Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
mama kuanzia leo nakuheshimu na kweli unastahili kuwa first lady kwa hekima hiziEEEeeeeeeiiiiii Jamani .. Polepole..ehe!! sasa matusi ya nini..!!
Mimi nadhani kuna TATIZO KUBWA SANA SEHEMU FLAN, Kuna mapandikizi ya watu wanaojiita waislam au hata wakristu lakini si kweli kwamba ni wapenzi wa dini husika, kazi yao ni kudhalilisha dini za Mwenyezi Mungu kwa kuandika taarifa ambazo zitaidhalilisha dini flani mbele ya jamii
.. Toka lini Masuala ya elimu yakamegeana na dini? ni kama mtu asemaye mapenzi yana dawa ni kudhalilishana tu. kwanza unaposema watu wanafelishwa ni kitu cha ajabu sana, watahiniwa hawaambatanishi majina yao na namba za mitihani yao sambamba, vitu hivi hutengwa, na msahihishaji asahishapo hajui kama huyu ni hamisi, ramadhani, neema, au Joni.. anapambana na namba ya mtahiniwa tena bila kujua ni wa jinsia gani na akimaliza kibarua chake humpatia karatasi mwenzie ambaye huhakikisha je ni kweli alivyosahihisha? na mwisho kiongozi wa stesheni huhakikisha, sasa wote hao watatu wanaweza kumchakachua mtu wasiyemjua?, wakimaliza huorodhesha matokeo na baadae kazi yote hupelekwa kwenye database yenye kumbukumbu ya majina na kuoanisha kabla ya kuyatangaza. na "Database" husika inabema maelfu ya majina na ukiikoroga tu kidogo umeharibu kila kitu. sasa nani huyo atokee ati achezeshe huyu afeli huyu asifeli, jamani mbona mambo ya aibu haya. vilevile maelfu ya wakristu wana majina ya kiislam, kusikia padri au mchungaji Ramadhani, Husein, Juma ni kitu cha kawaida kwenye jamii yetu, sasa nani huyo ati aangalie huyu ingawa ana jina la kikristu lakini inawezekana ni mwislam huyu wacha nimfelishe!!!! shit!! ni upuuzi na utani wa kudhalilisha Dini huu..Dini hizi zimekuja juzi tu hapa TZ, tulikuwa na majina yetu wajanja hawa wakatupachikia imani na dini zao plus majina yao kwamba tunakuwa hata wendawazimu wa kuandika wazimu gazetini.Dini ziliikuta jamii ya Kitanzania isitoshe zaweza ondoka Tanzania ikabaki pale pale.
.. Inakuwaje Mwandishi anapata nafasi ya kutumia kalamu yake kuandika kitu kama hii, kisha mhariri mkuu anasema Inshallah iandikwe, kisha Jopo la pasmota ya gazeti wanaridhia Habari kama hii itolewe, yenye kuleta aibu na kudhalilisha heshima na utu wa ustaarabu wa Dini na kisiwa chetu hifadhi ya neema ya marashi ya Karafuu na Utalii?
Kama Mchangiaji alivyosema, elimu ni mapambano, nadhani tupambane, lakini pia si hekima wachangiaji wakatumia mwanya huu kudhalilisha utu na Heshima za dini zetu za Ubudha, Uyoga, Ukristu au uislam.. Tuheshimiane kama jamii.. akiropoka mlemavu wa kimawazo na mtazamo mmoja basi tusionekane wote kuku na kuporomoshewa mimatusi..
ALAMSIK..