Anataka nimuoe ilihali sina kazi

Anataka nimuoe ilihali sina kazi

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2016
Posts
533
Reaction score
741
Huyu binti nilikutana nae chuo mwaka 2014 nayeye alikuwa anasoma hapohapo chuo ila coz tofauti na niliyokuwa nasomea mimi, mm nilikuwa nasoma mambo ya tourism na yeye alikuwa anasomea childhood. Baada ya kufahamiana tukaanza urafiki na baadaye tukawa wapenzi, alipomaliza chuo mwaka jana akaomba fld moja kati ya shule za private hapa mjini na kwa bahati nzuri alipata fld na alipomaliza fld kutokana na kufanya vizuri kipindi yuko training ile shule ikaamua kumuajiri moja kwa moja kwa sababu na wenyewe walikuwa wanahitaji mwalimu kwa kipindi hicho hivyo wakaona heri wamchukue yeye. Mimi pia nilipomaliza nikaomba fld TANAPA maana mm nilisomea tourism na nashkuru mungu nilipewa nafasi ya training moja kati ya hifadhi zetu hapa nchini na juzi ndo nimemaliza na kwa sasa nipo mtaani natafuta ajira. Sasa tangu nirudi kutoka fld nashangaa huyu binti kaja na wazo anataka tuoane kwa sasa tofauti na mipango yetu, tulikubaliana kuwa tutakapo pata kazi tujipange kwanza angalau tuwe tumeshajenga ili tukioana angalau tuishi kwetu maana mm kwa sasa bado naishi na wazazi wangu ila nashangaa yeye analazimisha tuoane kwa sasa wakati naendelea kutafuta kazi eti kwa kisingizio kuwa tutatumia mshahara wake kujikimu na maisha wakati naendelea kutafuta kazi ila mm nimekataa katukatu kumuoa kwa sasa maana tulikubaliana tutaoana miaka minne ijayo. Sasa tangu jana kanuna hataki kunisemesha wala kuelewa yeye anachotaka tu ni ndoa kwa sasa. Ila mm nimemwambia ukweli kwamba kumuoa kwa sasa ni vigumu ingawa nampenda huyu binti na nina malengo naye na sababu sinazonifanya nisioe nimemwambia kwanza mm sina kazi pili sijajipanga na mbaya zaidi bado naishi na kwa wazazi wangu ila yeye hataki kunielewa. Hebu nishaurini wana JF nifanyeje maana naona huyu mchumba wangu anaanza kunivuruga kwa kuanza kwenda kinyume na mipango yetu tuliyokubaliana hapo awali juu ya kuoana kwetu.
 
Watu wengine sijui kwanini huwa mnachezea bahati. Wewe hujui kuwa hata ukitumia vilivyo na vizuri hicho kiungo chako " korofi " kwa huyo Mwanamke tayari ni ajira kwako tosha kwani kwa " mpini " utakaokuwa unampa unaweza kupata " mijihela " ambayo hata Ofisini usingezipata achilia mbali fursa zingine nyinginezo. Acha " ubwege " Kijana.
 
fata moyo wako mdogo wangu. kama unaona hujawa tayari mwambie na shikilia msimamo wako. kama ni wako atakua tu wako.
 
Watu wengine sijui kwanini huwa mnachezea bahati. Wewe hujui kuwa hata ukitumia vilivyo na vizuri hicho kiungo chako " korofi " kwa huyo Mwanamke tayari ni ajira kwako tosha kwani kwa " mpini " utakaokuwa unampa unaweza kupata " mijihela " ambayo hata Ofisini usingezipata achilia mbali fursa zingine nyinginezo. Acha " ubwege " Kijana.
Jinga kabisa..
 
yaan hapo ndio mapenz ya chuo yanaponifurahisha.... mkimaliza tu mwezio anaona umri umeenda wewe unaona maisha ndio yameanza... nweis baki na msimamo wako mkuu maisha ya ndoa si mepesi kivyo na hata ndugu zako watakushangaa ukienda kuwaambia hilo...
 
Sasa jamaa we umekataa katu katu AF bado unakuja apa kutuomba ushauri unategemea sie tukushauri vp sasa ikiwa we umekataa katu katu
Tupe namb za uyoo dada sie waowaji tukuoneshe jinsi ya kufanya
 
yaan hapo ndio mapenz ya chuo yanaponifurahisha.... mkimaliza tu mwezio anaona umri umeenda wewe unaona maisha ndio yameanza... nweis baki na msimamo wako mkuu maisha ya ndoa si mepesi kivyo na hata ndugu zako watakushangaa ukienda kuwaambia hilo...
Kweli kaka wala sitathubutu kuwaambia
 
Mangi usije ukaingizwa chaka, ukakubali kuoa kwa kigezo kwamba mtajimudu kwenye maisha kupitia mshahara wake itakula kwako mazima. Cha msingi awe mvumilivu mbona kama bado ni babe girl, ila kua makini anaweza kukutana na anaetaka kuoa kwasababu yeye anataka kuolewa, ataolewa tu.
 
Back
Top Bottom