Anayeichafua TAHLISO huyu hapa

Anayeichafua TAHLISO huyu hapa

Uko chuo kikuu kweli wewe? Jamani naomba kuuliza, hivi zile sekondari za kata tangu zianze kutoa matunda form four, washafika chuo kikuu hao walomaliza?
 
Unawezakuta aliyemsahishia mtiahani wa necta naye hawezi tofautisha r na l, hivyo hata kwenye mtihani kama aliandika "leport"/"repolt" badala ya report na msahishaji hakuona tatizo.
 
Anaitwa Donath Sara na arikuwa makamu wa lais STEMMUCO.Ni katibu mkuu wa TAHLISO na ariingia kwenye mgogolo binafsi na mwenyekiti Amon Chakushemeile kwa kuwa arikuwa hamkubari na hata kwenye uchaguzi Zanzibar Donath arikuwa na kundi rake.

Mgogolo mkubwa ni masrahi kwani Amon ni kundi la Mwakyembe na Donath ni kundi la Lowassa.Tangu wamechaguliwa Donath amekuwa akifanya kasi kinafiki na Amon.

Uchu wa madaraka ndiyo iliyozaa mgogoro wote hadi kufikia Donath kumchafua Amon kwenye mitandao na kumuita raia wa Rwanda.

TAHLISO watapewa nafasi moja kwenye bunge la katiba sasa Donath anaitaka lakini kikatiba ni nafasi ya mwenyekiti hivyo ameona ampige zengwe la uraia ili nafasi hiyo apewe yeye kama katibu mkuu.

Kwa unafiki baada ya kumpiga zengwe hilo huyo huyo dogo akaja humu JF na kufungua akaunti mpya ili kumsafisha Amon.

Pia kuna safari ya kwenda China mwezi huu nalo limezidisha mgogolo baina yao.

Babajoni. Pole sana. Hoja unazo lakini kiswahili chako Mkongo wa DRC anakupita kwa mbali sana. Najua kuwa kuanza leo kutofautisha kura na kula au lead read {hapo najua huelewi tofauti} ni kazi ngumu kwako, lakini huna budi kuanza leo kwani kipaji cha kujenga hoja, bila kuwa na lugha sahihi ni sawa na UBUBU kwenye watu wasiojua alama za UBUBU. Anza leo, baada ya miaka mitatu minne utaweza kujua wapi utumie r, l, h, i, nk.
 
dah jamaa kaingia cha kike! hakuna hata mchangiaji mmoja wa hoja yake! jamani tumsaidie afikshe hoja yake
 
Wengine hata hatuelewi TAHLISO ni nini,i.e mnyama,mdudu,political party,dhehebu,kitabu,chakula,mtu,timu,taasisi,etc. hebu fafanueni vzr ili tujue pa kuanzia kuchangia!

kiwanda cha kusindika nyama ya nyati.
 
Ukimsoma kwa haraka mleta mada utahisi hajui lugha vizuri ila ukilinganisha mistari mitatu ya awali na inayofuata utagundua mwandishi kuna kitu alitaka kukificha kwa kutumia aina hiyo ya uandishi,km hivi ndivyo basi mwandishi ametumia akili ndogo sana.............
 
Ni jambo la busara kwamba kama kuna ushahidi wowote kuhusiana na jambo hili basi ni vyema ukawekwa hadharani hapa kwenye jf kwa sababu siyo vizuri kuipuuza hoja ya mtu pasipokuwa na sababu yoyote na pia siyo vizuri kumchafua bila ya sababu.
 
Bilashaka huyu jamaa kama si mkongomani basi Mnyarwanda. Huyu sio kwamba hajui kuadndika bali hafahamu kiswahili vizuri kwani ni 1wapo ya wale hamiaji haramu!
 
hiyo sijui TAHLISO ndio kituo cha kwenda wapi?
 
Back
Top Bottom