Anayekutawala amekuzidi Akili

Mtu kama hana akili hawezi kukutawala.
Akili anakuwa nayo ndio ila si lazima awe anakuzidi akili japo anaweza pia akawa anakuzidi akili. Kikubwa hapa ni nguvu; kwamba mnyonge hawezi kumtawla mwenye nguvu isipokuwa mwenye nguvu ndiye aliye na uwezo wa kumtawala mnyonge
 
Pengine una maanisha "ujasiri" = Being brave enough to...., na sio "Akili" = inteligence/cleverness.

Kwa baadhi ya mambo neno FATE = Majaliwa, linaweza kufit zaidi maelezo yaliyotolewa (mf. Historia ya Chifu Mkwawa).

Neno akili lina ukomo kwa vile baadhi ya mifano iliyotolewa haifui dafu kwa kundi kubwa la viumbe waliojipanga kutawala/kushinda kundi dogo hata kama lina akili kiasi gani.
Mfano, kundi la simba porini likimuua tembo limesaidiwa na:
-wepesi wa mwili
-Aina ya meno na makucha waliyoumbiwa (tearing)
-Msukumo (urge) wa njaa na mahitaji ya chakula chake (Carnival)

Tembo akiuawa ni kwa sababu:
-Ukubwa wa mwili, sio rahisi kujificha au kubadili uelekeo
-Naturally yeye ni chakula cha wanyama walao nyama,
-n.k.
Je unataka kusema Sadam Hussein au Osama walizidiwa akili na Taifa la Marekani?
Anyway, nakubaliana na mtoa mada kwamba, akili ina mchango mkubwa kutawala jambo lolote tena bila kutumia nguvu. Bali tusisahau nguvu iliyomo kupitia ulaghai, timing na mifumo.
 

Hata binadamu ni chakula kwa wanyama kama Chafu, chui, mamba, Simba n.k.
Kutokuliwa kwa wanyama kunatokana na uwezo wake wa kujilinda, Akili.

Simba atamuua tembo kutokana na Akili. Uwezo wa akili za simba ambao unawafanya kushirikiana ndio kunakowafanya wamshinfe tembo. Wanajua bila kushirikiana hawana uwezo wa kumshinda tembo. Hiyo ni Akili.
Simba meno yake hayana nguvu kubwa (bite strength) ukilinganisha Mamba, Tiger na Fisi.
Pia simba hana nguvu wala uzito kumshinda Tembo, kifaru na nyati. Ila akili na ujasiri amewazidi hao wote.

Ndio maana simba anaitwa mfalme wa nyika.

Sadaka Hussein na Osama Bin Laden walizidiwa karibu kila kitu na Marekani sio tuu Akili bali hata Nguvu, ushawishi, pesa n.k.
 
Akili anakuwa nayo ndio ila si lazima awe anakuzidi akili japo anaweza pia akawa anakuzidi akili. Kikubwa hapa ni nguvu; kwamba mnyonge hawezi kumtawla mwenye nguvu isipokuwa mwenye nguvu ndiye aliye na uwezo wa kumtawala mnyonge

Nguvu za nini?
Kama ni nguvu za mwili basi umekwama.
Wenye miili mikubwa wengi wanatawaliwa na wenye miili midogo midogo. Na wengi ni vibarua. Wanatumikishwa.

Akili ndio inayoongozwa hata huo mwili wako.
 
Aisee niliwaambia wanafunzi wangu kuwa wasimcheke mwanafunzi mfupi na mwembamba ila watazame kichwani kujua kabeba Nini ili wasimcheke boss wao wa kesho
 
[QUOTE="Robert Heriel Mtibeli, post: 48243606,

Kushindwa kujinasua individually kwenye situation fulani kwa kukosa nyenzo au sapoti ya society, hakumaanishi wewe hauna akili.

Yafaa nini uki-demonstrate akili zako ukaishia kupotea mazima? Ushahidi wa hizo akili utatoka wapi?
 
Ndugu kumbuka utawala ni mfumo, mtawala ni mtu aliye ndani ya mfumo.
 
Kuna utawala wa mabavu na utawala wa akili au vyote kwa pamoja.

Hata hivyo, kipimo kizuri zaidi cha akili ni uwezo wa ku- survive.

Kipimo hiki kinajifunua kupitia umahiri wa kubadilika kwenda na nyakati na mazingira, na wala sio mabavu au akili kama inavyopimwa darasani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…