Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
William Shakespeare ni kielelezo cha lugha ya kingereza. Alikuwa mshairi, mtunzi wa michezo ya kuigiza na mcheza sinema, aliishi 1564 - 1616. Ni mmoja wa watu ambao wametoa mchango mkubwa sana katika kuikuza lugha ya kingereza. Kinachokera sana ni kuwaona watu wakitaka marais wa nchi za kiafrika wawe watumwa wa lugha ya kingereza kiasi cha kuwa na ufundi wa kuongea kingereza kwa kiwango cha Shakespeare.
Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtaalam sana wa lugha ya kingereza, alikizungumza bila ya kusoma sehemu tena mbele ya wasomi wa kiwango cha juu sana. Lakini miaka mitano ya mwisho ya Nyerere Tanzania ilikuwa na uchumi mbovu kupita maelezo. Tulikula ugali wa njano usio na ladha mdomoni (yanga), mama zetu walivaa nguo za kupika. Mwalimu Nyerere alitaka kupinduliwa kutokana na ugumu wa maisha nyakati zile. Kingereza chake hakikuwa na msaada kwa masikini wa hali ya chini kabisa.
Mzee Mwinyi naye anajua kingereza, ni mwalimu mstaafu. Lakini kitu kinachoitwa ruksa kiliitia doa awamu ya pili. Kutokusanya kodi kuliongeza umasikini wa watu. Kingereza chake hakikumsaidia kikazi.
Mzee Mkapa ni fundi kweli kweli wa lugha ya kingereza. Akianza kuongea unatamani aendelee tu, unatamani umsikilize. Lakini awamu ya tatu ilibinafsisha mashirika, ikauza nyumba za serikali. Kingereza cha Mkapa hakijamsaidia katika kukwepa rundo la tuhuma kutoka kila kona.
Mzee Kikwete naye ni fundi wa kingereza, amehudhuria mikutano mingi sana, huyu ni mwanadiplomasia wa kiwango cha juu sana. Lakini makontena zaidi ya 11,000 yametoka nje ya bandarini bila ya malipo yote stahili kukamilika. Mafuta kutoka nje ya nchi yanaingizwa bila ya usimamizi makini. Kingereza chake cha kwenye mikutano hakijaisaidia nchi katika kuweza kuyapunguza matatizo yote yaliyojitokeza katika awamu ya nne.
Rais Magufuli naye anaanza kupimwa kupitia uwezo wa kuongea kingereza. Anapimwa kupitia mbwembwe za kisomi wakati amepigiwa kura na mamilioni ya watu ambao walikuwa tayari kupanga foleni juani ili waweze kumpigia kura. Awamu yake ikiisha atahukumiwa kwa kutazamwa kama aliweza kupambana na shida zinazoyakabili maisha ya walio wengi, hatapimwa kwa uwezo wake wa kuongea kingereza, atakumbukwa kwa kuleta tija inayoonekana.
Tunachagua rais ashughulike na shida za masikini wa nchi hii, hatumchagui William Shakespeare.