Anayefahamu taratibu za kusajili NGO

Anayefahamu taratibu za kusajili NGO

kusajor mkuu nenda ofisi ya makamu wa raisi kwa upande wa ngo, lakini kama ni cbo wilayani ofifi ya maendeleo ya jamii anamaliza kama unahitaji kuandikiwa katiba tupo wataalamu na inachukua si zaidi ya siku moja au mbili kupata gamba lako ila tu uwe na katiba ambayo ipo freshi.
 
una uhakika? Hakuna ngo hata moja inayosajiriwa kwa mkuu wa wilaya au kwa mkuu wa mkoa. Hata kama ina operate kwenye wilaya moja.

Muwe mnaandika vitu ambavyo una uhakika navyo na si kukurupuka tu. Kwa kifupi mwanzoni ngo zote zilikuwa zinasajiriwa wizara ya mambo ya ndani lakini hivi baadae wameamua wapeleke swala hilo wizara ya maendeleo ya jamii. Na wizara ya mambo ya ndani inasajiri zile za kimataifa tu kutokana na mambo ya kiusalama.

Nina uhakika ndiyo!

Wewe ndo umekurupuka!

Hebu muwe mnaelewa na nyie. Nenda hata sasa hivi kwa Mkuu wa Wilaya ukaulizie kama hutapewa fomu za kujaza kwa NGO itakayofanya kazi kwenye wilaya moja naona unaumwa wewe! Mimi niliyesema hayo nimeshafanya nikaambiwa hivyo, lakini baada ya kuona NGO yetu itakuwa ya Kitaifa nikaelekezwa wizara mambo ya ndani ofisi ya msajili wa vyama (na hicho unachosema wizara ya maendeleo ya jamii siyo kweli labda hiyo ni CBO wala siyo NGO). Hii kazi nimeifanya mwaka 2008 mpaka sasa hivi NGO yetu ilishasajiliwa.

Hiyo sheria unayozungumza ya kusajili maendeleo ya jamii sijui ya mwaka?
 
MKUU KWA KIFUPI NI KWAMBA HAKUNA HATA SIKU MOJA AMBAPIO MKUU WA WILAYA ANASAJIRI NGO. WATU WANASHINDWA KUTOFAUTISHA VITU HIVI,
1. KUSAJIRI
2. KUJITAMBULISHA. ili uanze shughuli.
KWA MKUU WA WILAYA UNAENDA KUJITAMBULISHA NA UNASAJIRIWA KWENYE DAFUTARI LAKE KAMA MMOJA WA WATU WANO FANYA KAZI KWENYE ENO LAKE LA UTAWALA.
mkuu wa wilaya hasajiri NGO hata siku moja

Usiwe unajidai kuandika hapa kabla ya kwenda kuulizia.

Ukishaonesha kwa Mkuu wa wilaya kwamba utafanya kazi kwenye wilaya moja anakupa fomu za kujaza (tena hii kazi inafanywa na Katibu Tawala wa wilaya, yaani DAS). Hicho unachosema kujitambulisha ni pale unapoingia na NGO yako kwenye eneo lake. Lakini kama utakauwa unataka kusajili NGO ambayo itafanyakazi Kitaifa yeye kazi yake hapo ni kukuandikia barua ya kukutambulisha kwa msajili wa vyama ambaye yuko hapo wizara ya mambo ya ndani au unataka mpaka tukupe na ramani ya ofisi yake ilipo?

Sasa nakushangaa umekazana tu kuropoka mkuu wa wilaya hasajili NGO bila kufanya uchunguzi bwana! Hebu nenda ukaulize hapo wilayani kwenu taratibu zilivyo halafu uje utujuze hapa jamvini. Maana tunaosema haya tulishayafanya. Huo ndo uhakika!! Tena wala siyo zamani sana ni mwaka 2008 tu!
 
asante sana, J3 natinga ofisini kwa DC,tayari kuandaa mpango wa kujisajili
 
Habari ya wana JF naamini ya kuwa humu ni jawabu la kila kitu ndugu zangu, naombeni msaada juu ya taratibu zote za kusajili N'Go na wapi wanakosajili....msaaada jaman!!!!!!!Aksante.
 
Habari ya wana JF naamini ya kuwa humu ni jawabu la kila kitu ndugu zangu,naombeni msaada juu ya taratibu zote za kusajili N'Go na wapi wanakosajili....msaaada jaman!!!!!!!Aksante.

1. Kuwe na wanachama waanzilishi au wajumbe wa Bodi.

2. Kuwe na ofisi ya hiyo NGO kule inakofanyiakazi/inakotarajiwa kufanyiakazi (hapa wanaogopa kusajili NGO ya mfukoni/Briefcase - ingawa kwa mission town jamaa huwa wanasajili).

3. Kuwe na Katiba ya hiyo NGO (ambayo sharti iwe imepitishwa na wanachama waanzilishi wote au hao wajumbe wa Bodi). Baada ya kuwa imeandikwa hiyo Katiba Mkuu wa Wilaya/DAS atapenda kuiona (hii ni aina fulani ya ukiritimba). Baada ya hapo mtaandika barua kwa msajili wa vyama (huyu huwa yuko Wizara ya Mambo ya Ndani) ya kuomba kusajiliwa ambayo itapitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata, Mkuu wa Wilaya (ambako ofisi zenu zipo). Pia Mkuu wa Wilaya atawaandikia barua ya utambulisho kwa msajili wa vyama akitambulisha uwepo wenu katika Wilaya yake.

4. Baada ya kumaliza huo mlolongo wa Wilayani utatakiwa kwenda Dar-Es-Salaam kwenda kusajili hiyo NGO, utaenda na nakala 3 za Katiba yenu iliyopitishwa na wanachama waanzilishi au wajumbe wa Bodi ya hiyo NGO na sahihi zao.

5. Utatakiwa kuwa na fedha/Ada ya usajili Tsh. 100,000/=

6. Fedha ya ada ya Mwaka mmoja (1) Tsh. 40,000/= (Local NGO) pia utatakiwa kuwa na Tsh. 10,000/= kwa ajili ya fomu ya usajili.

Fedha yote hii utailipa mara baada ya kitengo cha sheria kuwa kimejiridhisha na Katiba yenu kwamba imekaa vizuri na hivyo watakuelekeza mahali pa kwenda kulipia hiyo fedha na kupewa stakabadhi za Serikali (ERV)

Kama Katiba yenu itakuwa imekaa vizuri baada ya kitengo cha sheria pale kwa msajili kuipitia na kuridhika nayo utakuwa umefanikisha usajili ambao mpaka kufikia kupata cheti chenu cha usajili inaweza kuchukua mpaka siku 15 za kazi. Pengine unaweza kuwa na bahati ukamkuta Msajili mwenyewe yuko ofisini na watu wa kitengo cha sheria ukawakuta na morale ya kazi unaweza kukamilisha zoezi hili ndani ya siku 2. Hata ya kwangu nilikuwa nifanikishe ndani ya siku 2 lakini haikuwa hivyo maana msajili alikuwa nje ya Dar Kikazi hivyo wakanitaka nirudi baada ya siku 3 lakini sikuweza kutokana na majukumu.

Kumbuka kwamba huyu msajili wa vyama ni tofauti na yule mzee wa Washiri (Tendwa)!!!

Karibu kwenye Ulimwengu wa NGOs. Lakini uwe mvumilivu, kama umekuja na ndoto za kuchakachua huku utachemsha na mwisho wa siku utaishia kusajili tu hiyo NGO na kubaki na makaratasi. Hii ndo changamoto kubwa inayowakabili wadau wa NGOs. Wengi wanakuja na ndoto za kupata ufadhili ndani ya muda mfupi, mambo yakiwa kinyume na hapo wanata tamaa mapema sana!!

GOOD LUCK!!!!!
 
Aksante sana ndugu yangu......jamaa ni mchungaji hivo yupo kiutumishi zaidi
 
Hebu pia ingia kwenye tuvuti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto , humo ndani utapata utaratibu rahisi sana wa kusajili NGO/CBO hasa zinazohusu maendeleo ya jamii. Hapo wizarani yupo Msajili wa NGOs. Utaratibu wao ni rahisi ila ngoma inakuja kwenye uandikaji wa katiba ya hiyo NGO/CBO. Binafsi naweza kuwasaidia katika nyanja hii kwani nina kauzoefu humu ka karibu miaka 12 Tuwasiliane tu.
 
1. Kuwe na wanachama waanzilishi au wajumbe wa Bodi.
Wajumbe wa bodi wanahitajika wangapi?
2. Kuwe na ofisi ya hiyo NGO kule inakofanyiakazi/inakotarajiwa kufanyiakazi (hapa wanaogopa kusajili NGO ya mfukoni/Briefcase - ingawa kwa mission town jamaa huwa wanasajili).

3. Kuwe na Katiba ya hiyo NGO (ambayo sharti iwe imepitishwa na wanachama waanzilishi wote au hao wajumbe wa Bodi). Hii katiba unatengenezea wapi? Kuna watu wanaofanya hii kitu? Eg: Lawyers Baada ya kuwa imeandikwa hiyo Katiba Mkuu wa Wilaya/DAS atapenda kuiona (hii ni aina fulani ya ukiritimba). Baada ya hapo mtaandika barua kwa msajili wa vyama (huyu huwa yuko Wizara ya Mambo ya Ndani) ya kuomba kusajiliwa ambayo itapitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata, Mkuu wa Wilaya (ambako ofisi zenu zipo). Pia Mkuu wa Wilaya atawaandikia barua ya utambulisho kwa msajili wa vyama akitambulisha uwepo wenu katika Wilaya yake.

4. Baada ya kumaliza huo mlolongo wa Wilayani utatakiwa kwenda Dar-Es-Salaam kwenda kusajili hiyo NGO, utaenda na nakala 3 za Katiba yenu iliyopitishwa na wanachama waanzilishi au wajumbe wa Bodi ya hiyo NGO na sahihi zao.
Usajili lazima ufanyike DSM? Mikoani hakuna ofisi za msajili?
5. Utatakiwa kuwa na fedha/Ada ya usajili Tsh. 100,000/=

6. Fedha ya ada ya Mwaka mmoja (1) Tsh. 40,000/= (Local NGO) pia utatakiwa kuwa na Tsh. 10,000/= kwa ajili ya fomu ya usajili.

Fedha yote hii utailipa mara baada ya kitengo cha sheria kuwa kimejiridhisha na Katiba yenu kwamba imekaa vizuri na hivyo watakuelekeza mahali pa kwenda kulipia hiyo fedha na kupewa stakabadhi za Serikali (ERV)

Kama Katiba yenu itakuwa imekaa vizuri baada ya kitengo cha sheria pale kwa msajili kuipitia na kuridhika nayo utakuwa umefanikisha usajili ambao mpaka kufikia kupata cheti chenu cha usajili inaweza kuchukua mpaka siku 15 za kazi. Pengine unaweza kuwa na bahati ukamkuta Msajili mwenyewe yuko ofisini na watu wa kitengo cha sheria ukawakuta na morale ya kazi unaweza kukamilisha zoezi hili ndani ya siku 2. Hata ya kwangu nilikuwa nifanikishe ndani ya siku 2 lakini haikuwa hivyo maana msajili alikuwa nje ya Dar Kikazi hivyo wakanitaka nirudi baada ya siku 3 lakini sikuweza kutokana na majukumu.

Kumbuka kwamba huyu msajili wa vyama ni tofauti na yule mzee wa Washiri (Tendwa)!!!
Huu mlolongo wa kwenda urudi ni mrefu sana kuna namna ya kuupunguza? Labda kuna jamaa wanafanya hii yote kwa niaba ya founder wa NGO?
Karibu kwenye Ulimwengu wa NGOs. Lakini uwe mvumilivu, kama umekuja na ndoto za kuchakachua huku utachemsha na mwisho wa siku utaishia kusajili tu hiyo NGO na kubaki na makaratasi. Hii ndo changamoto kubwa inayowakabili wadau wa NGOs. Wengi wanakuja na ndoto za kupata ufadhili ndani ya muda mfupi, mambo yakiwa kinyume na hapo wanata tamaa mapema sana!!

GOOD LUCK!!!!!
Check maswali yangu ya rangi NYEKUNDU
 
Check maswali yangu ya rangi NYEKUNDU

Maswali yako nimeyaona mkuu!

Wajumbe wa Bodi wanatakiwa wasipungue 10 (humo ukifanya uchaguzi utapata mwenyekiti, Katibu, Mtunza fedha/Mweka hazina wa Bodi na wajumbe wa bodi). Mara nyingi Katibu wa Bodi anakuwa Mkurugenzi mtendaji wa hiyo NGO ingawa wakati mwingine mnaweza kumpata kwa kufanya uchaguzi wenu wa ndani).

Uandishi wa katiba siyo lazima uwapelekee wanasheria (ingawa pia ni vizuri zaidi - na hasa kama mna pesa ya kumlipa huyo jamaa), hii mnaweza kuifanya wenyewe kama NGO (yaani wanchama waanzilishi). Mkipata sampuli ya katiba yoyote ya NGO inakuwa rahisi katika uandishi wa hiyo katiba (Sampuli nyingi zinapatikana kwenye mitandao - Just google NGOs' constitution sample). Ukishaipata mna-edit kutokea hapo huku mkiongezea maneno yenu mnayoona yanafaa kuingizwa kwenye katiba yenu. Kama yote haya yanapatikana kirahisi kwa nini uliwe pesa yako? Mwanasheria (Commissioner of Oaths) anaweza kula hela yenu kwa kuthibitisha kuwa ni halali na ilijadiliwa na wanachama.

Mikoani ndugu yangu hawa jamaa hawajafungua ofisi zao, hivyo ni lazima iwe Dar tu! (Labda kama wamefungua hivi karibuni).

Ndiyo mlolongo ni mrefu lakini haina jinsi kama umedhamilia kufanya kitu sidhani kama utaona ni usumbufu kwenda Dar mara 2 au 3. Ukitaka mission town mbona wapo kibao!! Ila lazima upate mtu mwaminifu vinginevyo unaweza kuliwa kekundu jamaa akapotea na mzigo!!

NAKUTAKIA MAFANIKIO!!!
 
Habari zenu.
Mimi ni kijana nina Stashahada ya kawaida (ordinary Diploma) Ya Ustawi wa Jamii pamoja na Uzoefu kidogo katika kufanya kazi za jamii nilioupata kabla ya kujiunga na Chuo kwa kufanya kazi za kujitolea katika mashirika tofauti.
Nina mapenzi makubwa na fani yangu lakini bahati mbaya ni kwamba Tangu nimemaliza Chuo Mwaka jana sijapata ajira na hivyo huwa nafanya kazi za muda mfupi pale ninapohitajika mahali fulani na hivyo najikuta natumia muda wangu bila kuwa na kazi rasmi.
Nikashauriana na familia yangu na kufikia Uamuzi wa kusajili Taasisi ambayo itafanya kazi za kijamii ambapo nitashiriki kwa kiasi kikubwa pamoja na kujenga uwezo kwa vijana waliopo vyuoni na wanaomaliza mafunzo kupata uzoefu.
Swali langu ni Je, kwa elimu yangu nina uwezo wa kuanzisha Taasisi na kupata Usajili?
Pia naomba mnielekeze taratibu za kufuata ili kusajili.
Nawakilisha.
Piga 0684478000
 
wadau nisaidieni viambatanisho vinavyohitajika kusajili NGO kwa ngazi ya wilaya, mkoa, na taifa.

je kuna gharama yoyote? vitu gani nizingatie kama angalizo ktk usajili?

Asanteni!
 
Habari ya wana JF naamini ya kuwa humu ni jawabu la kila kitu ndugu zangu,naombeni msaada juu ya taratibu zote za kusajili N'Go na wapi wanakosajili....msaaada jaman!!!!!!!Aksante.
Habari ndugu. wengi wamejitahidi kukueleza, kwa kifupi sheria inaruhusu watu kuanzia watano kufungua NGO. Lakini kutokana na mfumo wa NGO ulivyo mnapokuwa wengi ndivyo inavyokuwa na legitimus kubwa. Hivyo ni bora mkawa zaidi ya watano angalau nane. Mtafanya kikao na kuchagua uongozi. Documents za usajili zitaandaliwa na kisha process kuanza. process huanzia serikali ya mtaa, kata, wilaya na kumalizia wizarani. Inaweza ikawa wizara ya mambo ya ndani au wizara ya maendeleo ya jamii kutegemeana na lengo la NGO husika.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini au kwa email au fika ofisini kwetu. Karibu sana.
 
Habari wadau naomba kujua taratibu za kusajili NGO hapa Tanzania zikoje?
 
Back
Top Bottom