Andaa kesho yako, leo muda si rafiki sana

Andaa kesho yako, leo muda si rafiki sana

mriringa

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
783
Reaction score
835
Miaka ya nyuma akili yangu iliwaza kwamba tajiri ni mtu mwenye fedha za kutosha na sikuwahi kuwaza kwamba tajiri mbali na kuwa fedha ila anaongozwa na umiliki wa asset za kutosha.

Tajiri anayemiliki ardhi ya kutosha na ndani yake akaweka mazao ya muda mrefu Hadi kuvuna ni tajiri mwenye maono makubwa na mara nyingi huchekwa kama wametupa fedha zao. Fedha ikikaa bila kuzaliana Haina maana.

Ninachotaka kusema ni kwamba vijana ni muda Sasa wa kuwaza kumiliki ardhi walau usiwe na chini ya eka 10+ na hakikisha unamiliki kisheria na panda miti ya mbao au matunda na uitunze kama mboni ya jicho lako.

Nilimchukia sana baba yangu kumiliki ardhi zaidi ya eka 100 kipindi mdogo na niliona anajitesa wakati ni mtumishi na anakula mshahara mkubwa tu ila Sasa Kila mwaka anauza viwanja zaidi 50 katika umri wake wa miaka 80 kasoro na hahitaji msaada wowote kutoka kwa watoto wake maana anajiweza kuliko hata sisi watoto wake.

Wakati unaofaa ni sasa na usichague wapi ununue ardhi bali popote inapopatikana ardhi na mfukoni fedha ipo usichelewe kuiandaa kesho Yako ili kuepuka kuja kuwalaumu watoto wako kwamba hawakusaidii.

Mimi nimeamua ni wakati wako eeh mpendwa kuamua Sasa kumiliki ardhi ya kutosha maana Kuna mikoa ardhi bado haiuzwi gharama kubwa.
 
Andaa kesho yako Leo.

Maneno machache ila yanabeba maisha yako.

Tafakari:- Hivi ushawah kujiuliza kama miaka 10 iliyopita (2015) ungepewa uwezo wa Kuona mbele yako ya leo(2025). je ungekuwa na hali kama uliyo nayo sasa?.
Bila shaka ni hapana.

Ungekuwa bora zaidi ya hapo, ungekuwa mtu mwenye mafanikio na malengo yako meng yangekuwa yametimia.

Kwasababu ya Clear Vision.

Well, hatuna clear vision 100% , ila unaweza ukaweka mipango ya Miaka 10 + mbele. Na ikawa ni vision yako.

Mafanikio ya watu weng unayoyaona leo wameyaandaa miaka ming nyuma,

Iwe kazi, biashara, familia, makazi, mahusiano nk.

The Future is NOW.
 
Upo sahihi mkuu. Miaka kumi ukiwa huna vision unaona mingi sana ila kuifikia ukiwa na Hali ya umaskini uleule ni rahisi.

Tuamke japo kwa kuchelewa maana wahenga wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Back
Top Bottom