Hii mada ni sensa inayotaka suala la dini liwepo au ni ya ushoga? Idadi ya dini kwangu si tija kabisa maana dini yako hainihusu kabisa mimi wala dini yangu si suala linalokuhusu wewe. Sasa hivi tuko kwenye michango ya kujenga nyumba ya ibada, hata kama najua dini yangu ni half the number of ppopulation, how does that help?
Kwanza chambua (fanya analysis)ya maoni yangu, usivurumishe majibu bila ya kuendana na mtazamo wa maoni halisi. Jibu lako ni finyu wakati maoni yangu ni mapana, fungua macho.
Hata hivyo nakuongeza:
Kuwanayo dini na kuitanganza kuwa nayo ni "proactive deterrence against potential spread of immorality" kwa maana kule kujitangaza kuwa una dini fulani kunakufanya kuji-commit mwenyewe na watu kukuwekea vipimo vya matarajio ya tabia na hulka zako na watakuhumu kutokana na commitment uliyojitangazia.
Na kutokuwa nayo dini au kutojitangaza kuwa nayo ni opportunity ya kufanya mischief on the land bila ya watu kuweza kuku-judge kwasababu unakuwa huna vipimo ulivyoji-commit mwenyewe kwa watu kuweza kukupima kutokana navyo.
Nimekwambia kwamba Sensa ni social profiling ya population husika. Society husika (mfano sisi waTanzania)ikiwa katika profile yetu inaonyesha tumeji-commit katika dini fulani, ina maana kwamba watu wategemee kutupima wao kutokana na commitment tuliyojiwekea wenyewe, yaani diiiiiini zeeeetu, ndugu yangu.
Na ni
1. Diiiiiiini zetu (mfano mafundisho ya Qurani na wanayoiiamini Qurani, na mafundisho ya Biblia na wanayoiiamini Biblia)
2. Sheria zetu zinazopangwa na wabunge wetu, na
3. Mila na desturi zetu za kikabila na kibantu...
Ndio mihimili mitatu ya kutulindia maadili yetu (proactive deterrence against any potential immorality). Katika mihimili mitatu hiyo hapo juu ni upi muhimili madhubuti?????Mimi naamini nambari moja (Diiiiini zeeetu) ndio madhubuti ya hiyo mitatu kutokana na mapungufu yaliyowazi wa hiyo mingine miwili, sheria zitokanazo na wabunge wetu hawa ambao tayari wamesimamia kidete kuondosha kipengele cha dini, au na mila na desturi za kikabila zilizowagawa na kuwadhoofisha mababu zetu dhidi ya wakoloni.
Sasa ukiondosha mmoja madhubuti(kama unavyotegemewa kuondosha mwezi kesho kwa sensa wanayoidhamini hawa hawa wanatuletea haya mambo ya sodoma na gomora) kwa kutumia mradi wa "Millenium Development Goals" na "Haki za binadamu" tutabaki na nini???? Mimi binafsi siamini hawa wabunge wetu wala mila za makabila na kibantu kusimama dhidi ya gharaka hii.
Kwanini maaskofu wasilijuwe na kulitambua hili wakati ndugu zao wavaa vibalaghashia (waislamu) wanaliona na kulitambua hili??? Isitoshe pale wanaposhirikiana na viongozi wa serikali kuwaona ndugu zao wavaa vibalaghashia (waislamu) kuwa wakorofi, basi hiyo inaweza kuonyesha kwamba wao vile vile ni washiriki katika njama, na hivyo nchi yetu imakalia jiti kavu labda wavaa vibalaghashia tu ndio last men/women stand.
Unafahamu ndugu yangu....