atafanya shughuli nyingine za Chama kama atakavyoelekezwa na vikao vya Chama
vii) Atapendekeza kwa Kamati Kuu majina ya watu wanaofaa kuteuliwa kuwa Manaibu Katibu wakuu kwa kushauriana na Kamati ya Uongozi ya Kitaifa Nakadhalika
Ukisoma katiba hii ya ACT, Utagundua yafuatayo;
1. Mwenyekiti wa chama hana mamlaka kumzidi kiongozi wa chama.
2. Mwenyekiti wa chama anafanyakazi kwa kufuata maelekezo ya vikao vya chama, hivyo hana maamuzi.
3. Mwenye mamlaka yote ya Chama ni kiongozi wa chama.
Kitendo cha Kiongozi wa chama kujilimbikizia mamlaka yote hayo ni cha kibinafsi na kinatakiwa kuogopwa na wapenda demokrasia wote hapa nchini,
Kwa muktada huo, kuna kila dalili za udikteta kwenye chama cha ACT wazalendo na umehalalishwa kabisa kisheria.