Katika sehemu ambazo zimepangika musoma ni moja wapo,nadhani hata majiji ya hapa nchini yakasome….Tazama mpangilio wa huu mji unavyopendeza
Laiti kama Nyerere angekuwa mbinafsi huu mji ungekuwa jiji linalopendeza sana
Nadhani kuna kitu hukijui.
Ukweli ni kwamba miji yote tanzania, makazi yaliyoanzishwa miaka hiyo yalikuwa yamepangika vizuri.
sasa sijui shida ilitoka wapi, wakati tunaamini kwa sasa ndiyo tuna wataalamu na vifaa zaidi lakini ukitazama makazi ndiyo tumevuruga zaidi.
miji inayokua kwa kasi imekuwa na kasi ya ukuaji wa makazi holela.
In short mawaziri wa ardhi nyumba na makzi wote wa hivi karibuni ni ovyo kabisa, sijui kina Lukuvi, tibaijuka.
Yaani waziri anakaa aofisini na kutembea nchi nzima akitangaza wenye migogoro ya ardhi waje na hatekelezi jukumu lake la msingi na taifa linamuona "hero"
Wataalamu wanakwambia maendeleo ya kwanza katika mji wowote ni mpango wa makazi, huo ndiyo unarahisisha huduma zote za jamii. watu wanakaa kwa ustaarabu.
lakini usipoanga kwanza watu wanakaa kama wanyama na pili maisha ya watu yanakuwa magumu zaidi.