Kwa ajili ya usalama wa nchi ndio maana usambazaji unaachwa mikononi mwa TANESCO!
Nimtetee Muhongo kwa misingi ipi? Maswali ambayo nimekuuliza hakuna hata moja ambalo umejibu! By the way, unapohoji kwanini wasianzishe za kwao; unamaanisha nini hasa? Kwani Songas leo hii wanapozalisha umeme si kwamba wameanzisha za kwao? Kwani Aggreko wanapozalisha umeme leo hii unadhani wanatumia mitambo ya TANESCO? Ikiwa kampuni X inazalisha umeme ni kwamba from the grassroots wanachoanzisha ni cha kwao! Ikiwa wanataka kuzalisha umeme wa mafuta... watalazimika kununua majenereta ya kuzalishia umeme na watalazimika kuagiza mafuta kwa ajili hiyo! The same apply kwa watakaokuwa wanazalisha kwa gas, upepo, maji n.k! Sasa ni nini hicho unachosema kwanini wasianzishe cha kwao?
Halafu unapohoji "kwanini wachukue generation ya TANESCO" unamaanisha nini hasa? Nina mashaka wewe ndo hujaelewa vinginevyo ni generation ya TANESCO ipi unayosema wanataka kuchukua? Kwani IPTL, Songas, Aggreko, Symbion wamechukua generation ya TANESCO?
Kwamba umeme wa dharula ulikuwa deal la kupangwa! Ina maana ule ukame wa 1991 ambao ulipelekea IPTL ulikuwa ni wa kupangwa? Ina maana ile 2007/2008 hakukuwa na matatizo ya umeme? Kinachopangwa ni upatikanaji wa hao wazalishaji lakini ukisema kwamba hata ile dharula ni ya kupanga wakati unafahamu kabisa kwamba wakati ule tulikuwa tunatgemea chanzo kimoja tu cha maji basi sidhani kama huu mjadala utafika mwisho