The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,320
- 117,615
Kwanza niseme nimemuunga mkono Magufuli kwa kurekebisha kosa alilolifanya
la kumteua Eliai\kim Mawsi TRA bila kujali sana watu watasemaje, kitendo cha kumuondoa haraka Maswi ni kizuri.
Sasa cha kushangaza ni kuwa toka waziri Muhongo ateuliwe ni kama amekuja na 'sera zake binafsi' kuhusu umeme.
Muhongo hataki kabisa TANESCO wazalishe umeme wao, mara kwa mara
anazungumza na kusema 'WAWEKEZAJI WAJITOKEZE' au 'UZALISHAJI WA UMEME UFANYWE NA SEKTA BINAFSI', hili amerirudia zaidi ya mara 10 toka apewe hii wizara.
Kibaya zaidi ameanzisha mchakato ambao ulizuiwa alipoondolewa wa kubinfsisha
'uzalishaji umeme unaofanywa na TANESCO.
Anataka TANESCO ibaki na kusambaza na kusafrisha umeme tu huku 'IKINUNUA UMEME' kutoka kwa 'HAO WAWEKEZAJI BINAFSI ANAOWAPIGIA DEBE'
Yaani sio tu wawekezaji binafsi waje kuwekeza vyanzo vipya lakini na 'vyanzo vyote vya TANESCO viende mikononi kwa wawekezaji binafsi.
Ikumbukwe TANESCO haiwezi kununua umeme na kuuza....sababu 'umeme wa kununua ni ghali sana'
TANESCO ili iweze kununua inalazimika kupewa ruzuku na Serikali kuu'
Achilia mbali baadhi ya hao wawekezaji binafsi wanatumia mitambo ambayo ilinunuliwa na TANESCO lakini wanaitumia kuwauzia umeme TANESCO kwa bei ghali na kodi hawalipi kabisa au kulipa kidogo sana.
Hiii yote ilikuwa ni mipango ya Muhongo kabla hajaondolewa, alipoondolewa TANESCO ikaanza kujiimarisha kuzalisha yenyewe umeme.
Sasa karudi na keshaanza tena kuwapigia debe 'wawekezaji binafsi'
Swali ni je Magufuli ana yaa approve yote haya?
Hii ni sehemu ya mipango mipya ya Magufuli?
Kwamba TANESCO inunue umeme asilimia 90 au 100 ndo iuze? ina uwezo huo?
itasaidia kweli?
Ni mipango ya serikali yote au Muhongo binafsi?