Anatamani arudishiwe hela zake

Anatamani arudishiwe hela zake

basha unguja

Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
83
Reaction score
77
Wasaaalamu,

Kuna best alikuwa anatupa story!

Kuna jamaa alikuwa amekutana na msichana mmoja mrembo sana chuoni kwao alipokuwa akisoma jamaa alikuwa mwaka wa pili na yule binti alikuwa mwaka wa kwanza , kutokana na uzuri wa yule binti mshkaji akaona ajikombekombe kwa yule demu ili kama vipi mshkaji akamatie fursa.

Mshkaji pamoja na kukutana na mrembo siku zote hakuwahi kumwambia dhamira yake ila kutokana na maisha waliyokuwa wakiishi aliamini ataingia king muda wowote ule coz walikuwa na tabia ya kutembeleana geto, kula pamoja na kutoa out pamoja.

Kutokana na matukio hayo mshkaji akajipa uhakika wa asilimia mia kuwa yule ni kuku wake tu, kutokana na ukaribu wao hadi marafiki zao walikuwa wakiwatania mtu na mchumba wake, na kutokana na uzuri wa yule binti, yani mshkaji akisikia hivyo anajihisi kama vile anatembea angani katika zero gravitation, hata miondoko alikuwa akitembea as if yeye ndiye mmiliki halali wa yule binti.

Siku moja yule binti hakuwa na furaha kiasi cha yule mshkaji kumuuliza kulikoni mrembo mbona hivyo? Yule binti kwa upolee akajibu, "yani we acha tu, ninashida hapa kama ya laki hivi" Jamaa kwa kujitutumua akijua anawekeza akampa mrembo laki na nusu huku akimsihi kama akiwa na shida asisite kumwambia. Kiukweli yule mdada alifurahi mno, akamshukuru yule kaka kisha akasepa zake.

Kesho yake mshkaji akakutana na yule mrembo akiwa na furaha tele, bila kujali mshkaji akamwambia naona leo unafuraha kweli kweli bila shaka tatizo lako liko solved? Yule Binti akafunguka, yaani huwezi kuamini ile hela uliyonipa haijanisaidia peke yangu, mpenzi wangu alikwama hela ya kujikimu hivyo aliponiambia ile hali ilikosesha sana raha, hivyo uliponipatia zile pesa nikatumia zote na hivyo hakuamini hata kidogo, huku yule mrembo akitoa simu yake na kumuonyesha mshkaji sms alizotumiwa na mpenzi wake hali, jinsi alivyoshukuru.

Mshkaji alihisi kama, jua limebadili direction ya kuchomoza na kuzama, kama jua lina chomoza Kaskazini na Kuzama kusini vile, ghafla tumbo lake lilivurugika na alihisi kama homa kali sana na aliondoka bila kumuaga yule mrembo! Yule mrembo asielewe nini kinaendelea akabaki na butwaa.
Mshkaji unaambiwa kutokana na mawazo yale alipata hadi vidonda vya tumbo. ILA ANATAMANI HADI LEO ZILE PESA ZAKE ARUDISHIWE TU, Roho inamuuma sana.

NB: TENDA WEMA NENDA ZAKO, KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI, SEMA YA MOYONI ILI MOYO UWE HURU, CHUNGA CHA KUONGEA!
 
Aise mwambie ajifunze.. usije mpa hela mwanamke ambae.. humfaham vizur au hata kwama unampango nae.. mpaka ujue status yako kwake. Lasii hivyo pesa inaliwa na hupati kitu
 
huyu jamaa asamehe tu ila kinauma kinoma tena sana..... cha kufanya ili asijiumize kihisia zaidi sasa akae mbali kabisa na huyo manzi hiyo itasaidia maana manzi ashamzidi akili kilichobaki akimbie tu na wale asiweke kinyongo cha hela hayo mambo ya kawaida
 
huyu jamaa asamehe tu ila kinauma kinoma tena sana..... cha kufanya ili asijiumize kihisia zaidi sasa akae mbali kabisa na huyo manzi hiyo itasaidia maana manzi ashamzidi akili kilichobaki akimbie tu na wale asiweke kinyongo cha hela hayo mambo ya kawaida[/QUOTE
Yakhe! sasa hiyo ni miaka ya nyuma sasa je, ingekuwa kipindi hiki cha uncle hahaha sipati pichA
 
Hivi kumbe ile misaada mnayotupa huwa mawazo yenu ni mwisho wa siku mtugegede, acheni hizo jamani.
 
Back
Top Bottom