Anastahili au kaonewa?

FundiNgoma

Senior Member
Dec 26, 2019
132
264
Kuna jamaa angu tunaishi mtaa mmoja na tunashauriana vitu vingi kama vijana tuliooa tayari

Jamaa yeye kiukweli ni bonge la mchepukaji me simfikii amekuwa na hiyo tabia for a long time mke wake alikuja kugundua wakawa wanagombana sana ndani jamaa anatulia kidogo anaanza tena upya mwisho wake juzi kati hapa jamaa akanambia wife siku hizi simuelewi simu nyingi sana nikamwambia tulia utajua tu

Basi bwana jamaa akaja kufuma meseji za WhatsApp kati ya shemeji (mke wa jamaa) na msela bwana ilikuwa hivi

Msela: nitumie picha zako basi my
Shemeji: akatuma picha
Msela: nimependa hii,(akionesha picha aloipenda)
Shem: Asante my
Msela: tukikutana utakuwa mwepesi
Shemeji: Mmh (inaonekana kama alikuwa akisita fulani maana jamaa alimuhoji sana ndo akamwambia nilikuwa siwezi kufanya ujinga huo japo wewe unanisaliti wazi wazi)

Basi jamaa aliwaka sana hakumpiga akamuuliza tu taratibu kwa nini unafanya hivi?

Shem anasema (huku akilia kwa uchungu na kuomba msamaha) kwamba alifanya vile ili apate faraja baada ya kuona jamaa hana muda nae anapokwenda kazini hata hampigii hamchatishi kama zamani na sio mara moja anakuta meseji za madem wengine wanaochati na jamaa na akimzuia haachi(ni kweli kabisa hiyo)

Hivo huyo jamaa alianza kumtongoza kitambo akaona amkubalie ila kwa sharti, kwamba ye ni mke wa mtu hivo awe na mipaka na anachohitaji yeye ni kampani tu kuondoa upweke na sio sex maana mmewe mbali na yote on bed yuko vzur jamaa akakubaliana na hali wakaanza kuwasiliana maana wapo mbali mbali kidogo ,mawasiliano na mahusiano yalikuwa kama na mwezi hivi ndo jamaa akaja kugundua.

Wakati huo wanawekana sawa kuhusu hiyo kesi me nilikuepo hivo kwa ushauri wangu nikawashauri wasameheane maana chanzo cha mwanamke kucheat ni jamaa hivo wasameheane maisha yaendelee kweli wakasemeheana na jamaa akampigia huyo msela (mchepuko wa shemeji) akamwambia kistaarabu kwamba achana na mke wangu na mikwara mingi na jamaa akaacha kabisa maana aliogopa Sana.

Maisha yakaendelea ila shida kubwa mpaka naandika uzi huu uzi ni kwamba jamaa alinieleza pamoja na kwamba wamesameheana yeye bado anaumia sana moyoni mwake anaona kama mke wake kamfanyia bonge la kosa yani na ana panga kuachana nae maana hiyo ishu haimtoki kichwani mwake.

Naombeni wana JF tumpe ushauri au tumsaidie kisikolojia kila litakaloandikwa hapa nitamuonesha.

Karibuni
 
Yaani kisa kidogo tu hicho ndio waachane? Watoto siku hizi mnaingia kwenye ndoa wakati akili bado za kitoto sana mmejaaliwa maumbo makubwa ila akili za ndoa hamna.
 
Ukiona ndoa imedumu muda mrefu basi jua kuna mmoja wapo kati ya hao wanandoa amejifanya "bwege".

Hivyo mwambie huyo rafiki yako kuwa mwanzoni yeye alipojifanya mwerevu na kumuona mkewe mjinga aelewe kuwa "Mjinga akierevuka mwerevu yu mashakani" kwasasa mwanzoni yeye alijiona mjanja lakini sahv anamuona mkewe mjanja.

Ndoa nyingi sana ni sisi wenyewe wanaume ndio tunaozitia kijiti... wake wetu wanavumilia mengi sana na hadi ukiona wameanza kufanya vitendo hivyo basi tambua uvumilivu wao umefikia kikomo.

Hivyo akiamua ndoa iendelee au wapeane talaka ni juu yake maana ameyasababisha yeye mwenyewe!
 
Back
Top Bottom