Anataka nimuoe ilihali sina kazi

Anataka nimuoe ilihali sina kazi

Kwa kipindi hiki alicho nuna, ikitokea amepata jamaa mwingine ambae hajapata ajira na akakubali kumuoa kwa ahadi ya kutumia mshahara wa huyo mwanamke.
Je, utakuja kuleta uzi wa kujiliza kwa malalamiko tena?
 
Mmmh mzee....

Mie demu wangu anasema mwaka huu ukiisha next year lazima AOLEWE. Anasema umri unaenda...
Mie namsikilizia tu mzee, hata sina presha.
Ndio kwanza ERB hawajani approve kuwa Profesional Engineer halafu nikimbilie kuoa..
HIZO NI AKILI MATOPE!!!!

Ndoa mkataba mzee, jipange kwanza.

#Chief Eng.
Mkuu hawa viumbe wananichekeshaga sana sijui hili suala la ndoa wanalichukuliaje wao
 
Yaani wewe ni mtumwa wa fikra zako mwenyewe unadhani mpaka upate ajira ndio utakuwa mwanamme kamili.Kama binti atakuwa na uwezo wa kukupa hela ukalipie mahali chukua zigo hilo .Uwoga wako ndio umasikini wako.
 
Ujinga ni sifa, baada ya masomo yako bado "una sifa ya ujinga" wa kutambua "bahati" utakuja kuowa tegemezi we binadamu changamka kazi ni kazi hata ligilove ni kazi
 
Kua consistent. Kama unataka unataka, kama hutaki usimwambie asubiri miaka minne.
 
Ujinga ni sifa, baada ya masomo yako bado "una sifa ya ujinga" wa kutambua "bahati" utakuja kuowa tegemezi we binadamu changamka kazi ni kazi hata ligilove ni kazi
Kwa hyo unaoa mwnye kaz ili akusaidie maisha kwa kuwa ww yamekushndaaa?.....Aina ya ujnga huu n mzgo wa hatar
 
Usijaribu akichoka kukulea utagongewa,utanyanyaswa ,kila atakachosema utafanya ata chooni utapiga deki vumilia kwanza pata kazi alaf ndo mfunge Ndoa
 
Mkuu sikiliza moyo wako..Daima mshahara wa mwanamke ni wakwake mwenyewe.Wewe ndio kichwa hata kama yeye ni shingo asikuzungushe anavyotaka..Kwa huo mshahara wake hawezi kukuvalisha akulishe bado mjenge na matumizi madogmadogo...
Kijana wenzangu nafuta ajira kwanza uwe na pesa yako hata kama hautajenga mapema
 
Huyu binti nilikutana nae chuo mwaka 2014 nayeye alikuwa anasoma hapohapo chuo ila coz tofauti na niliyokuwa nasomea mimi, mm nilikuwa nasoma mambo ya tourism na yeye alikuwa anasomea childhood. Baada ya kufahamiana tukaanza urafiki na baadaye tukawa wapenzi, alipomaliza chuo mwaka jana akaomba fld moja kati ya shule za private hapa mjini na kwa bahati nzuri alipata fld na alipomaliza fld kutokana na kufanya vizuri kipindi yuko training ile shule ikaamua kumuajiri moja kwa moja kwa sababu na wenyewe walikuwa wanahitaji mwalimu kwa kipindi hicho hivyo wakaona heri wamchukue yeye. Mimi pia nilipomaliza nikaomba fld TANAPA maana mm nilisomea tourism na nashkuru mungu nilipewa nafasi ya training moja kati ya hifadhi zetu hapa nchini na juzi ndo nimemaliza na kwa sasa nipo mtaani natafuta ajira. Sasa tangu nirudi kutoka fld nashangaa huyu binti kaja na wazo anataka tuoane kwa sasa tofauti na mipango yetu, tulikubaliana kuwa tutakapo pata kazi tujipange kwanza angalau tuwe tumeshajenga ili tukioana angalau tuishi kwetu maana mm kwa sasa bado naishi na wazazi wangu ila nashangaa yeye analazimisha tuoane kwa sasa wakati naendelea kutafuta kazi eti kwa kisingizio kuwa tutatumia mshahara wake kujikimu na maisha wakati naendelea kutafuta kazi ila mm nimekataa katukatu kumuoa kwa sasa maana tulikubaliana tutaoana miaka minne ijayo. Sasa tangu jana kanuna hataki kunisemesha wala kuelewa yeye anachotaka tu ni ndoa kwa sasa. Ila mm nimemwambia ukweli kwamba kumuoa kwa sasa ni vigumu ingawa nampenda huyu binti na nina malengo naye na sababu sinazonifanya nisioe nimemwambia kwanza mm sina kazi pili sijajipanga na mbaya zaidi bado naishi na kwa wazazi wangu ila yeye hataki kunielewa. Hebu nishaurini wana JF nifanyeje maana naona huyu mchumba wangu anaanza kunivuruga kwa kuanza kwenda kinyume na mipango yetu tuliyokubaliana hapo awali juu ya kuoana kwetu.
Washirikishe wazazi wako labda wanaweza wakakusaidia amgalau mtaji wa milioni mbili tatu ufungue duka maisha yaanze...
 
mkuu mimi nakushauri uweke booking kwa kumtundika mimba ili uongeze kasi ya kutafuta hiyo kazi,otherwise wanakubebea huo mzigo soon...usije kudondosha tena chozi hapa!
 
Mkuu sikiliza moyo wako..Daima mshahara wa mwanamke ni wakwake mwenyewe.Wewe ndio kichwa hata kama yeye ni shingo asikuzungushe anavyotaka..Kwa huo mshahara wake hawezi kukuvalisha akulishe bado mjenge na matumizi madogmadogo...
Kijana wenzangu nafuta ajira kwanza uwe na pesa yako hata kama hautajenga mapema
Kweli mkuu nashkuru sana
 
Nothing is good or bad but your thinking make it so.

Ni vizuri kama wote mna malengo sawa na mnaweza kufika mnakotaka, anzeni na Ndoa ya kimila. Katoe mahali binti wa watu "pressure" imshuke.

Ukimaliza kufanya hivi endelea kukaa kwenu huku ukitafuta jinsi ya kujiingizia kipato. Mambo yakiwa kwenye mstari mnapelekana kwenye nyumba ya ibada.

Mwenzio ana "hangover", ili imtoke anahitaji kuitwa mke wa fulani.
 
Usioe ukitegemea pesa za mwanamke subir ujipange afu huyo mwanamke anayelazimisha kuolewa namuonea huruma hajui alitendalo
 
Ngoja nijikumbushe ka msemo ka bibi yangu mwaka 1960
UKITUMIA AKIKI NYIIIIIIINGI KWENYE NDOA UJUE MAALIFA YAKO YA KUFIKIRIA FAMILIA NI MADOGO MNO

Sikuwahi kumuelewa mpaka ilipofika miaka ya 1974 ndio nikaja kumuelewa
Aliekuwa TAYARI KUOLEWA WAKATI HUO MIMI SIKUWA TAYARI

NILIPOKUA TAYARI WAKATI MWINGINE WA KUOA NILIYETAKA KUNUOA HAKUA TAYARI

Hapo ndio nikaitafakari sentenei ya bibi yangu

Inasemekana japo sina uhakika kwa nyie vijana mtaihakiki hiii kua
Mwanaume yeyote anapogundua mpenzi wake anahitaji kuolewa na yeyw hujihisi kama vile anabahati kuliko wanaume wengine na wakati mwingine hufika mbali zaidi kufikiria kua wasichana wote wako tayari pindi atakapotaka kuoa.

Ukisubiri ujipange hata upewe miaka mia hutojikamilisha na ni kitu cha kushangaza na umri wote huo bado unakaa kwenu, kweli vijana wa siku hizi ni shida

Ok ni vema kama hauko tayari kumuoa mpe nafasi aolewe kwani amejitambua abagitaji kuitumikia familia yake akiwa bado kijana na anaoenda azitumie nguvu za ujana wake kuilea familia yake,
Wewe uendeleee kujipanga huju unachangis mlango mmoja na baba yako

Angalizo
Naamini mbeleni utamkumbuka huyo dada, ikumbukwe si kila aliesoma hupata kazi
Wakati mwingine elimu yako inapaswa ikutumikie na sio wewe uitumikie

Kwa mfano ungeamua kua mjasiria mali mkeo akawa mtaji huku ukisubiri hizo kazi

Ikumbukwe kuna watu wana miaka kama kumi na ushehe hawajapata ajira toka wamalize vyuo
 
Back
Top Bottom