Kuna vitu viwili ambavyo kwa maoni yangu serikali isingeachia sekta binafsi ivitawale. Kimoja ni uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme na cha pili ni uagizaji na uuzaji wa nishati ya mafuta. Hivi ni vitu vya muhimu sana kwa uchumi na usalama wa nchi na nadhani ni kosa kuiachia sekta binafsi. Nilikuwa nangoja nisikie wakisema kuwa wanafufua kiwanda cha uchakataji wa mafuta ghafi-TIPER- ambapo serikali ingeagiza na kuchakata mafuta hayo humu nchini. Bei ya mafuta ingepungua sana na serikali ingepata faida kubwa licha ya ajira lukuki ambazo zingetengenezwa. Kwa sasa ambapo bei ya mafuta katika soko la dunia ni $30 sidhani kuwa bei ingekuwa wastani wa sh. 1800 kwa lita ambazo tunauziwa kwa sasa. Ni ukweli unaouma kuwa TANESCO ilishanyanganywa uwezo wake wa kuzalisha umeme isipokuwa ule wa vyanzo vya maji. Kwa gesi yetu ungedhani kuwa umeme ushuke bei lakini sivyo. Kuna vigogoi wanaoitwa wawekezaji ambao wamekopeshwa na serikali pesa za kununulia majenereta na wameyategesha wakaunganisha na gesi na wao ndo wanaoiuzia TANESCO umeme. Wananunua gesi kwa makampuni ya gesi inayoitwa ni yetu??? na wanazalisha umeme na kuiuzia TANESCO kwa bei juu. Nini kingekuwa kigumu kwa tanesco kumiliki majenereta hayo? Ilianza wakati wa Net group solutions wakati ule wa Mkapa....!!!!
niliiona hatari wakati wakipewa city water...nilisikitika ila sikuwa na platform ya kusemea kama ilivyo leo!usalama wa taifa upo sehemu nyingi zaidi ya umeme...lakini mada iliyoletwa mbele yetu inahusu umeme...hebu jaribu kufikiri kama umeme utakosa mbadala yake itakuwa nini!!viwanda...ofc...majumbani...hata hiyo mitambo ya kusukuma maji itasimama...si wazo jema kuruhusu 100% umeme uzalishwe na kampuni binafsi...ila wanaweza kushiriki katika kuzalisha umeme ili hali TANESCO nayo ikiendelea...Usal
Usalama unauona kwenye Umeme tu Mkuu? Maji walipewa city water hukuoiona hatari hapo? Muhongo yuko sahihi Tanesco ni wababaishaji waondoke.
Lizaboni,sasa hivi hiyo bei ya umeme wanaozalisha AGGREKO,Pan African Energy, IPTL, SYMBION na wengine,serikali ndio wamewapangia hiyo bei?Maswali yako mbona ya kitoto sana? Tena serikali ifanye haraka kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kuzalisha umeme. Nchi zilizoendelea zinatumia utamaduni huo. Serikali ibaki na kazi moja tu ya kusambaza umeme kwa wananchi. Mambo ya uzalishaji waachiwe sekta binafsi. Wapo akina IPTL, SONGAS, AGGREKKO na wengine ambao wamekuwa wakifanya hivyo tangu muda mrefu. Cha muhimu hapa ni serikali kuwapangia bei hao wazalishaji ili wasituumize wananchi
Hivi unaelewa hata tunacho andika humu?
au uko kwa kazi ya kumtetea Muhongo?
Hakuna anaepinga wawekezaji kufanya generation lakini why wachukue generation ya Tanesco?
why wasianzishe za kwao?
Umeme wa dharula haujui kuwa ilikuwa ni dili la kupangwa?
hujui kweli au unajifanya hujui?
Apparently Muhongo kajibu Bungeni hoja za bandiko hili few minutes ago. Still anakaribisha wawekezaji na ameongeza kuwa miradi ya uzalishaji na uboreshaji wa miundombinu ya umeme inaendelea.
Jembe la udongo!Mzimu wa Muhongo unawasumbua kwelikweli tueleze ni wapi na lini muhongo katamka kkwamba tanesco haitazalisha umeme??? Kinachosisitizwa na jembe hili ni wawekezaji binafsi pia kuzalisha umeme ili uwe wa kutosha na si kutegemea tanesco pekee. Kukiwa na mgawo wa umeme mnalalamika monopoly ya tanesco, watu wakialikwa kuzalisha umeme zaidi mnalalamika ooohhh tanesco inanyang'anywa jukumu lake. Acheni jembe lifanye kazi hizi cheap politics hazitawasaidia
umenichekesha sana mkuunadhani pia kwa usalama wa uchumi na taifa kwa ujumla utaratibu wa kubinafsisha uzalishaji wa umeme huenda ukawa hatari!fikiri kama mzalishaji kwa sababu yoyote ile akashindwa kuelewana na TANESCO na kuamua kusitisha uzalishaji nini kitatokea...nchi inaweza kuwa gizani!na vipi huyo mzalishaji akisema hapati faida au ghafla 'akafirisika' kama home shopping centre...tutakaa gizani!!!!