Angalia kwa makini vijana hawa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia kwa makini vijana hawa.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mdau, Jul 25, 2010.

 1. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Ati,hivi hawa vijana walikua wanamaanisha nini???

  [​IMG]


  12121.jpg
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nadhani umefika wakati sasa mtu anapotoa malalamiko yake akatumia lugha fasaha na inayoeleweka kwa watu wote, Kutumia maneno kama "tatizo ni Serikali ya Kishkaji ya Kikwete inaweza kutafsirika tofauti na ulivyokusudia na matokeo yake hata uliotegemea wakuunge mkono wakakutupa kwa sababu tu hawajakuelewa.

  Nawasilisha.
   
 3. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Walikuwa wanamaanisha kuwa wasomi wengi ni wanafiki. Juzi juzi ndio wao pamoja na kukosa pesa walijitolea kumchangia na kumdhamini huyo wanayesema ana serikali ya kishkaji.
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nakereka nikiona maandamano ya vyuo vikuu. Mara wawalalamikie, mara wawasifie viongozi, unafiki mtupu
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  tatizo wengi wa wasomi wa vyuo wameingia vyuoni kwa uwezo mkubwa wa kukariri
  na uwezo wa kuwa wadadisi na wafikilivu, waelewa wenye akili ya kujitegemea kuwaza
  saa ingine hapo walikaririshwa tu wafanye hivyo
  hiyo imepelekea hata wawapo kwenye mambo nyeti kama hayo hujikuta kuwa
  wanalalamikia wasichokijua, na wanakijua wasichokilalamikia
  wanavaa wakati wa kuvua, na wanavua wakati wa kuvaa
   
 6. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wametumwa na 'Panga" hao
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Jul 25, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Lakini tatizo hapo ni nini wakuu, unajua hawa tunao waita wasomi na tuna wakosoa sana utadhani wengi wetu hatujapitia huko. nina hakika asilimia kubwa hu jf tumepitia huko huko, hivyo wapo wanaofuata mkondo kumuunga jk na wapo wanao jua kusimamia na kudai haki zao
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  "Panga" ndio nini mkuu?
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  mimi nadhani msomi ndiye mtu wa kwanzza anayepaswa kujitambua....tatizo hapa nchini kwetu,wasomi wengi wanajitambua "negatively",badala ya kufanya mema na kusaidia wananchi,waningia kwenye mkumbo wa maisha ya kujilimbikizia mali, whether kwenye siasa au mambo mengine..
   
 10. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  vijana hawa walikua Diamond Jubilee tena...
   
 11. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  wasomi wetu waoga wa kusema ukweli,na hii imetokana na elimu yetu ya kusomea vyeti tu na si elimu ya kujiwezesha kuwa mwenyewe katika maisha.
   
 12. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu sio wote wanaisapoti serikali. Kama ilivyo kwa jamii yeyote, wanafiki hawakosekani. CCM inawatumia wanafunzi wanafiki wenye njaa ya mkate au sifa kuwasaliti wenzao. Hawa ndo wanaojikomba kwa viongozi na kubinafsisha elimu yao. Haihitaji hata certificate ya VETA kugundua kuwa CCM hakuna cha maana wanachokifanya nchi hii hivyo ukiona mwenye degree/msomi anaisifia na hata kumchangia mgombea wake ujue kuna ..........
   
 13. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wasomi wetu hawajitambui kama ulivyosema thats why hata wahadhiri badala ya kukata nyanga wanakimbilia siasa. Jamaa wameonyesha kero zao lakini bado hawajatoa demo ya kutosha ili kufikisha ujumbe wao. Maana kubeba bango hakutoshi na matendo yanatakiwa. Shida za watz ndizo zinaleta undumilakuwili wa watu. Huku wanataka na huku wanataka. Chagua chema kwa tz bora.
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mtatiro atawamiss sana jimbo la UBUNGO....
   
 15. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Anyisile hauko sahihi sana kwa ulichoandika. baada ya kuangalia hiyo picha ilikupasa urudishe kumbukumbu zako nyuma na kujiuliza; Picha hiyo ilipigwa lini? Ilipigwa chuo gani? Nini lilikuwa suala la msingi mpaka hao wakaandamana? Maana ya ujumbe uliopo hapo ndani ya mabango? Nini yalikuwa matokeo ya ujumbe wa bango hilo na maandamano/mgomo wao?

  Usikurupuke tu kudharau wakati unaonyesha ni bingwa wa kusahau( unamatatizo makubwa). Nani kakwambia kuwa walikaririshwa wafanye hivyo? Rudia kuyasoma mabango yote mawili, halafu tumia akili yako kuyatafsiri maudhui yake

  Labda kukukumbusha wewe nawale wengine wanaotafsiri vibaya ni kuwa picha hiyo ilipigwa pale UDSM-Main campus wanachuo walikuwa wakilalamikia kutopewa pesa zao toka Bodi ya Mikopo.

  Hawa wasomi walitumia fikra zao kiusahihi katika kutafuta chanzo cha matatizo waliyonayo. Japo kwa nje tatizo laonekana ni Bodi ya Mikopo, lakini kiuhalisia tatizo la msingi lilikuwa serikali ambayo watendaji wake walichaguliwa ama kupewa vyeo kwakuwa ni marafiki wa Jakaya Kikwete au walimsaidia kuingia madarakani (connect na yule mama aliyekuwa anahusika na kashfa za EPA akapelekwa kwenye Bodi hiyo).

  Japo walisalitiwa na yule Raisi wa TAHLISO (ambaye ni kada CCM) na kisha kufukuzwa, ukweli umebaki vilevile hadi leo ya kwamba "TANZANIA TUMEPATA MATATIZO MAKUBWA SANA KATIKA AWAMU HII YA NNE HATA WENGINE KUSHINDWA KUWAJIBISHWA JAPO NI WEZI, KWASABABU TU NI WASHIKAJI (MARAFIKI,VIBARAKA,etc) wa KIKWETE".

  Need I say more?

  Naomba tujiulize wanafunzi hao walikuwa waongo?
   
 16. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Pengine huelewi changamoto zinawapata wanafunzi wa vyuo vikuu! Wakati fulani mwaka jana, nilianza kuona idadi ya wanafunzi wanakuja kuniomba msaada wa fedha ya chakula inaongezeka, nikawa nimewauliza kulikoni, ndio nikagundua hawakuwa wamewekewa pesa yao ya mkopo kwa muda mrefu. Baada ya wiki tatu, wanafunzi waliandamana na wiki moja baadae waliwekewa hela na kulaumiwa mno.

  Wanafunzi wanaotaka mikoani wasio na ndugu Dar wanateseka sana mikopo inapocheleweshwa, na hata wangekuwa 'watakatifu' kiasi gani, inawabidi wajiunge na mgomo kama upo.

  Uongozi wa vyuo nao unawatesa na kuwanyanyasa wanafunzi kwa namna ambayo wale walioko nje ya hivi vyuo ni vigumu kuelewa. Nafahamu nyakati wanafunzi wamevurujiwa usajili wao kutokana na kumbu kumbu hovyo za utawala. Siku chache kabla ya mitihani wanaambiwa hawawezi kufanya mitihani kwani hawajalipa. Kupata ufafanuzi ulichukuwa muda na alnusura ilete kutokuelewana.

  Lakini yote tisa, jamani hawa ni wanafunzi wa vyuo vikuu, they are supposed to be mature enough and thinkers at that to the extent they have an opinion about what is happening in their own environment, if this opinion is not respected, they may take to voting, going for a strike. Hivi vimoto moto vya matatizo ya vyuo vikuu ndio yamezalisha midahalo ambayo iliwajenga baadhi ya wanafunzi hao na kuonyesha vipaji ambavyo leo hii ndio viongozi wa taifa, (ingawaje wengine wanakuja kukumbatia ufisadi)
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180


  ilikua ni 2007...
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  nashukuru san amkuu lakini nadhani huo ni ukweli japo wewe umeona kuwa nimeangalia sana upande mmoja na kukurupuka kutoa mawazo yangu, pengine siwezijua wewe uko upande gani katika hilo uwazi uko pale pale kuwa wasomi wa tanzania ni wababaishaji tu, hilo hatuwezi kulivika nguo lionekane kama unavyotaka, unafiki wetu wa kutaka kuvuna wakati hatujapanda, na kutaka kupanda ambacho hatutavuna ndiyo ulikutawala wewe katika mawazo yako na kuona wakati wasomi walizalisha lililo jema katika nchi hii,
  ni miongoni mwa wasomi wanaotete ughafidhuna, ufirauni na umafia wa serikali ya kinduli ya ccm pamoja na uozo wake ambao hata mtoto wa darasa la saba hataki kuuona vipi kwako wewe na mimi?
  tafakali!!! wasomi wetu ni mamluki na wanafiki sana
   
 19. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Serikali ya kishkaji....
   
 20. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Jamani vijana hawa walikua sahihi, JK hawezi kulivua wa kujivua GAMBA!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...