Anayekutawala amekuzidi Akili

Kwenye comment yangu ya mwanzo nimekuonesha namna jamii mbalimbali zote duniani zilitumia mabavu kutawaliana.

Kitu ambacho kinapingana na dhana yako kuwa jamii fulani ina akili nyingi kwa sababu ya kuitawala jamii nyengine kitu ambacho sicho.

Kwa faida zaidi nikuongezee kuwa wachina ndio jamii ya mwanzo kufika Afrika mashariki kabla hata wazungu hawana mpango huo lakini hawakuitawala east Africa zaidi ya kufanya biashara na kuondoka ila wazungu walitumia mabavu kutawala east Africa.
 

Huwezi tumia mabavu kwa Watu wenye Akili utapigwa.
Mabavu hutumika kwa Watu uliowazidi Akili na nguvu.

Hizo jamii zote zilizotumia mabavu zilikuwa na Akili.
Kumbuka jeshini kuna vifaa ambavyo ili uvitengeneze lazima uwe na Akili.
Sasa niambie ni utawala gani uliotawala pasipo kuwa na silaha.
Na ili uwe na silaha lazima akili ihusike.

Hao wachina unaowataja wanaweza kuwa na akili kwako au kwa jamii za chini yao lakini kidunia bado hawapo namba Moja mpaka tatu.

Utawala unahusisha Akili
 
Kwhyo brother ndio umeamua kutukandia kbs eeh! Bnafs ninaamini ulichoandka ingawa kuna mengne hapo nahtaj niyang'amue kwanza.
 
Kwanza unapaswa ufahamu kila nchi,taifa, jamii ina taratibu zake za kiulinzi wengine sera zao za kiulinzi ni kijilinda tu sio kushambulia au kupora.

Turudi kwa wachina hiyo ya kusema hawana uwezo mkubwa wa akili ni kwa mujibu wako binafsi au kwa mujibu wa taifiti gani ?

Mimi nacho fahamu tafiti za kimataifa zimewataja watu wa Asia mashariki kama watu wenye akili nyingi kushinda jamii zote na hao ni wachina, wajapan na wakorea.

Unafahamu Chinese Civilization ? imeanza lini na ina miaka mingapi mpaka sasa ?
 

Hata wewe unawezakuwa na akili kwa level ya familia yenu. Halikadhalika na Mimi.
Huyo China anaweza kuwa na akili kwa level ya jamii zao(Wachina, Wajapan, Wakorea) na ukanda wa Mashariki ya mbali . Lakini tukizungumzia Ulimwenguni hapo tunazungumzia habari nyingine kabisa.

Ni sawa useme Chadema inanguvu kisa umeenda Moshi au Arusha. Kitaifa Watu watakushangaa.

Hao Wachina hawana Rekodi yoyote ya maana katika mambo ya Akili na utawala ulimwenguni.
Labda kama unazungumzia habari za Future ambazo kwa sasa hazina maana yoyote.
 
Hata ule uwezo wa kutawala na kudhibiti hisia zako binafsi, unategemea kwa kiasi kikubwa, uwezo wako wa kusimamia , na kuelewa akili yako.

Watu wenye uwezo Bora, wa kudhibiti na kusimamia ( kutawala) hisia zao , mara nyingi wana uwezo wakufanya maamuzi bora, na kushughulikia changamoto katika njia bora zaidi.

Mtoa mada upo sahihi sana.
 
Hilo la wanawake kutokutawala na kutokuwa na akili, nakupinga 100%

Mwanamme kwa ujinga wako hata nyumbani unajiona unatawala wewe, hujielewi kuwa kuna Malkia anaekutawala.

Watawala wa kiasili, iwe kwa Binadam, wanyama na hata wadudu ni wanawake.

Sijawahi kusikia kuna mtawala "mfalme" kwenye himaya zote nje ya binadam.

Binadam, mwanamme anajidai tu kuwa anatawala, kwa ujinga wake, lakinimtawala haswa ni mwanamke.

Kama unabisha soma biblia kisa cha Tamari alivyomzidi akili hata baba mkwe wake.

Soma Malkia wa Sheba alivyotawala.

Soma kuhusu kina Nfertiti, malikia wa Kufarao.

Soma chuo kikuu cha kwanza duniani kimeanzishwa na nani, utakuta ni Mwanamke.


Soma historia ya Somalia, walipokuwa na Malikia Fatma (Faduma) hawajawahi kutawaliwa, mpaka walipokuja kurithi wanaume, Somalia imekuwa janga.


Tazama Uingereza, si unaona miaka aliyotawala Malkia nchi ilivyotawala ulimwengu? Sasa tazama akiingia mwanamme itavyokuwa. Itakosa hata heshima inayopewa duniani.


Hakuna Mwanamme anayeweza kumzidi akili Mwanamke hata siku moja.++Basi hujasoma hata Alfu lela ulela?
 

Ndio.
Kujidhibiti na kudhibiti wengine na mazingira ndio akili yenyewe
 

Nikujibu kwa upande wa Historia, dini au kisayansi?
 
Kwhyo brother ndio umeamua kutukandia kbs eeh! Bnafs ninaamini ulichoandka ingawa kuna mengne hapo nahtaj niyang'amue kwanza.

Hiyo inanihusu hata mimi Mkuu.
Huo ndio ukweli.
Mimi nikiona umenizidi kipato na tunarika sawa moja kwa moja na- appreciate kuwa umenizidi Akili Kwa eneo hilo. Kuhusu kufanya changes kukufikia au kukupita hiyo ni ishu nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…