Anatafutwa: Ted Kennedy wa Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anatafutwa: Ted Kennedy wa Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 1, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wasifu mkubwa wa Ted Kennedy ni Utungaji sheria, kupigania maslahi ya walalahoi, na kubwa ni kitendo chake cha kugombea kuchaguliwa kuwa mgombea wa Uraisi akiwakilishe chama cha Democrats akipingana na aliyekuwa Rais wa Marekani Jimmy Carter ambaye alikuwa naye ni Democrat.

  Je tunaweza kuona kitu kama hichi ndani ya CCM?

  Je kitendo cha Zitto kugombea uenyekiti kupingana na Mwenyekiti wake tutakiweka sawa na cha Kennedy kupingana na Carter?
   
 2. Sungi

  Sungi Senior Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sijui kama atapatikana hivi karibuni, ingawa naweza kusema walikuwapo zamani, nao hawakuishi maisha marefu. Tatizo la kwetu wanasiasa wengi wanaingia kwenye siasa wakiwa na nia ya kuwa matajiri, na "celebrities", na sio kwa dhumuni hasa la kutetea maslahi ya mnyoge, mwanakijiji ambaye hana mtu wakumsemea. Watu kama Kennedy, waliingia kwenye siasa kama wito na sio utajiri maana tayari familia yao ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, hilo la kwanza.

  Pili, wapo wanaojaribu kugombea nafasi hizi za juu, kama ambavyo tumeona, lakini wanashawishiwa kutoa majina yao kwenye list ya candidates. Lazima pia tutambue kwamba utamaduni wetu ni tofauti na wawazungu na kwa maoni yangu, kwa sababu ya hili (utamaduni) haliweza kutokea mara kwa mara. Kama watu wanasikilizana na kuamua kutogombea nafasi za juu kwa hiari yao ni vema sana. Mambo yalitokea Chicago kwenye hio democrat convention mwaka 1980 yalikuwa na athari kubwa sana kwa chama cha Democrat na nchi nzima, hata uhasama ambao uliendelea kichinichini kati ya mzee Carter na marehemu Ted, mpaka leo hii (mzee Carter akiri mwenyewe, juzi alipohojiwa na CNN).

  Kwa kifupi, akijatokea mwanasiasa mtanzania atakaye simamia haki ya wananchi wanyonge, ambaye hana hidden agenda, ila hii moja tu, ya kusaidia watanzania, itakuwa siku ya kumshukuru Mungu sana.
   
 3. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yah ryt Bro! Tanzania will tek long tym 4 tht to happen...
   
 4. b

  bambumbile Senior Member

  #4
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev. Kishoka,

  Na wewe ni matheory tu ya Wamarekani kila siku huku nyumbani watu hata kula kunawashinda.

  Vijana wenzenu wakitokea kugombea mnawapiga vita; sasa mnafikiri huyo mtu atatoka wapi?

  Kennedy hakuwa clean kwa matendo yake kama kijana lakini moyoni alikuwa mtu mzuri na alipopata nafasi akabadilika na kuwa mzuri katika matendo mpaka hapo alipofikia.

  Njooni nyumbani muje muanze na A, B, C badala ya kuhubiri mambo ya Marekani tu ambayo kwa kweli kwa huku nyumbani ni ndoto tu.

  Kinachonisikitisha nyie wasomi wetu na mlio kaa majuu ni WIVU wa KIKE ambao wengi wenu mnao. Mkiona mwenzenu mmoja anataka kufanya la maana mnaanza kuleta mambo ambayo hayana maana kabisa. Sababu kubwa inakuwa wivu; kama jambo huwezi kufanya wewe, akifanya mwingine ni WIVU tu.

  Wivu ndio unatufanya vijana hata tushindwe kusaidiana na kuaminiana na matokeo yake wote tunaganga njaa pale pale tu.

  Samahani kama nimetumia lugha mbaya lakini mambo mengine yanaudhi. Leo hii tunajadili mambo ya Zitto, wale mabingwa wa theories za demokrasia mko wapi? Mnaanza kuhalalisha au kukaa kimya. Kwenye suala la Mwakalinga nyie wenyewe ndio mlikuwa vinara wa kumchafua huku mnajua kabisa he is a good man. Wengine wakakaa kimya kama hawaoni. Jamaa yangu mmoja akasema hao wangependa hayo anayofanya Mwakalinga kwao wao ndio wangefanya, hapo ungewaona vichwa juu juu.

  Inabidi kuwaunga mkono watu kama akina Zitto; ndio kuna wakati watafanya makosa mengi maana hakuna asiyefanya makosa. Lakini angalia dhamira ya Zitto ni nzuri na ameonyesha mfano. Sisi tunakuja kumchafua hapa JF bila sababu za msingi kabisa.

  Mnataka hao wa kuibadili CCM au Tanzania watoke wapi?
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijui kama tunahitaji supporter wa abortion clinics kwa kisingizio cha rights of women to choose and same sex marriage Tanzania - simply ni abomination
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Sep 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Tanzania tunahitaji transformational figure kama Ronald Reagan....siyo maliberali kama huyo Kennedy
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  yaaah I agree!
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..familia ya kina Kennedy walikuwa wanapenda sana madaraka.

  ..kwa maoni yangu walihusika kuwahujumu Lyndon Johnson na Jimmy Carter kwa mambo ya kibinafsi na kupenda madaraka.

  ..Ted Kennedy alikuwa anajua kabisa kwamba alikuwa hawezi kumtoa Jimmy Carter who was a sitting President, lakini akalazimisha kugombea na kukihujumu chama.

  ..Jimmy Carter alishindwa uchaguzi na Ronald Reagan, ambaye alikuwa mkatili sana kwa nchi za Kiafrika haswa zilizofuata siasa za Ujamaa kama Msumbiji na Angola. pia Reagan ndiyo aliyewafadhili Mujahedeen[wasoviet walikuwa wawamalize hawa] ambao baadaye wakahitimu na kuwa Taliban na Al-Qaeda.

  NB:

  ..zile hotuba zake moto-moto zilikuwa zinatayarishwa na jamaa anaitwa Bob Shrum "the word smith of the kennedy's family."

  ..pia nimeona TED KENNEDY naye alikuwa akitumia TELEPROMPTER. kumbe teknolojia hiyo imekuwepo tangu miaka ya 1980.
   
  Last edited: Sep 1, 2009
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Sep 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Joka na wewe bana...yaani ulikuwa hujui kuwa prompter ziko mrefu? Wewe ulidhani Obama ndio kazivumbua nini? Aahahahahaha...wewe utakuwa umenyweshwa kool-aid ya Obama wewe
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Sep 1, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Nyani Ngabu,

  ..unajua nimekutana na watu wenye elimu na madaraka makubwa serikalini na wanaamini kwamba Obama zile hotuba zote zinamtoka kichwani.

  ..sasa tangu hapo nikaanza kuwa makini sana. kila nikiangalia speech natafuta teleprompter iko wapi.

  ..sasa kwenye ile hotuba "the dream shall never die" ya Ted Kennedy inabidi uwe makini kidogo kugundua kuwa kulikuwa na telepromter pale.

  NB:

  ..pamoja na hayo lazima ujue kuitumia teleprompter na jinsi ya ku-pose.

  ..ukiwa hujui kusoma vizuri kama Sarah Palin teleprompter haiwezi kukusaidia sana.
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Sep 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wow! Just wow! Lakini unachosema ni kweli. Kwa viongozi wetu hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, sishangai hata kidogo kama wakidhania Obama huwaga anatema off the top of the dome.

  Mtu ambaye alikuwa na uwezo wa kutema ni MLK bana. Jamaa alikuwa ni kichwa kwelikweli. I really admire him.
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  bahati yako hajui kiswahili!
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bambumbile,

  Sikumleta Ted Kennedy ili tuchangue Ujana wake wala matendo yake akiwa kijana. Kila binaadamu, kadri anavyokuwa ndivyo anavyozidi kupevuka.

  Ila kuna tofauti sana ya wale ambao hupatiwa ushauri nao wakaukataa, na wale wanakaa chini na kutafakari ushauri waliopewa, kisha kuufanyia kazi.

  Umekuja kwa ghadhabu nyingi sana na ukali na hata umekosa mwelekeo wa kujenga hoja yako.

  Kwanza unanishambulia kwa kuwa nina theory za Wamarekani na watu Tanznaia wanashindwa kula. Je Tanzania haikujengwa kwa theory?

  Je tulipoachwa na Mkoloni si tayari Demokrasia iliyoko Marekani na Uingereza leo hii, ilikuwepo Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Japani na nchi zote zilizoendelea na zenye Uchumi imara na Demokrasia? Kilitushinda nini kujenga mfumo mzuri wa Kisiasa na Kiungozi ili badala ya kurudi nyuma, tungeendelea kupiga hatua mbele na kurekebisha makovu ya Ukoloni?

  Je Vyama vya Siasa na Uchaguzi wa wakilishi tulivitoa wapi? kama hazikuwa theory za Marekani na Uingereza au Wagiriki ambazo zilishakuwa practical kwa miaka zaidi ya 150 siku tulipopata Uhuru? Kwa nini basi alikuwepo Mtemvu na Chama chake tulikimbilia kumtwez na kumfananisha na Mkoloni kaa si Msaliti kwa kuwa yeye hakuwa TAA/TANU?

  Je tulipokumbatia theory za Mashariki, UChina, Urusi na mkorogo kati ya Ukomunisti na Ujamaa, mbona hukupiga kelele kulalamika bali uliandamana kuunga mkono Azimio la Arusha?

  Kama watu hawana uwezo wa Kula na wanakufa njaa, linahusianaje na Mchungaji au kumtafuta Maverick kama Kenndy au McCain Tanzania?

  Ukosefu wa Chakula ni kutokana na sababu mbili kubwa, ya kwanza ni ya binafsi ya anayeshinda njaa ambayo inatokana na Uvivu, Uzembe, Utegemezi na Ujuvi. Sababu ya pili ambayo ndiyo wengi wanaikimbilia kuhalalisha umasikini na njaa Tanzania ni Serikali, Mvua, Soko, Ajira na Kipato.

  Sasa kama Mnyaturu na ardhi yote aliyonayo, yeye kazi yake ni kutega panzi na kulima hataki wakati kuna mvua, kinapokuja kiangazi ile robo heka yake ya mtama ikanyauka, kwa nini ilaumiwe Serikali au Mchungaji Kishoka?

  Sina Wivu wa Kike, wala wa Kiume. Wivu ni wivu na sina wivu na mtu yeyote kwa sababu yeyote kwa kwa lolote. Simuonei gere mtu yeyote awe kaufuma, kapata au hanazo, wote ni sawa kwandu. Simtegemei mtu aninunulie Bofulo na yule anayekula chapati maji kila siku asubuhi na mayai ya kukaanga hiyo ni staha yake na sioni wivu kwa maana mimi mhogo wa kukaanga ndiyo chapati maji yangu.

  Zitto kugombea Uwenyekiti, Mwakalinga kugombea Ubunge viweje viwe ni vitendo vinavyonikera? Si uamuzi wao binafsi na kwa manufaa yao na mtazamo wao, au kinacho kutatiza na hata kudai tuna Wivu wa Kike ni kile cha kawaida kumhoji mtu nia yake ya kuwa mwakilishi? Mbona Kikwete, Lipumba, Nape, Lowassa nao waliulizwa kwa nini wanataka uongozi?

  Nikianza na Mwakalinga, ni wapi nilipomkashifu au kumbeza Mwakalinga? Kibinafsi nilimuuliza Mwakalinga masuali yafuatayo ninayo yanukuu hapa
  Kisha kabla ya CHADEMA kuboronga na kuonyesha hawafai kutuongoza nikamuuliza kwa nini aliamua kwenda CCM na si TLP, CUF au chama chochote cha Upinzani na si CCM

  Mwakalinga akanijibu
  Nami nikamjibu

  Sikujihusisha na upuuzi uliokuwa humu ndani JF kuhusiana na Mwakalinga na Mwakyembe kwa kuwa tayari mjadala ulishakosa mwelekeo. Wengiwa wana JF wana imani na "Pimbi" Mwakyembe kuwa ni shujaa kutokana na kitu kimoja tu, Richmond, lakini ilipojulikana kuwa Mwakyembe naye ana kampuni yake ya kufua umeme na huku ni Mwanakamati ya Nishati ya BUnge tukasema kakosea kufanya hilo, ndipo sura ya JF ilipoonekana kuwa wamekula kiapo kwa Mtu na si kumpima matendo yake.

  La Zitto, nitalipambanua kwa namna mbili. Kwanza, Zitto alikuwa anataka kugombea Uenyekiti, lakini hajawahi kusema ni vipi alipingana na Mwenyekiti wake na ni vipi ataleta mageuzi Chadema tofauti na Mbowe. Binafsi nilichopigia kelele na kutahamaki ni mchakato mzima wa yeye kutangaza kugombea na hata kuamua kujitoa na nilisema kuwa amefanya kitendo cha Kitoto.

  Najinukuu
  Sasa kama kuhoji mtu ni Wivu wa Kike, basi tukubali kutokukubaliana.

  Nimeleta mfano wa Kenndy nikiwa nimekilenga Chama cha Mapinduzi na zaidi nikiwa nimelenga hili kundi linalojiita la Wapiganaji ndani ya CCM.

  Uchaguzi Mkuu unakuja mwakani na CCM inatafuta mgombea URais, kama kina Mwakyembe, Seleli, Kimaro, Kilango wanaona kuwa Uzalendo wao unavunjwa nguvu kutokana na Rais kutokuwa Imara, kwa nini basi nao wasiwe kama Kennedy na kugombea ndani ya CCM ili wachaguliwe kuwa Mgombea Urais kupitia CCM?

  Na wao wakichukua fomu, nitawauliza Maswali yale yale niliomuliza Mwakalinga na wakilazimishwa wajitoe ili Kikwete awe mtu pekee CCM, nami nitawakung'uta kwa nilichosema kuhusu Zitto na Chadema.

  Tanzania itajengwa na wote, walioko ndani ya nchi na walioko nje ya nchi. Si lazima wote tuwe Dar Es Salaam, Dodoma au Unguja. Tunaweza kuwa kila kona ya nchi hii.

  Si lazima wote tuwe Wanasiasa, Wabunge au Rais ili kuleta maendeleo, tunaweza kuwa Waalimu, Wakulima, Wavuvi, Wahasibu, Machinga, tukiwa kila kona ya Dunia.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inawezekana akapatikana kabisa na pia kuna makosa mengi kama vile binadamu wakawaida kufany kwa wanasiasa kama wakina Zitto lakini wana nafasi kubwa sana katika kufanya na kuweka historia. Kwa CCM labda wote watoke ndani ya CCM ndio wanaweza kusimamia ukweli kwa uhuru wote bila ya kuficha
   
Loading...