Angalia guide book mpya ya NACTE 2016/2017 na majina ya waliochaguliwa

Angalia guide book mpya ya NACTE 2016/2017 na majina ya waliochaguliwa

INFOT 23

Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
18
Reaction score
12
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) NA KUTANGAZWA KWA MAJINA YA WAOMBAJI UDAHILI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA
Date Posted: 22nd July 2016 00:00:41 Posted By: NACTE

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.

Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.

Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi. Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 22 Julai, 2016
 
Samahani naomba kuuliza kidogo juu ya hili.

ina maana waliomaliza form six mwaka huu nao wanaeuhysiwa ku apply? na je baada ya maombi haya kufungwa watafungua lini tena?
 
Samahani naomba kuuliza kidogo juu ya hili.

ina maana waliomaliza form six mwaka huu nao wanaeuhysiwa ku apply? na je baada ya maombi haya kufungwa watafungua lini tena?
form six wameshaanza kuapply tcu mda kidgo umepita,kuhusu kifungua tena mkuu bado haijulikani ni lini mara baada watakapofunga
 
Nimejaribu kuangalia hiyo guidebook nimeona kama haijamzungumzia mtu wa form six alikosa vigezo vya kuingia degree sasa anataka aombe diploma kupitia nacte ila nimeona tu kwengine uwe na d nne za form 4 au uwe na nta level nk sasa sijaelewa ina maana huyy mtu wa form six nae akitaka kuanza diploma atachukuliwa kwa vigezo kama vya form 4 ama nini
Nawasiliza
 
jaman hizi guidebooks walizoweka mbona sijaona ya ualimu? msaada jaman
 
form six wameshaanza kuapply tcu mda kidgo umepita,kuhusu kifungua tena mkuu bado haijulikani ni lini mara baada watakapofunga
Asante mkuu, lakini mimi naulizia hawa form six ambao wamekosa qualifications za kuingia chuo kikuu na wale ambao wana wish kusoma diploma
 
form six wameshaanza kuapply tcu mda kidgo umepita,kuhusu kifungua tena mkuu bado haijulikani ni lini mara baada watakapofunga
Asante mkuu, lakini mimi naulizia hawa form six ambao wamekosa qualifications za kuingia chuo kikuu na wale ambao wana wish kusoma diploma
 
Nimejaribu kuangalia hiyo guidebook nimeona kama haijamzungumzia mtu wa form six alikosa vigezo vya kuingia degree sasa anataka aombe diploma kupitia nacte ila nimeona tu kwengine uwe na d nne za form 4 au uwe na nta level nk sasa sijaelewa ina maana huyy mtu wa form six nae akitaka kuanza diploma atachukuliwa kwa vigezo kama vya form 4 ama nini
Nawasiliza
Ndio atatumia cheti cha form kuomba kusoma diploma
 
Hivi jamani aliyekosa nafasi akitaka kuaplai tena anatumia pesa nyingine au anatumia plofaili lile la mwanzo kuaplai tena?msaada please maji yako shingoni.
 
Mbona hawakutoa majina ya vyuo vyenye nafasi? Pia sababu hawakutoa kwa nini mwombaji hakuchaguliHilHii ni muhimu
Mkuu hawa nacte naona sasa wamechoka kufanya kazi, haiwezekani kutomwambia mtu nini kimesababisha asichaguliwe halafu wanakuja na general sababu.Hakika kweli sasa nimemuelewa rais wangu Magufuli kuhusu IT wa Tz .
 
Back
Top Bottom