Anataka kujiua

Anataka kujiua

Kifulambute

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2011
Posts
2,539
Reaction score
764
Habari za asubuhi great thinkers, nisaidieni kwa ushauri wenu kwa huyu rafiki yangu maana naona anaelekea shimoni na jini mauti anamsumbua.

Alikuwa anafanya kazi shirika moja hapa mjini na kwa kweli kwa background yake amepambana sana kuwasaidia wazazi wake na yeye pia, na wanamtegemea 100%, mwezi wa nane alisimamishwa kazi na alikuwa na mkopo bank(unsecured loans guaranteed na employer), sasa ametafuta kazi hajapata na bank wanamsumbua...juzi nilienda kumtembelea kwake kiukweli anakoelekea siko kuzuri maana nilijaribu kumdadisi namna gani amejipanga kurudisha mkopo na kuendelea kupambana...inaonesha amekata tamaa ya kuishi. Kwa bahati tu siku hiyo niliwahi alikuwa kanunua dawa ya panya na alikuwa ready kuinywa nikamshauri sana akawa kama amenielewa..lakini jana tena mke wake kanipigia alitaka kunywa dawa za variam...sasa mi kama rafiki wake wa karibu nakuwa busy kumshauri..naombeni mniongezee maneno ya kumshawishi na.kumnusuru maisha yake
 
Dah aisee nasikitika sana kuusoma huo ujumbe wako. Mi ilishanikuta hiyo makitu lakini sijafikia wa la kufikiria kujiua, bado CV zangu zinanibeba sana kwenda ninakotaka kwa field yangu....mi nadhani asikate tamaa,bado maisha atayamudu tu...I hope hata 35 hajafika bado. Mtahadhalishe mkewe awe nae karibu sana manake inaonesha akipata mtu wa karibu kwa advice jamaa anaelewa na mtu wa advice akiwa mbali jamaa anaingiwa na pepo.

Kikubwa kama hiyo kazi aliipata kwa kubahatisha then itamcost bt kama CV na vyeti vyake vipo safi akomae tu, mkopo huwa ni nouma sana.
 
Kama kweli unampenda
1.Mtafutie kazi ingine
2.Tafuta hela mkafute deni bank.
 
habari za asubuhi great thinkers, nisaidieni kwa ushauri wenu kwa huyu rafiki yangu maana naona anaelekea shimoni na jini mauti anamsumbua.

Alikuwa anafanya kazi shirika moja hapa mjini na kwa kweli kwa background yake amepambana sana kuwasaidia wazazi wake na yeye pia, na wanamtegemea 100%, mwezi wa nane alisimamishwa kazi na alikuwa na mkopo bank(unsecured loans guaranteed na employer), sasa ametafuta kazi hajapata na bank wanamsumbua...juzi nilienda kumtembelea kwake kiukweli anakoelekea siko kuzuri maana nilijaribu kumdadisi namna gani amejipanga kurudisha mkopo na kuendelea kupambana...inaonesha amekata tamaa ya kuishi. Kwa bahati tu siku hiyo niliwahi alikuwa kanunua dawa ya panya na alikuwa ready kuinywa nikamshauri sana akawa kama amenielewa..lakini jana tena mke wake kanipigia alitaka kunywa dawa za variam...sasa mi kama rafiki wake wa karibu nakuwa busy kumshauri..naombeni mniongezee maneno ya kumshawishi na.kumnusuru maisha yake
mkopehse hela ili aweze kulipa deni au nenda kwa hiyo benki eleza madhara anayoyapata mteja wao kwa usumbufu wanaompatia kufuatilia deni lao wakati hana kazii
 
mkuu kawaida ya mikopo ya namna hiyo benki hawaidai baada ya MTU kusimamishwakazi,kinachotakiwa baada ya yeye kusimamishwa kazi atoe taarifa benki ili mkopo usimamishwe,then atakapopata kazi sehemu nyingine atatoa taarifa ili waendelee kumkata,hii mifano nimeiona kwa staff mwenzangu,na kawaida loan kama hiyo benki wanakuwa wameshaikatia bima ila wakiona hujui huo utaratibu ndo hua wanasumbua
 
Kama kweli unampenda
1.Mtafutie kazi ingine
2.Tafuta hela mkafute deni bank.

Mkuu deni kubwa na nampenda msela.tumetoka mbali ila na mimi nina majukumu meeeengi sana kama watz tulivyo..jamaa ana qualification nzuri sema ni mwepesi wa kukata tamaa sana
 
Habari za asubuhi great thinkers, nisaidieni kwa ushauri wenu kwa huyu rafiki yangu maana naona anaelekea shimoni na jini mauti anamsumbua.

Alikuwa anafanya kazi shirika moja hapa mjini na kwa kweli kwa background yake amepambana sana kuwasaidia wazazi wake na yeye pia, na wanamtegemea 100%, mwezi wa nane alisimamishwa kazi na alikuwa na mkopo bank(unsecured loans guaranteed na employer), sasa ametafuta kazi hajapata na bank wanamsumbua...juzi nilienda kumtembelea kwake kiukweli anakoelekea siko kuzuri maana nilijaribu kumdadisi namna gani amejipanga kurudisha mkopo na kuendelea kupambana...inaonesha amekata tamaa ya kuishi. Kwa bahati tu siku hiyo niliwahi alikuwa kanunua dawa ya panya na alikuwa ready kuinywa nikamshauri sana akawa kama amenielewa..lakini jana tena mke wake kanipigia alitaka kunywa dawa za variam...sasa mi kama rafiki wake wa karibu nakuwa busy kumshauri..naombeni mniongezee maneno ya kumshawishi na.kumnusuru maisha yake

Mi nimechoksa kila mtu akija rafiki yangu kakuta na ili aya bwana ayo ndo maisha ni kuishi cut
 
Sifa kubwa ya mtu anaetaka kujiua ni "secrecy"
hiyo itakuwa ni defensive mechanism
 
Ebwana endelea tu kumshauri, kujinyonga sio suluhisho, maisha ni kama mchezo wakuvuta kamba, huyu akivuta huku na mwingine(adui) anavuta kule. Awe nasubira tu na awe na imani na aendelee tu kuvuta kamba upande wake, atashinda yeye tu, is just the matter of time. Mungu anaweza yote, hakuna jambo gumu asiloweza. Yaliyomshinda mwanadamu ye anaweza. Asome Zaburi ya 71, 91 na 119 ( aanze na zaburi 51 kwaajili ya toba) na pia asome Isaya 44:25-28, Isaya 45:1-3, Isaya 42:22 na Yeremia 33:3!!. Awe na amani tu moyoni mwake mapito anayopitia yatakwisha tu.Hilo ni jaribu tu, na Mungu alitoa ahadi yakutotuacha tujaribiwe kupita uwezo wetu, lazima atafanya njia tu yakutokea.KRISTO TUMAINI LETU!!!
 
kwanza pole sana kwa yaliyompata mwezetu...pili aende akaongee na watu wa benk kuhusiana na yaliyompata..tatu asichoke kutafuta kazi yoyote ile sio lazima aliyosomea.nne aanzishe kabiashara chochote kitakachoweza kumsaidia katika kipindi hiki kuliko kuwa tegemez.mwisho mtafutie mwanasaikolojia wakumshauli kwa ukalibu..ni hayo tuuu
 
Mikopo itolewayo na bank ina bima,awajulishe bank,utaratibu wa kumkata utaendelea baada ya kupata kazi.
 
Mkopo wa benki mbona siyo ishu hiyo. Hebu ongea naye vizuri huenda kuna mambo huyajui, kuna watu ni wasiri balaa.
 
Sema jina la benki labda bosi mmoja atasoma na kuku pm.
Mwambie familia inamuitaji, na atavuka matatizo awe na imani ili aweze fuzu interviews. Tafuta ndugu zake wengine kama ameishi nao vizuri wanaweza msaidia as mambo duniani siku hizi ni networking.
 
Back
Top Bottom