Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Anayoyasema Muhongo katumwa na Magufuli?

Wapi wewe unapata hizi habari za TANESCO wanazuiwa kuzalisha? Wapi unapata hii ya "generation ya Tanesco" (sic) iwe ya kwanza kubinafsishwa? Na hayo mengine yote ya "why itakiwe kununua asilimia 90" unayapata wapi?

I must say you very ill informed. Embu hao wanaokulisha hizo information waulize kuhusu uzalishaji wa Kinyerezi I na Kinyerezi II?
Cheap politics jamaa nimemdharau sana leo
 
Muhongo labda anazungumzia wawekezaji wa nje,
Mana wawekezaji wa ndani wana hela ya biashara bya maandazi by Muhongoo
Haya ni moja ya maneno mliyomlisha profesa ili kumjengea chuki na watanzania asichotaka muhongo ni wawekezaji wababaishaji bhaaaaass. Na katika hili alitoa angalizo tu Kuwa uwekezaji katika uchimbaj wa gesi ni pata potea kwa mitaji yetu watanzania tunaweza wekeza kwenye miradi mingine kama juice. Yani wabongo bana
 
Kama ni kweli kuwa uzalishaji umeme uwe wa private sector, it is shocking kwani tunaelekea kwenye kulipa capacity charges kama zile za IPTL. Tuelemishwe itakuwaje. Sipendi huo mpango. Tumechoka na kulipa capacity charges!
Mleta mada kaleta habari za kupika hakuna sehemu muhongo alitamka hayo maneno anachotaka muhongo ni wazalishaji wa umeme kuongezeka ili kuwa na umeme wa uhakika na unaotabirika. Tanesco hatanyang'anywa hilo jukumu bali atasaidiana na wawekezaji wengine kuzalisha umeme. Hata sasa wako watu kwa mfano wanazalisha umeme wa maji huku mbinga, mawengi na chipole na wanasaidia wananchi wa huku kupata umeme. SUALA LA CAPACITY CHARGE MUHONGO ALISHAPIGA MARUFUKU KUINGIA MIKATABA YENYE HICHO KIPENGELE NA TANESCO WANALIJUA HILO
 
Sio swala geni tume ona ni Wizi mtupu.pia hiyo distribution mmeiacha kwajili ya sababu zenu Za kisiasa na sio mapenzi mliyo nayo Kwa wananchi hakuna kampuni binafsi itakayo kubali kuchukua distribution
Kama una pointi vile kumbe upupu mtupu someni documents jamani muone mipango ya serikali yetu si kuja na mipango yenu ya vyumbani
 
Kuna kitu hujakijua ndio maana unaongea ukihisi hilo jambo ni gumu sana, pole sana aisee hii inchi ni tofauti kabisa na ujuavyo. Hiyo mikataba ni kinyaa tupu wewe huoni unaambiwa ni siri. Shauri lako na pole sana.
Tutajie nchi ambayo huanika mikataba yake peupe. Iweke hapa
 
Sawa mkuu, japo naweza sema mimi nilishaelewa kabla hata ya uchaguzi. Hii issue ilitaka ifanyike tangu 2015 katikati mikakati ilishaanza kuna kimbembe kilitokea ikawa ngumu kumeza ikapigwa pending mpaka 2017 bahati mbaya mwenye mkakati akaingia ktk kashfa akakaa pembeni workers wakafurahi kidogo, sasa baada ya uchaguzi kabla ya kutangazwa mawaziri lilitokea neno moja linaitwa 2020 ndipo mpango ufanyike sasa baada ya mawaziri kutangazwa si ndio karudi yule yule so haieleweki bado kichwani mwake kuna neno 2017 au kichwa kimekua updated to 2020. Stay tune
Tuache kuishi katika historia hapa anachoangalia muhongo ni uwepo wa umeme wa kutosha basi hizo kashfa wamebaki nazo waliomuundia zengwe, sasa jembe liko kazini mnaofukua makaburi shauri zenu hapa ni aluta continua
 
Kama hat
Wapi wewe unapata hizi habari za TANESCO wanazuiwa kuzalisha? Wapi unapata hii ya "generation ya Tanesco" (sic) iwe ya kwanza kubinafsishwa? Na hayo mengine yote ya "why itakiwe kununua asilimia 90" unayapata wapi?

I must say you very ill informed. Embu hao wanaokulisha hizo information waulize kuhusu uzalishaji wa Kinyerezi I na Kinyerezi II?

Kama hata TV huangalii
wala magazei husomi nitakusaidiaje?
iko all over the media google it
 
Pole sana mzalendo , hili ndilo lilimfanya magufuri azibe masikio na kutuletea mtu yuleyule aliyetimuliwa bungeni , tena eneo lilelile !
Kashfa za kupika peleka kwa mkeo. HAPA KAZI TU. Mmeumbuka wazee wa vitalu haaaahaaaaaa, naona mnaanza tena 😛😛😛😛😛😛
 
Mtoa mada una hoja ya kitoto kama alivyosema mmoja wa wachangiaji. Hakuna mahala Waziri Muhongo amezuia Tanesco wasizalishe umeme...na haingii akilini kufanya hivyo, badala yake anahimiza sekta binafsi kuongeza uzalishaji. Muhongo alishatamka mara kadhaa mpango wa kuzalisha megawatt 10,000 ifikapo 2025...hii pia ipo kwenye mpango kabambe wa uzalishaji wa miaka 10. Soma hii Tanzania Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap 2014/15 — Ministry of Energy and Minerals

Mbona Muhongo kaongea na tv imemuonesha?
asilimia 90 ya uzalishaji itatoka kwa wawekezaji binafsi
na Tanesco generation inaondolewa
hukuelewa nini labda?
 
Hii kitu kiujumla inaitwa 'deregulation of electricity market', ni kitu kimefanyika nchi nyingi na kinaendelea kufanyika. Dhana ya mfumo huu ni kwamba shughuli za umeme (uzalishaji, usambazaji na uuzaji umeme) ni ngumu (complex) kiasi kwamba zinapofanywa na kampuni moja (e.g.TANESCO) kunakuwa hakuna ufanisi. Hivyo shughuli hizi zikigawanywa na kupewa makampuni mbalimbali basi kutakuwa na ushindani utakaopelekea kuwepo huduma bora na ufanisi

Mfano mzuri ni sekta ya mawasiliano ya simu (telecommunications). Utakuwa unakumbuka enzi za TTCL ambapo hata ukiwahonga wanaweza wasikuunganishie simu nymbani kwako. Hakukuwa na huduma nzuri kwa wateja-bili za kubambikiza, n.k. Baada ya 'deragulation', sasa tunapata dakika kumi na tano kwa shilingi 500.

Sasa katika kujibu swali lako, sekta ya umeme iko tofauti kidogo na sekta nyingine. Kama unafanya deregulation, lazima uhakikishe hakuna kampuni ina nguvu kubwa kupita kiasi katika soko, maana itazuia ushindani na inaweza hata kupandisha bei ya umeme kwa 'kutengeneza uhaba wa umeme' ambao kimsingi haupo ili kufanya bei ziwe juu. Nchi zote zinazofanya deregution ya umeme moja ya masharti zinazoyafuata ni kubinafsisha makampuni yenye monopoly. So kuuzwa kwa Tanesco ni kuzuia kitu inaitwa 'Market Power'. Ndo kusema Tanesco itatakiwa ibakiwe na kazi ya kujenga na 'kupangisha' transmission and distribution lines tu. Kutakuwa na makampuni ya uzalishaji umeme ya binafsi (tayari yapo-IPTL,Songas), makampuni ya kuuza umeme na kampuni moja ya umma ya kukodisha na kujenga transmission lines. Kenya hili wameshalifanya.

Kiujumla hili ni suala ya kulifanya kwa ueledi na uaminifu mkubwa maana kuna ujanja ujanja mwingi unaweza kukwamisha mambo kama ilivyotokea California, USA. Kuna wajanja watabuku transmission lines ili kuwazuia wengine wasipitishe umeme wao na hivyo kuzuia wengine wasifanye biashara. Kuna wengine watajifanya wanazifanyia plants zao matengenezo kumbe wanataka kutengeneza uhaba wa umeme ili bei iwe ya kuruka.

Mwisho, kama alivyosema mdau, hili wazo lipo zaido ya miaka 10 iliyopita, lilikosa fedha za utekelezaji tu.

Muhongo mwenyewe amekwenda Uganda kaona lilivyo feli
nchi nyingi zilizo fanya hilo...zinajuta

Mwenyewe ushasema inahitajika uaminifu wa hali ya juu liweze fanikiwa
halafu unasahau hii ni Tanzania?

Already baadhi ya hizo kampuni hata kodi tu hazilipi
achilia mbali ambazo zinazalisha kwa kutumia mitambo ya Tanesco ..mitambo iliyoipata kiujanjaujanja
mbona jibu liko waazi kabisa
 
Hii kitu kiujumla inaitwa 'deregulation of electricity market', ni kitu kimefanyika nchi nyingi na kinaendelea kufanyika. Dhana ya mfumo huu ni kwamba shughuli za umeme (uzalishaji, usambazaji na uuzaji umeme) ni ngumu (complex) kiasi kwamba zinapofanywa na kampuni moja (e.g.TANESCO) kunakuwa hakuna ufanisi. Hivyo shughuli hizi zikigawanywa na kupewa makampuni mbalimbali basi kutakuwa na ushindani utakaopelekea kuwepo huduma bora na ufanisi

Mfano mzuri ni sekta ya mawasiliano ya simu (telecommunications). Utakuwa unakumbuka enzi za TTCL ambapo hata ukiwahonga wanaweza wasikuunganishie simu nymbani kwako. Hakukuwa na huduma nzuri kwa wateja-bili za kubambikiza, n.k. Baada ya 'deragulation', sasa tunapata dakika kumi na tano kwa shilingi 500.

Sasa katika kujibu swali lako, sekta ya umeme iko tofauti kidogo na sekta nyingine. Kama unafanya deregulation, lazima uhakikishe hakuna kampuni ina nguvu kubwa kupita kiasi katika soko, maana itazuia ushindani na inaweza hata kupandisha bei ya umeme kwa 'kutengeneza uhaba wa umeme' ambao kimsingi haupo ili kufanya bei ziwe juu. Nchi zote zinazofanya deregution ya umeme moja ya masharti zinazoyafuata ni kubinafsisha makampuni yenye monopoly. So kuuzwa kwa Tanesco ni kuzuia kitu inaitwa 'Market Power'. Ndo kusema Tanesco itatakiwa ibakiwe na kazi ya kujenga na 'kupangisha' transmission and distribution lines tu. Kutakuwa na makampuni ya uzalishaji umeme ya binafsi (tayari yapo-IPTL,Songas), makampuni ya kuuza umeme na kampuni moja ya umma ya kukodisha na kujenga transmission lines. Kenya hili wameshalifanya.

Kiujumla hili ni suala ya kulifanya kwa ueledi na uaminifu mkubwa maana kuna ujanja ujanja mwingi unaweza kukwamisha mambo kama ilivyotokea California, USA. Kuna wajanja watabuku transmission lines ili kuwazuia wengine wasipitishe umeme wao na hivyo kuzuia wengine wasifanye biashara. Kuna wengine watajifanya wanazifanyia plants zao matengenezo kumbe wanataka kutengeneza uhaba wa umeme ili bei iwe ya kuruka.

Mwisho, kama alivyosema mdau, hili wazo lipo zaido ya miaka 10 iliyopita, lilikosa fedha za utekelezaji tu.

Muhongo mwenyewe amekwenda Uganda kaona lilivyo feli
nchi nyingi zilizo fanya hilo...zinajuta

Mwenyewe ushasema inahitajika uaminifu wa hali ya juu liweze fanikiwa
halafu unasahau hii ni Tanzania?

Already baadhi ya hizo kampuni hata kodi tu hazilipi
achilia mbali ambazo zinazalisha kwa kutumia mitambo ya Tanesco ..mitambo iliyoipata kiujanjaujanja
mbona jibu liko waazi kabisa
 
Wapi wewe unapata hizi habari za TANESCO wanazuiwa kuzalisha? Wapi unapata hii ya "generation ya Tanesco" (sic) iwe ya kwanza kubinafsishwa? Na hayo mengine yote ya "why itakiwe kununua asilimia 90" unayapata wapi?

I must say you very ill informed. Embu hao wanaokulisha hizo information waulize kuhusu uzalishaji wa Kinyerezi I na Kinyerezi II?

Huo mpango upo muda mrefu na umesharipotiwa na vyombo vya habari vya bongo. Just google it. Hata ZZK ameshawahi kuuongelea bungeni. Haukutekelezwa kwasabau ya uhaba wa pesa-zinahitajika trilioni zaidi ya 10. Huo mfumo sio kitu kipya, kimefanywa toka miaka ya 90 na nchi kama Chile na zingne za Amerika kusini. Moja ya masharti muhimu ya mpango huo ni kubinafsisha uzalishaji wa shirika kuu (monopoly utility), yaani Tanesco iuze plants zake za uzalishaji kama Mtera, Kidatu, Kihansi, n.k. Wanunuzi sio lazima wawe watu/kampuni binafsi, hata Halmashauri zaweza kununua mitambo hiyo.

Kwanini ni lazima Tanesco iuze plants zake? Ili kuruhusu uwepo ushindani. Kama unataka watu washindane mbio, basi wote waanzie sehemu moja. Sio mwingine ameshakimbia mita 500, halafu unataka ashindane na ambaye hajaanza. Pia lengo ni kufanya sekta za umeme zenye ushindani zitenganishwe. Katika umeme, sekta zenye ushindani ni uzalishaji umeme na uuzaji umeme. Hakuna ushindani katika kusafirisha umeme kwasababu ni kitu kunahitaji mtaji mkubwa sana na ni kazi inayopaswa kufanywa na serikali maana ni kama kujenga 'barabara' ya umeme.

Je mfumo huu ni wa haki? Kuuza mitambo ya Tanesco ili kuipunguzia nguvu ya soko sounds like Ujamaa 101!Kiukweli mfumo huu unaweza usiwa wa haki. Kwanza kunaweza kusitokee kampuni/taasisi ya kununua plant kubwa kama Mtera kwa bei halali na halisi. Pili mkishafanikisha ubinafsishaji, suala la ununuzi, uuzaji na usafirishaji umeme limejaa mianya mingi ya udanganyifu. Matokeo yake ni kwamba japo tunafanya ili kuongeza uzalishaji, kupunguza bei na huduma bora, tunaweza tusipate yote hayo pamoja na kuitoa kafara Tanesco.

Je hali ya umeme ni mbaya kiasi cha kuhitaji mipango kama hiyo? Tanzania inazalisha takribani 2GW za umeme, wakati South Africa inazalisha 45GW za umeme na wana idadi sawa ya watu kama sisi, lakini bado kuna mgao wa umeme huko kwa Madiba. Hapa nataka kuonyesha ni kweli tuna safari ndefu, kiasi kwamba hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa kufanya mambo kwa namna ile ile. Mfano mwingine, Tanzania tuna karibu asilimia 30% ya makazi yenye umeme, South Africa ina 85%. Pia kumbuka rais wetu muda wote wa kampeni amezungumzia viwanda. Pia viwanda vya saruji vinaongezeka na kushusha bei yake na kufanya ujenzi kuwa bei rahisi. Kuongezeka makazi bora kunaenda sambamba na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme.
 
Muhongo mwenyewe amekwenda Uganda kaona lilivyo feli
nchi nyingi zilizo fanya hilo...zinajuta

Mwenyewe ushasema inahitajika uaminifu wa hali ya juu liweze fanikiwa
halafu unasahau hii ni Tanzania?

Already baadhi ya hizo kampuni hata kodi tu hazilipi
achilia mbali ambazo zinazalisha kwa kutumia mitambo ya Tanesco ..mitambo iliyoipata kiujanjaujanja
mbona jibu liko waazi kabisa

Kweli kabisa, nakubaliana nawe. Hata USA kwenye structure na system imara wame-suspend hiyo process ktk baadhi ya states. California watu walipiga hela kwa kutengeneza uhaba wa umeme ambao haupo mpaka ikatangazwa hali ya hatari kutokana na giza. Walijua watu wanachezea mfumo huo mpya na namna gani wanachezea, lakin wakashindwa namna ya kuwachukulia hatua. Labda ni kitu itabid wajukuu wetu ndo watekeleze. But hata hivyo, hata sasa ktk mfumo huu ambao tunadhani ni afadhali, watu wanapiga hela mpaka wanagawana kama njugu kama tulivyoona kwenye escrow.
 
Masuala ya Umeme mumuachie Prof. Mhongo, atawanyoosha!!. Majuzi tu tulikuwa na Simbachawene , mgao usiku na mchana. Mkalalama bora Mhongo arudi, leo karudi -filimbi tele tena!! Daaah wabongo bhanaa!! kila kitu wajuaji
 
Kweli kabisa, nakubaliana nawe. Hata USA kwenye structure na system imara wame-suspend hiyo process ktk baadhi ya states. Labda ni kitu itabid wajukuu wetu ndo watekeleze. But hata hivyo, hata sasa ktk mfumo huu ambao tunadhani ni afadhali, watu wanapiga hela mpaka wanagawana kama njugu.

Alipaswa kuhakikisha Tanesco hainunui umeme
na kama ikinunua basi inunue kutoka mashirika mengine ya umeme
NSSSF mfanno na mradi wao wa makaa ya mawe na kadhalika
au manispaa zingeiuzia umeme tanesco vyanzo vikiwa waste nakadhalika

kama ku privatize kungeanzia na disrtibution....hasa kuunga watu umeme
Tanesco ingelazimishwa other small players wawe wanaunga wateja fast..kuliko wao..
huduma inge improve so fast
 
Mtoa mada Ana point Muhongo anataka kuigawa Tanesco na kuiondolea wajibu wa kuzalisha la muhimu kama ataanzisha kampuni nyingine basi tumuombe Magufuli iwe chini ya serikali maana muwekezaji yupo kibiashara na umeme Tanzania mwingi unazalishwa na kuuzwa kwa ruzuku nitoe mfano mfupi umeme wa mafuta ni ghali sana na kuna maeneo bado yanatumia magenerator kama Mafia na Kigoma ukimpa muwekezaji hawezi kuzalisha ule umeme maana Ile ni huduma isio na faida kabisa
 
Muhongo anadai asilimia 90 ya umeme Tanesco inunue...
hatari sana

Nakubaliana na wazo la kuruhusu private sector kuzalisha umeme lakini sikubaliani na hii model ya kulazimisha TANESCO kununua umeme toka kwa private producers. Tanesco mpaka sasa wanayo infrastructure yote toka kuzalisha, kusambaza na mpaka kuuza umeme; hakuna sababu yeyote kuwalazimisha Tanesco kununua umeme badala yake Taneco ndio wawakodishie hao private producers kama wanataka miundombinu ya kusambazia umeme kama wanataka kufanya biashara hiyo. Tanesco waendelee kuzalisha kama kawaida na hao wazalishaji wa binafsi wawe washindani wao lakini kuwalazimisha Tanesco kuacha uzalishaji kuwaachia private sector peke yao hakuta tuletea tija!!

Kama hao private sector watataka kuzalisha ,kuzambaza na kuuza umeme waruhusiwe kujenga miundo mbinu yao kama iavyofanyika kwenye mashirika ya simu na hapo ndipo Tanesco itapata ushindani. Mifano iko mingi duniani ambapo industrial sectors zimeruhusu ushindani wa kweli na tija imepetikana. Sector ya utengenezaji magari kwa mfano huko marekani; zamani kulikuwa na kampuni za GM, FORD na CHRYSLER ndizo zilikuwa zinatengeneza magari yanayotumia mafuta lakini kwa kuwa ushindani katika sector hiyo unaruhusiwa kuna kampuni ya TESLA ambayo siku hizi inatengeneza magari yanayotumia umeme hivyo kulinda mazingira!!!! TESLA ina miundombinu ya kuhudumuai magari yanayotumia umeme ambapo wenye magari hayo huweza kucharge batteries zao bure!

Kuna mambo tunaweza kujifunza toka kwenye mfano huu.
 
nadhani pia kwa usalama wa uchumi na taifa kwa ujumla utaratibu wa kubinafsisha uzalishaji wa umeme huenda ukawa hatari!fikiri kama mzalishaji kwa sababu yoyote ile akashindwa kuelewana na TANESCO na kuamua kusitisha uzalishaji nini kitatokea...nchi inaweza kuwa gizani!na vipi huyo mzalishaji akisema hapati faida au ghafla 'akafirisika' kama home shopping centre...tutakaa gizani!!!!
Mkuu, uko sawa kabisa!
 
Kwanza niseme nimemuunga mkono Magufuli kwa kurekebisha kosa alilolifanya
la kumteua Eliai\kim Mawsi TRA bila kujali sana watu watasemaje..
kitendo cha kumuondoa haraka Maswi ni kizuri....

Sasa cha kushangaza ni kuwa toka waziri Muhongo ateuliwe
ni kama amekuja na 'sera zake binafsi' kuhusu umeme

Muhongo hataki kabisa Tanesco wazalishe umeme wao.....mara kwa mara
anazungumza na kusema 'WAWEKEZAJI WAJITOKEZE' au 'UZALISHAJI WA UMEME UFANYWE
NA SEKTA BINAFSI'...hili amerirudia zaidi ya mara 10 toka apewe hii wizara

Kibaya zaidi ameanzisha mchakato ambao ulizuiwa alipoondolewa wa kubinfsisha
'uzalishaji umeme unaofanywa na Tanesco'

Anataka Tanesco ibaki na kusambaza na kusafrisha umeme tu huku 'IKINUNUA UMEME'
kutoka kwa 'HAO WAWEKEZAJI BINAFSI ANAOWAPIGIA DEBE'

Yaani sio tu wawekezaji binafsi waje kuwekeza vyanzo vipya lakini na 'vyanzo vyote vya Tanesco'
viende mikononi kwa wawekezaji binafsi....

Ikumbukwe Tanesco haiwezi kununua umeme na kuuza....sababu 'umeme wa kununua ni ghali sana'

Tanesco ili iweze kununua inalazimika kupewa ruzuku na Serikali kuu'

Achilia mbali baadhi ya hao wawekezaji binafsi wanatumia mitambo ambayo ilinunuliwa na Tanesco..
lakini wanaitumia kuwauzia umeme Tanesco kwa bei ghali na kodi hawalipi kabisa au kulipa kidogo sana

Hiii yote ilikuwa ni mipango ya Muhongo kabla hajaondolewa....
alipoondolewa Tanesco ikaanza kujiimarisha kuzalisha yenyewe umeme...

Sasa karudi na keshaanza tena kuwapigia debe 'wawekezaji binafsi'

Swali ni je Magufuli ana yaa approve yote haya?

Hii ni sehemu ya mipango mipya ya Magufuli?

kwamba Tanesco inunue umeme asilimia 90 au 100 ndo iuze?
ina uwezo huo?
itasaidia kweli?

ni mipango ya serikali yote au Muhongo binafsi?
Mimi ni mdau wa umeme kama hili litafanyika jiandaeni kununua unit moja ya umeme kwa 500 au zaidi tanesco wanazalisha umeme kwa hasara sana cost ni kubwa lakini kwa sababu ya intervation ya serikali wanauza bei ya chini haswa
 
Back
Top Bottom