Anayempinga Kikwete si mzalendo

Pamoja na hizo ngebe mbona hali yetu kiuchumi ni mbaya kulikoni miaka mitano iliyopita?

Alitoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya wananchi kujikwamua kiuchumi na wote tu mashahidi wa hili. Shule za kata kila kona, chuo kikuu cha dodoma, machinga complex,Kigamboni new City, amewashughulikia mafisadi wa EPA, mpinga ufisadi, mchukia rushwa, mtu wa watu.
Tatizo lililojitokeza ni baadhi ya wasaidizi wake wamekuwa sio wazuri na hilo litashughulikiwa ipaswavyo miaka mitano ijayo.
 
Mazeee hivi wewe ni kibaraka nin? ........ Ongeza hoja kwanza hueleweki kabsaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa............. go through the forest dont go arond the forest.... leta hoja za msingi..... JK needs to assess himself then come up with new strategic performance plans for da next 5yrs na atupatie right nau tu evaluate.... ukimwabia haya ata dondoka tena.
 
Ndugu watanzania wazalendo na wapenda maendeleo ya nchi yetu, h.... akuna nchi africa ambayo rais wa marekani amekaa kwa muda mrefu katika ziara zake kama tanzania.

Kwa hiyo??? Imewasaidia nini wananchi wanaoshindia mlo mmoja kwa siku ??
Kujikomba kwa viongozi wa mataifa makubwa ndio kazi aliyotumwa na watanzania? Ndio maana anaona sifa kwenda kuombaomba na kusifia jinsi alivyoahidiwa misaada.
 
Ndugu watanzania wazalendo na wapenda maendeleo ya nchi yetu, wote tunatambua kazi nzuri aliyo ifanya Rais wetu kipenzi JK ndani ya miaka mitano yake ya uongozi. Ni ukweli usiopingika hasa kwa watu wote wenye akili timamu za watu wenye uwezo wa kupambanua mambo kuwa JK ameacha alama nyingi za kudumu hapa nchini na hamna mtu atakayeweza kuzifuta.
Heshima ya nchi yetu imezidi kujionesha kitaifa na kimataifa, Hakuna nchi africa ambayo rais wa marekani amekaa kwa muda mrefu katika ziara zake kama tanzania. Rais Bush na Obama ni mashahidi wa hili.
Alitoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya wananchi kujikwamua kiuchumi na wote tu mashahidi wa hili. Shule za kata kila kona, chuo kikuu cha dodoma, machinga complex,Kigamboni new City, amewashughulikia mafisadi wa EPA, mpinga ufisadi, mchukia rushwa, mtu wa watu.
Tatizo lililojitokeza ni baadhi ya wasaidizi wake wamekuwa sio wazuri na hilo litashughulikiwa ipaswavyo miaka mitano ijayo.
Viva kikwete, nenda mwanakwetu wanao tuko nyuma yako.
May your star keep on shinning................. Bravo, bravo, bravo, .... Aluta continua..............
Happy Birthay baba yetu, Tanzanians loves you and we are all behind you dont give up!!
May God bless you and God bless Tanzania!!

Kwenye red hapo umesema ukweli mtupu, hakuna mtanzania anayeweza kufuta maumivu na makli ya maisha tuyapatayo sasa, vifo kwa magonjwa yanayoweza zuilika vimeongezeka kipindi hiki cha "mpendwa" wetu JK kuliko wakati mwingine wowote, mzaha serikalini umeongezeka na pengo kati ya tajiri na maskini limetanuka kwa nguvu zaidi, ni kweli hakuna atayeweza futa kumbukumbu hizi!
 
Katika mambo ambayo huwa siku zote yananishangaza, ni kuona hata mashabiki wa kikwete wana hoja za kitoto kama Kikwete mwenyewe. Hivi mtu mzima unakaa chini na kuanza kujisifia kwa kumlete Bush nchini na kupewa msaada wa vyandarua? Ulimbukeni gani huu? Hivi ina maana CCM na kikwete wenu uwezo wenu wa kufikiria ndo unaishia hapo tu, kufikiria zaidi misaada kuliko namna nzuri ya kuzitumia resources zilizopo ndani ya nchi ili kuwaongezea wananchi kipato na kuboresha maisha yao?
Waambie bwana
 
Kwenye red hapo umesema ukweli mtupu, hakuna mtanzania anayeweza kufuta maumivu na makli ya maisha tuyapatayo sasa, vifo kwa magonjwa yanayoweza zuilika vimeongezeka kipindi hiki cha "mpendwa" wetu JK kuliko wakati mwingine wowote, mzaha serikalini umeongezeka na pengo kati ya tajiri na maskini limetanuka kwa nguvu zaidi, ni kweli hakuna atayeweza futa kumbukumbu hizi!

Maendeleo ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja, hata huyo WPS akichaguliwa hali itakuwa hivi hivi, cha msingi watanzania tuache uvivu na kutaka utajiri wa haraka bila kufanya kazi!!! Watanzania ni wavivu, mnataka kikwete auze dhahabu amgawie kila mtu pesa!! Hapo ndo mtamwona mzalendo, mbona wakenya waweze through hard work.
Kazi ya kiongozi ni kutoa dira na wananchi kumfuata kwa kuchapa kazi, hapo tutatoka katika umaskini!!!! China, Japan, Korea, Indonesia ........... ni mfano wa kuigwa!!!!
 
Sikatai kama maendeleo ya nchi huletwa na uchapa kazi, lakini kumbuka kuwa hata ukichapa kazi vipi kama wizi na matumizi mabaya ya mapato ya serikali vitakuwa ndio msingi mkuu wa uendeshaji wa serikali yoyote ( kama ilivyokuwa serikali ya JK iliyopita) hakuna maendeleo hapo. Na nikuambie tu waTZ tumechoka kutajirisha familia ya Kikwete na Syndicate yake kwa gharama ya jasho na damu zetu! kama tusipotaka kikwete atugawie mapato ya dhahabu ambayo ni urithi wetu sote, we watakaje, we unaona ni sawa hivi wafanyavyo sasa wanauza dhahabu yetu kwa beii ya chee na kujenga mahotel ya kifahali south africa, kufungua accounts dubai, kununua majumba ya kifahari South of France na kwenye fukwe za belgium wewe ndio unaona uzalendo huo? Ni kweli kazi ya kiongozi ni kutoa dira, lakini for the past five years tanzania hatujawa na kiongozi wa aina hiyo, kiongozi tuliyekuwa nae ni yule anayefuata maagizo ya mabwana zake waliomuingiza ikulu kwa faida yao, ni kiongozi aliyeendekeza starehe za kusafiri bila kujali njaa iliyokuwa inatuua hapa nyumbani. Umetaja nchi za China, Japan, korea na nyingine, nikupe siri ya mafanikio yao, kama hujui ni uadilifu wa viongozi wao, kitu ambacho hadi yesu arudi huwezi kukipata ndani ya CCM!
 
Eti mafanikio ya rais kajenga Machinga complex tena jengo moja!!!!!. Hii nchi itabakia kuwa masikini hadi mwisho wa dunia wakati tuna kila kitu.
 
Anna_Lupembe.JPG
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom