Anayefahamu ubora wa vifaa vya Sundar

Mkuu Sundar wana bidhaa kawaida kama watu wengine walivyotangulia kusema hapo.
Solar panel, battery na vitu vingine vinavyohusu mfumo wa umeme wa jua vipo vyenye ubora mzuri na vinavyodumu na vinapatikana kwa wakati(inategemea mfuko wako tu)
Kuna kampuni zinatengeneza battery kama Rittar, Deka, Chloride Exide, Surette, BAE n.k.
Kuna kampuni zinatengeneza Solar panel km Oceanic, Ying Li n.k
Kuna inveta za kampuni kama Magnum, Victron, Xantrex n.k
Kuna kampuni zinauza bulb km Phocos, Bramax n.k.
Ni mfuko ndio unaamua unataka mfumo wa umeme wa solar utakaodumu mda gani.
Asante
 

Nimesoma coment yako, ww ndio unajua solar vizuri. watu wabongelea rubish kabisa







Proffesional tunatumia hivi vitu
 
Kiasi gani hii?
 
Mzee hapa imekutoka kama kiasi gani, na je huu mzigo unasukuma nyumba nzima, kuangalia tv, huku unapiga pasi, friji limewashwa.. unapandisha maji kwenye tanki, taa ziko on, feni hapo hapo etc.
 
Nina Battery la pro solar linapiga kazi balaa N100 natumia panel za sundar, ukinunua battery la pro solar hutojutia. Sema panel zao ndio ziko ghali sana.
 
Wakuu ninaswali nina battery N100 je' ninaweza kutumia Friji?

Kaka kuuliza swali la kiufundi bila kutoa details maana yake unataka tuague au tupige ramli ndio tukupe jibu.

Ilo fridge lako sisi tunalijua?
Unataka lifanye kazi masaa mangapi sisi tutajuaje?

Kindly provide supportive information
 
Hao Zola na mobisol wanabidhaa ghali lakini sijui kama wanauza rejareja nadhani wanakufungia mfumo wao na unalipa kwa mwezi,mimi ningependelea kampuni zinazouza bidhaa iliyo bora na nafuu.
Suluisho ni AG energies tuu hao wengine wote changa la macho
 
Mwenye uhitaji wa BETRI ZILIZOTUMIKA KWENYE MINARA ninazo.
Usafiri kwa kahama, Singida,Dodoma, morogoro, Mwanza, geita bure mpaka inakufikia no utapeli ushahidi upo kwa wateja wote waliozipata.

BETRI ni 160N/ah
BEI 330,000.

0629945110.
Bukoba.
 
Kaka kuuliza swali la kiufundi bila kutoa details maana yake unataka tuague au tupige ramli ndio tukupe jibu.

Ilo fridge lako sisi tunalijua?
Unataka lifanye kazi masaa mangapi sisi tutajuaje?

Kindly provide supportive information
Mkuu sina friji ila nikipata uhakika kama nitaweza kutumia friji kwenye battery N100 ndio ninunue friji kama hiyo hapo. Kuhusu Solar zangu nina panel 2 za watt 80 kila moja jumla ni 160. Nisaidie.
 
Nilinunua Solar Panel ya Sundar, Nimepewa Warranty Miaka 25, Hivi hapa Nasubiri nione kama itafika Mwaka 2044 😕
 
Natumia tv hata pasi ya kunyoosha nguo.
Panel watt 100
Battery 75
Nashukuru kwa ushauri wenu kwa sasa ninaburudika,nilinunua betri ya sola aina ya RITAR 80 Ah ya Vietnam na Panel ya BP SOLAR(niliuziwa na rafiki yangu,iliyotumika miaka10)140watt. TV ya chogo masaa 4,taa 4 @ 1watt,kuchaji Smartphone 3 bado moto haujaisha.Sasa nina mpango wa kununua Flat Screen Tv kupunguza mzigo hasa siku ambayo jua halikuwaka vizuri asante kwa cyber ghost
 
Nina Battery la pro solar linapiga kazi balaa N100 natumia panel za sundar, ukinunua battery la pro solar hutojutia. Sema panel zao ndio ziko ghali sana.
Mkuu Mondela salam kwako. Naomba kujua hizo Pro solar ni Dry au wet Batteries? Mkuu samahani, Je matumizi yako yanajumuisha nini mfano Tv, Taa ngapi nk.

Ahsante
 
Nicheck nikupe betri na solar panel zake znazotumika kwenye minara achana na mavitu ya kichina hayo masundar sjui Zola sjui mobisol hamna kitu utauziwa Kwa mikopo kitu kidogo mil 2 na ufanisi wake ni kawaida Sana.
Njoo PM
Betr mkuu zipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…