Anayempinga Kikwete si mzalendo

Pamoja na hizo ngebe mbona hali yetu kiuchumi ni mbaya kulikoni miaka mitano iliyopita?

 
Mazeee hivi wewe ni kibaraka nin? ........ Ongeza hoja kwanza hueleweki kabsaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa............. go through the forest dont go arond the forest.... leta hoja za msingi..... JK needs to assess himself then come up with new strategic performance plans for da next 5yrs na atupatie right nau tu evaluate.... ukimwabia haya ata dondoka tena.
 
Ndugu watanzania wazalendo na wapenda maendeleo ya nchi yetu, h.... akuna nchi africa ambayo rais wa marekani amekaa kwa muda mrefu katika ziara zake kama tanzania.

Kwa hiyo??? Imewasaidia nini wananchi wanaoshindia mlo mmoja kwa siku ??
Kujikomba kwa viongozi wa mataifa makubwa ndio kazi aliyotumwa na watanzania? Ndio maana anaona sifa kwenda kuombaomba na kusifia jinsi alivyoahidiwa misaada.
 

Kwenye red hapo umesema ukweli mtupu, hakuna mtanzania anayeweza kufuta maumivu na makli ya maisha tuyapatayo sasa, vifo kwa magonjwa yanayoweza zuilika vimeongezeka kipindi hiki cha "mpendwa" wetu JK kuliko wakati mwingine wowote, mzaha serikalini umeongezeka na pengo kati ya tajiri na maskini limetanuka kwa nguvu zaidi, ni kweli hakuna atayeweza futa kumbukumbu hizi!
 
Waambie bwana
 

Maendeleo ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja, hata huyo WPS akichaguliwa hali itakuwa hivi hivi, cha msingi watanzania tuache uvivu na kutaka utajiri wa haraka bila kufanya kazi!!! Watanzania ni wavivu, mnataka kikwete auze dhahabu amgawie kila mtu pesa!! Hapo ndo mtamwona mzalendo, mbona wakenya waweze through hard work.
Kazi ya kiongozi ni kutoa dira na wananchi kumfuata kwa kuchapa kazi, hapo tutatoka katika umaskini!!!! China, Japan, Korea, Indonesia ........... ni mfano wa kuigwa!!!!
 
Sikatai kama maendeleo ya nchi huletwa na uchapa kazi, lakini kumbuka kuwa hata ukichapa kazi vipi kama wizi na matumizi mabaya ya mapato ya serikali vitakuwa ndio msingi mkuu wa uendeshaji wa serikali yoyote ( kama ilivyokuwa serikali ya JK iliyopita) hakuna maendeleo hapo. Na nikuambie tu waTZ tumechoka kutajirisha familia ya Kikwete na Syndicate yake kwa gharama ya jasho na damu zetu! kama tusipotaka kikwete atugawie mapato ya dhahabu ambayo ni urithi wetu sote, we watakaje, we unaona ni sawa hivi wafanyavyo sasa wanauza dhahabu yetu kwa beii ya chee na kujenga mahotel ya kifahali south africa, kufungua accounts dubai, kununua majumba ya kifahari South of France na kwenye fukwe za belgium wewe ndio unaona uzalendo huo? Ni kweli kazi ya kiongozi ni kutoa dira, lakini for the past five years tanzania hatujawa na kiongozi wa aina hiyo, kiongozi tuliyekuwa nae ni yule anayefuata maagizo ya mabwana zake waliomuingiza ikulu kwa faida yao, ni kiongozi aliyeendekeza starehe za kusafiri bila kujali njaa iliyokuwa inatuua hapa nyumbani. Umetaja nchi za China, Japan, korea na nyingine, nikupe siri ya mafanikio yao, kama hujui ni uadilifu wa viongozi wao, kitu ambacho hadi yesu arudi huwezi kukipata ndani ya CCM!
 
Eti mafanikio ya rais kajenga Machinga complex tena jengo moja!!!!!. Hii nchi itabakia kuwa masikini hadi mwisho wa dunia wakati tuna kila kitu.
 
Hakuna umasikini Mbaya kama wa kufilisika kimawazo,kama huyu jamaa alivyo choka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…