kinyangesi
JF-Expert Member
- Jul 15, 2012
- 247
- 86
Habari wanajamvi?
Mimi nna mwenzi wangu ambaye tumepanga kutambulishana kwa wazazi mwishoni mwa mwaka huu. Huyu binti ambaye natarajia awe mke wangu tulijuana zaidi ya miaka 6 ivi ila si kama wapenzi.
Tatizo linalomsumbua ambalo nimeona niombe ushaur wenu ili nimsaidie ni kwamba alipokuwa anasoma Sekondari aliwahi kukamatwa akifanya mapenzi, alifukuzwa shule na baadae wazazi waliamua kumuamisha Mkoa akaendelea na kumaliza elimu yake.
Sikuwahi kuijua story hii mpaka tulipokuwa wapenzi ndo aliniadithia. Amekuwa akirudia mara kwa mara kuniambia tukio lile la aibu uwa linamuumiza sana sasa hata anaogopa kuwaambia wazaz wake kuwa ana mtu anayetaka kumtambulisha ili baadae niwe mumewe.
Mimi na yeye tunaishi mikoa tofauti kwani yupo Arusha nami nipo Dar, pia sijawahi kufanya nae mapenzi. Mnishauri wana Jf jinsi ya kumsaidia huyu binti kwani nampenda.
Nahitaji awe huru