Angalia hapa kama unamtoto chekechea

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Chekechea ni shule ya vidudu ya watoto wadogo sana wengine kuanzia mwaka mmoja ambao wanahitaji huduma na mapenzi ya karibu sawa na mama zao. Lakini utakuta shule zingine za aina hii wanaajiri watoto wadogo kucheza nao na matokeo yake hawa watoto wanawatesa na kuwapiga sana hawa viumbe malaika ambao hata kuongea hawawezi.

Hakikisha unakuwa makini na shule hizi, kagua kabla ya kumwacha mwanao kuona ni watu wa aina gani unawaachia wakulele mtoto. Unapomwacha huko shuleni je Unajua mwanao anapatwa na nini akiwa shuleni? Je kuna tabia unaziona kwa mtoto anaporudi shuleni? Amekua mkiya sana au muoga sana? Ana michubuko? Je unamkagua? Au haumkagui?

Video hii hapa ni ya kusikitisha sana ambayo inaonesha jinsi shule moja ilivyokuwa ikiwatesa, kuwapiga na kuwafanya kama mpira wa kuchezea watoto waliletwa ili wawatunze:



#Chukua tahadhali!
 
Tatizo kila kitu kimekuwa biashara hapa, wenzetu wa magharibi walianza kindergartens tangu mwaka 1850 na vikwazo ni vingi sana,

Waalimu lazima wawe wanesomea kulea hao watoto na kuwa wavumilivu wa hali ya juu na kujua tabia (behavior) za watoto.

Kindergarten zilifunguliwa kwa mara ya kwanza huko ujerumani kwa ajili ya wafanyakazi kuwaacha watoto wao pindi wanapokuwa kazini na Amerika walipofungua walikuwa wanachukua mwongozo kutoka Germany kwa sababu walikuwa hawajui namna ya kuanza sasa swali Je sisi tuna waleaje wazuri?

Sishauri kumpeleka mtoto chini ya miaka 3 tena acheze kwa masaa mawili au matatu.

Kweli kuna binadamu wabaya child abuse na paedophile (Psychiatric Disorder) hapo ni pa kuangalia sana na wenye shule ni lazima wajue backgrounds zao wakishirikiana na social workers na serikali pia wawe wanafanya mzunguko wa mara kwa mara kwenye preschools hizo
 
Dah nimeiona hio clip Sijaelewa kitu ki 1
Huyo dg wa kiume anayepiga Watoto na ye ndo mlezi wao au vp
 
Back
Top Bottom