Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Mimi ni mdau wa umeme kama hili litafanyika jiandaeni kununua unit moja ya umeme kwa 500 au zaidi tanesco wanazalisha umeme kwa hasara sana cost ni kubwa lakini kwa sababu ya intervation ya serikali wanauza bei ya chini haswa
watu wanafikiri utani
shida kuubwa inakuja
 
watu wanafikiri utani
shida kuubwa inakuja
Mkuu kwenye zile isolated plant mfano songea etc zinazotumia mafuta kuzalisha umeme production cost per unit ni zaidi ya 1000 lakini unit 1 haiuzwi bei hiyo ukiwapa watu binafsi kama watazalisha kwa bei hiyo sidhani kama watauza kwa hasara kubwa namna hiyo
 
Ni wapi Muhongo alisema TANESCO wasizalishe umeme kabisa?
 
Alipaswa kuhakikisha Tanesco hainunui umeme
na kama ikinunua basi inunue kutoka mashirika mengine ya umeme
NSSSF mfanno na mradi wao wa makaa ya mawe na kadhalika
au manispaa zingeiuzia umeme tanesco vyanzo vikiwa waste nakadhalika

kama ku privatize kungeanzia na disrtibution....hasa kuunga watu umeme
Tanesco ingelazimishwa other small players wawe wanaunga wateja fast..kuliko wao..
huduma inge improve so fast
Mapendekezo mazuri, let's hope policy makers wanayaona. Taasisi kama NSSF inaweza kuwa na mradi mkubwa wa umeme maana mtaji wanao. Baadala ya taasisi zote za hifadhi ya jamii kujikita kwenye ujenzi wa majumba tu, wanaweza wakafikiria pia ku-diversify investment zao kwa kuwekeza kwenye sekta ya umeme. Naamini taasisi kama hizo zitakuwa na 'huruma' zaidi kwa mlaji kuliko IPTL maana ni taasisi za umma.
 
Nakubaliana na wazo la kuruhusu private sector kuzalisha umeme lakini sikubaliani na hii model ya kulazimisha TANESCO kununua umeme toka kwa private producers. Tanesco mpaka sasa wanayo infrastructure yote toka kuzalisha, kusambaza na mpaka kuuza umeme; hakuna sababu yeyote kuwalazimisha Tanesco kununua umeme badala yake Taneco ndio wawakodishie hao private producers kama wanataka miundombinu ya kusambazia umeme kama wanataka kufanya biashara hiyo. Tanesco waendelee kuzalisha kama kawaida na hao wazalishaji wa binafsi wawe washindani wao lakini kuwalazimisha Tanesco kuacha uzalishaji kuwaachia private sector peke yao hakuta tuletea tija!!

Kama hao private sector watataka kuzalisha ,kuzambaza na kuuza umeme waruhusiwe kujenga miundo mbinu yao kama iavyofanyika kwenye mashirika ya simu na hapo ndipo Tanesco itapata ushindani. Mifano iko mingi duniani ambapo industrial sectors zimeruhusu ushindani wa kweli na tija imepetikana. Sector ya utengenezaji magari kwa mfano huko marekani; zamani kulikuwa na kampuni za GM, FORD na CHRYSLER ndizo zilikuwa zinatengeneza magari yanayotumia mafuta lakini kwa kuwa ushindani katika sector hiyo unaruhusiwa kuna kampuni ya TESLA ambayo siku hizi inatengeneza magari yanayotumia umeme hivyo kulinda mazingira!!!! TESLA ina miundombinu ya kuhudumuai magari yanayotumia umeme ambapo wenye magari hayo huweza kucharge batteries zao bure!

Kuna mambo tunaweza kujifunza toka kwenye mfano huu.
Mkuu, lakini sekta ya umeme sio sawa na sekta ya mawasiliano au magari, hivyo ubinafsishwaji wake ni tofauti. Kwanza tayari Tanesco inanunua umeme toka private producers(IPTL, Songas,etc). Kwani kuna tatizo gani tukisema hebu Tanesco iuze plant yake ya Kidatu kwa taasisi ya umma mfano NSSF? Ili yenyewe ijikite ktk kusafirisha umeme? Lengo la mfumo kama huu ni kuimarisha ufanisi na kuleta ushindani. Ni kama kwenye ngumi, Tyson asingeweza kupambana na Cheka bila ya Tyson kupunguza uzito. Otherwise, nafurahi kwamba sasa haya mambo yanajadiliwa hapa ukumbini, badala ya kuwaachia Tanesco na wanasiasa wafanye yao chumbani.
 
Mkuu, lakini sekta ya umeme sio sawa na sekta ya mawasiliano au magari, hivyo ubinafsishwaji wake ni tofauti. Kwanza tayari Tanesco inanunua umeme toka private producers(IPTL, Songas,etc). Kwani kuna tatizo gani tukisema hebu Tanesco iuze plant yake ya Kidatu kwa taasisi ya umma mfano NSSF? Ili yenyewe ijikite ktk kusafirisha umeme? Lengo la mfumo kama huu ni kuimarisha ufanisi na kuleta ushindani. Ni kama kwenye ngumi, Tyson asingeweza kupambana na Cheka bila ya Tyson kupunguza uzito. Otherwise, nafurahi kwamba sasa haya mambo yanajadiliwa hapa ukumbini, badala ya kuwaachia Tanesco na wanasiasa wafanye yao chumbani

Ungesoma vizuri bandiko ungeelewa kuwa sijasema kuwa sector ya magari au simu ni sawa na sector ya kuzalisha umeme; nilichokuwa naonesha ni model ambayo imetumika kwenye automotive industry kuwa inaweza kutusaidia kuleta ushindani wenye tija!!

Sikubaliani kabisa kuwaTanesco iwauzie mitambo ya uzalishaji ya kidatu NSSF ili wazalishe umeme halafu wawauzie huo umeme Tanesco kwasababu mifuko ya jamii ina kazi maalum na kuzalisha umeme sio moja ya kazi zake!! Tanesco haifanyi vizuri sio kwa sababu ni shirika la umma bali halifanyi vizuri kwasababu haina uongozi mzuri unaojua nini wanatakiwa kufanya!! Uongozi wake hauna weledi. Competition should be encouraged within the energy sector between the public and private sectors for the sector to become efficient.
 
Pole sana Kwa kuwa na akili Za kushikiwa ndio maana hata uuzaji wa mashirika yetu ya umma ni mipango ya serikali Je ulikukuwa ni uwamuzi sahihi ???mfano benki ya NBC iliyo uzwa Kwa bei ya kutupwa.uuzwaji wa nyumba Za serikali Kwa bei Za kutupa pia ulikuwa ni mpango wa serikali Je huu ulikuwa ni uwamuzi sahihi ????usifikili sisi wananchi hatuna akili wala usifikili viongozi ndio wana uchungu na hii nchi kuliko sisi wananchi.
Na mimi ni mwananchi nisiyeamini katika habari za kupika, naomba sauti, video au docments kuthibitisha kauli hiyo ya muhongo vinginevyo unabwabwaja na kuishi katika historia
 
Kuna kitu hujakijua ndio maana unaongea ukihisi hilo jambo ni gumu sana, pole sana aisee hii inchi ni tofauti kabisa na ujuavyo. Hiyo mikataba ni kinyaa tupu wewe huoni unaambiwa ni siri. Shauri lako na pole sana.
Badala ya kunipa pole; wewe unaekijua hicho kitu ndie unatakiwa kusema kuna tatizo gani kwa private sector kuzalisha umeme! Hoja kwamba wanaweza kuzalisha halafu wasituuzie ni hoja isiyo na maana yoyote kwavile kila mwekezaji anaamua kuwekeza only to make profit na hakuna faida pasipo kufaya mauzo!

Narudia; shughuli za uzalishaji hazitafanywa na vyama vya siasa bali na wafanyabiashara wenye lengo la kutengeneza faida. Hilo moja lakini pili msiongee as if hii ni biashara ya matikiti maji; kwamba unayatoa Mkuranga ili upeleke Kariakoo lakini ghafla unaghairi unaamua kuuza rejareja Mbagala na hakuna wa kukuuliza! Hizi ni biashara zinazohusu country core issues with business contracts. Kwahiyo there's no way eti umeshaingia mkataba wa kuiuzia umeme TANESCO halafu ugome kufanya hivyo wakati hiyo itakuwa ni sawa na uhujumu! Tigo wana miaka zaidi ya 20 hivi sasa! Unataka kuniambia wanaridhika kwa kila kitu? Umeshawahi kusikia Tigo wamezima mitambo? Vodacom wana almost 15 years now; ushawahi kusikia wamezima mitambo yao?
 
May be itasaidia mgao hautakuepo,,acha makampuni yajitokeze kuzalisha umeme kunaweza kukuwa na ushindani wa kibiashara na bei kupungua km ilivyo kwenye makampuni ya simu,,
 
kama ku privatize kungeanzia na disrtibution....hasa kuunga watu umeme
Tanesco ingelazimishwa other small players wawe wanaunga wateja fast..kuliko wao..
huduma inge improve so fast
Yaani una-propose kama ni private sector basi wafanye kwenye distribution... are you serious? Yaani mtu binafsi ndo unampa mamlaka ya kukata na kuwasha umeme?! Assume mimi ndie distrubutor mwenyewe ambae nina affiliation na maadui wa nje! Siku ya siku, mna-organize mnakubaliana wakae stand-by mahali walipopanga kuhujumu na muda ukifika, una-create electric surge kwenye eneo husika na umeme unakatika kwa hata dakika 5 tu! Umeshapata kufikiria organized damage ambayo inaweza kupatikana ndani ya dakika 5 zisizokuwa na umeme ambazo zinaweza kuwa technically justified kwamba kulikuwa na matatizo ya kiufundi!!!! Kama issue ni kuunga kwani wanaounganisha umeme wa REA kule vijijini ni nani?
 
Kwanza niseme nimemuunga mkono Magufuli kwa kurekebisha kosa alilolifanya
la kumteua Eliai\kim Mawsi TRA bila kujali sana watu watasemaje..
kitendo cha kumuondoa haraka Maswi ni kizuri....

Sasa cha kushangaza ni kuwa toka waziri Muhongo ateuliwe
ni kama amekuja na 'sera zake binafsi' kuhusu umeme

Muhongo hataki kabisa Tanesco wazalishe umeme wao.....mara kwa mara
anazungumza na kusema 'WAWEKEZAJI WAJITOKEZE' au 'UZALISHAJI WA UMEME UFANYWE
NA SEKTA BINAFSI'...hili amerirudia zaidi ya mara 10 toka apewe hii wizara

Kibaya zaidi ameanzisha mchakato ambao ulizuiwa alipoondolewa wa kubinfsisha
'uzalishaji umeme unaofanywa na Tanesco'

Anataka Tanesco ibaki na kusambaza na kusafrisha umeme tu huku 'IKINUNUA UMEME'
kutoka kwa 'HAO WAWEKEZAJI BINAFSI ANAOWAPIGIA DEBE'

Yaani sio tu wawekezaji binafsi waje kuwekeza vyanzo vipya lakini na 'vyanzo vyote vya Tanesco'
viende mikononi kwa wawekezaji binafsi....

Ikumbukwe Tanesco haiwezi kununua umeme na kuuza....sababu 'umeme wa kununua ni ghali sana'

Tanesco ili iweze kununua inalazimika kupewa ruzuku na Serikali kuu'

Achilia mbali baadhi ya hao wawekezaji binafsi wanatumia mitambo ambayo ilinunuliwa na Tanesco..
lakini wanaitumia kuwauzia umeme Tanesco kwa bei ghali na kodi hawalipi kabisa au kulipa kidogo sana

Hiii yote ilikuwa ni mipango ya Muhongo kabla hajaondolewa....
alipoondolewa Tanesco ikaanza kujiimarisha kuzalisha yenyewe umeme...

Sasa karudi na keshaanza tena kuwapigia debe 'wawekezaji binafsi'

Swali ni je Magufuli ana yaa approve yote haya?

Hii ni sehemu ya mipango mipya ya Magufuli?

kwamba Tanesco inunue umeme asilimia 90 au 100 ndo iuze?
ina uwezo huo?
itasaidia kweli?

ni mipango ya serikali yote au Muhongo binafsi?
Nilidhani hata anampango wa kujenga ukuta daraja pale wami ili maji yatumike kisawasawa kuzalisha umeme! Hivi kwanini akili za hawa mawaziri wachache zinawaza tu wawekezaji wawekezaji hawawezi kuwa wabunifu wa tiba ya milele au hata nusu karne ya moja wapo ya matatizo sugu kama hili la umeme? Jamani tuna mito mingapi inashindana kujaza bahari ya Hindi maji hapa Tanzania!!? Wao kazi kupigania wawekezaji wafanye kazi ndogo na zenye kulikosti taifa hasara juu ya hasara kila siku!? Fungeni na kusali enyi mawaziri ili MUNGU awape maono sio kilakitu unaweza kufanya bila muongozo wa kutoka kwa MUNGU! Inatia aibu,eti mpaka moto wa kupikia uwashiwe na mwekezaji fungukeni jicho la tatu na mkatae sababu zozote za uvivu wa kufikiri na rushwa
 
Me nataka kuwe na makampuni binafsi yanayozalisha umeme na kutuuzia wananchi direct kwa sababu umeme wa tanesco ni ujinga mtupu
 
Tumepoteza viwanda vingi na vingi havizalishi sababu ya huu uwekezaji kwenye umeme tusije rudia makosa Hawa watu wengi ni wajanja wajanja yasije yakawa Yale ya NET GROUP SOLUTION sio sifa kubinafsisha kila kitu wazalishe Ila Tanesco au kampuni ya Uma kusimamia uzalishaji lazima iwepo sasa watu wanataka plant ziuzwe halafu iweje sasa hatujui vitu hivi serikali imemwaga mabilioni kuvifanya vilivyo leo Unataka kumkabidhi mtu for a cheap price lazima kesho muanze kulalamika kama ilivyo kawaida ya Mtanzania
 
Maswali yako mbona ya kitoto sana? Tena serikali ifanye haraka kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kuzalisha umeme. Nchi zilizoendelea zinatumia utamaduni huo. Serikali ibaki na kazi moja tu ya kusambaza umeme kwa wananchi. Mambo ya uzalishaji waachiwe sekta binafsi. Wapo akina IPTL, SONGAS, AGGREKKO na wengine ambao wamekuwa wakifanya hivyo tangu muda mrefu. Cha muhimu hapa ni serikali kuwapangia bei hao wazalishaji ili wasituumize wananchi

Nina hakika, ama unajua ama hujui kabisa kuhusiana na hii issue ya uzalishaji na ununuaji wa umeme una faida zipi zikiwa mikononi mwa serikali au taasisi binafsi. Na ikiwa hujui sana ila unaendeshwa tu ni mihemko ya ushabiki wa kisiasa, acha kuchangia. hili ni swala nyeti linalohitaji michango na mijadala ya kina kuliko utani ulionao. Na kama unajua vizuri na mchango wako ndio huo basi tuamini tu kuwa kuna baadhi ya watanzania wenzetu hawajali na wala hawana mpango na maendeleo ya nchi. Sihitaji confrontation yoyote na wewe, ila naheshimu mawazo chanya ya wachangiaji wenye uchungu na mawazo yanayonia ustawi wa nchi yetu
 
kwa hali ilivyo kwa yanaipata kutoka IPTL nk, lazima tujifunze kitu kabla ya kukurupuka
 
The Boss,umetoa mada nzuri sana kwa maana kwamba kama Umeme,Maji na Usafiri wa daladala kuwekea kwa ajili ya uwekezaji basi kama Taifa tumekwisha.Maana wawekezaji watatuhujumu sana na hili la viongozi wetu kutenda rushwa na ufisadi wajue fika sasa wanaenda kuliumiza Taifa.
Sijaona sababu ya kuibinafsisha Tanesco ULA kwa vile ni shirika kubwa wangeligawa moja liwe la Ugavi na kingine la usambazaji.Na kiukweli wakaboresha miundo mbinu ya tanesco na kununua mitambo mipya ya kuzalisha umeme.
Since hakuna Mtawala mwenye uchungu na Taifa basi tutegemee huu ujinga kufanyia.Muhongo ameishi sana nje sidhani kama.kuna nchi umeme wake umebinafsishwa.Unaweza kuwa Prof wa Miamba lakini ukakosa maarifa na hekima ya uongozi
Pili mbaya zaidi tumegawanyika katika sehemu tatu kubwa:
1.Hawa ni wanufaikaji wa ufisadi na rushwa na uzembe wa watawala wetu,hawa hata uongee njema as long as unachallange Utawala utabezwa tu.
3.Kuna wale tunaoangalia Ukanda gani unetoa changamoto hiyo Kaskazini ,kusini,mashariki au Magharibi basi kama ni Kaskazini utasakamwa na Ukaskazini wako mpaka ujutie kwanini ulizaliwa huko.
3.Kuna wale wanaccm kindakindaki hawa wanadhani ukichallange utawala basi humtakii mema mtawala.

Na mwisho kwa sababu tumeamua kukubali ubaguzi tusitegemee kushinda kwenye vita vya Rushwa na Ufisadi.
Pole mtoa mada
 
Muongo kawekwa pale tayari akiwa na kashfa ya escrow,...na ufanyaji kazi wake unaeleweka,..
hawezi kazi mohongo,..
ila ukiona vyaelea ujue vimeundwa.,...
yule kawekwa pale apige dili wandugu,..
 
Maswali yako mbona ya kitoto sana? Tena serikali ifanye haraka kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kuzalisha umeme. Nchi zilizoendelea zinatumia utamaduni huo. Serikali ibaki na kazi moja tu ya kusambaza umeme kwa wananchi. Mambo ya uzalishaji waachiwe sekta binafsi. Wapo akina IPTL, SONGAS, AGGREKKO na wengine ambao wamekuwa wakifanya hivyo tangu muda mrefu. Cha muhimu hapa ni serikali kuwapangia bei hao wazalishaji ili wasituumize wananchi
We mwenyekiti wa wapumbavu, hii sio siasa uchwara yako uliozoea, hapa yanaongelewa mambo ya kitaalamu. Hivi unaujua mzimu mmoja uitwao Capacity Charge? Unaelewa athari zake kwenye suala zima la umeme, hasa bei kwa mlaji?

We subiri thread za mipasho na fitina za kisiasa, haya waachie members wengine wenye uelewa na masuala ya umeme na mikataba yake ya kinyonyaji.
 
Usal
nadhani pia kwa usalama wa uchumi na taifa kwa ujumla utaratibu wa kubinafsisha uzalishaji wa umeme huenda ukawa hatari!fikiri kama mzalishaji kwa sababu yoyote ile akashindwa kuelewana na TANESCO na kuamua kusitisha uzalishaji nini kitatokea...nchi inaweza kuwa gizani!na vipi huyo mzalishaji akisema hapati faida au ghafla 'akafirisika' kama home shopping centre...tutakaa gizani!!!!
Usalama unauona kwenye Umeme tu Mkuu? Maji walipewa city water hukuoiona hatari hapo? Muhongo yuko sahihi Tanesco ni wababaishaji waondoke.
 
Back
Top Bottom