Anataka kunipeleka ustawi wa jamii

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,916
24,674
Nipo kwenye mtihani sana siku hii ya leo Mr Zero,
Huyu binti nilizaa nae tu ile one take na sikuwa na nia ya kumuoa awe mke wangu,sasa tatizo linakuja kwamba leo amekuja kuninyea hapa kwa maneno ya shombo na kutishia kwamba ananipeleka ustawi wa jamii,

Siyo kwamba sitoi huduma hapana na nafikiri katika vitu ninavyojitahidi kuviangalia na kuhudumia basi ni huyu mtoto,

Hakuna homa inayompata nisimchukue na kumpeleka hospital, hela ya matumizi natoa kadri ninavyopata,

ila tatizo ni kwamba huyu binti anapenda vikubwa akiomba kitu kwa sababu ya mtoto ukimwambia asubiri kidogo umtafutie anang'aka yeye anataka papo kwa papo,

Kiukweli hali si hali na hivyo anaona naingiza kidogo kitu kwenye kibanda changu cha kiepe anajua basi kila siku nakuwa na hela, anasahau kwamba nina majukumu mengine nje ya mtoto,

Mi nilimwambia kitu kimoja tu aende uko ustawi wa jamii kama anaona huduma zangu hazimtoshelezi,CC Zero IQ
 
Wakati mnatiana mimba mlitushirikisha!?
Pambana na hali yako Mr akili zero

Sent by Diaspora
 
Hakuna sehemu nzuri utapata unafuu wa kutoa matumizi Kama ustawi wa jamii.
Kama ulikuwa unampa 200k itawekwa kisheria apewe 45000/-

Yaani mkitoka ustawi wa jamii huyo mwanamke anakuja kukuomba samahani ili uendelee kumpa kiasi ulichokuwa unampa mwanzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu alipost kuwa wauza viepe mnaingiza laki 2 kwa siku huyo bado anakusumbuaje mkuu!
 
Back
Top Bottom