Anayeishi na simba achaniwa suruali sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayeishi na simba achaniwa suruali sita

Discussion in 'Celebrities Forum' started by kilimasera, Jan 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MTAALAMU wa tabia za wanyama aliyeamua kuishi na simba wawili kwa kipindi cha mwezi mmoja, ametimiza siku ya tano na tatizo lake kubwa ni kuchaniwa nguo. Jim Jablon anayeishi na simba ndani ya banda moja kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia chakula na matunzo kwa wanyama waliojeruhiwa porini, ameanza kuonja shubiri ya simba hao ambao katika siku tano tayari wamemchania suruali sita aina ya jinzi. Mtaalamu huyo anaishi na simba hao aliowapa majina ya Lea na Ed, kwa kipindi chote cha mwezi huu wa Januari, ambapo hata hivyo ndani ya banda hilo kuna sehemu za usalama kama simba hao watakuwa wakali kwake.
  Jablon (42) ambaye anajiita ‘mfalme wa porini’ alisema meno ya simba hao yamekuwa yakirarua suruali ambapo hadi sasa amelazimika kutupa suruali sita, kwakuwa hazivaliki tena. Alisema simba hao huwa wanakula mlo mmoja kwa siku, hali ambayo imemfanya na yeye awe anakula mlo mmoja kwa siku. Jablon anasaidiwa na binti yake Chelsey mwenye umri wa miaka 13 ambaye kazi yake ni kupeleka chakula na mahitaji mengine.
  Jablon alisema chakula chake huwa anakula kwa kujificha ndani ya moja la banda lake la usalama aliloliweka juu ya mti.
  Alisema yeye huwa anakula chakula kilichopikwa kwa kupelekwa na kuwekwa sehemu maalumu, ambapo simba hao hupewa nyama.
  Jablon alisema wakati wa usiku huwa analala ndani ya banda lake la usalama alilojenga juu ya mti, urefu wa futi 12 kutoka ardhini, na kwamba eneo hilo simba hao hawezi kulifikia.
  Alisema kwa ujumla simba hao huwa wanalaa kwa kati ya saa 18 hadi 20 kwa siku, ambapo na yeye hutumia muda huo kupumzika.
  Jablon alisema pia ana eneo lingine dogo lenye uzio ambalo nalo ni kwa ajili ya usalama wake, kama simba hao watageuka mbogo kwake.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  the dude is nomaaaaaaaaaaa

  http://www2.hernandotoday.com/exposure/ar/659/372/2011/01/04/89964_wildlife8.jpg
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hao watakuwa simba koko wala sio wale wa serengeti ninaowafahamu!
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,052
  Trophy Points: 280
  Duniani kuna mambo na vibweka bwerere
   
 5. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  I agree with you 200% wale wa Sere sio suruali tu wangechana dakika 5 tu na dalili kwamba kulikuwa na mtu huko ndani ingekuwa ngumu kutambua
   
 6. M

  Msharika JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
 7. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  huyu simba lazima shoga
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hakuna wanyama wenye AIBU kama simba. Simba hawezi kukuangalia usoni kwa zaidi ya nusu dakika. Ukimtazama sana huwa anakwepesha macho na kuangalia mbali.
  Simba ni mvivu sana. Baada ya kula na kushiba hana kazi nyingine zaidi ya kulala. Ikitokea uka-volunteer kumletea mlo kila siku na akashiba, basi huwa anazoea na hujenga mazea ya kuletewa chakula. Serengeti kuna project ya simba. Mojawapo ya majukumu ya simba ni kuangalia maisha ya simba hawa. Simba anapopata ajali watafiti humwonea huruma hivyo kumtafutia chakula. Ikichukua muda kwa mnyama huyu kupona hubadilika tabia na kuwa kama ombaomba. Huwa hawindi tena ila huishi kwa kutegemea leftover kwa wanyama wengine. Simba akizoea unaweza kucheza naye utakavyo ili mradi usimuumize au kumpiga kwa nguvu.
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  .

  Mwanga huyooooooooooooooooooooooooooo
   
Loading...